Ujue ugonjwa wa ebola

Ujue ugonjwa wa ebola

mtvbase

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2014
Posts
1,243
Reaction score
563
TAARIFA MUHIMU 

Mlipuko unaokuwepo sasa wa Ugonjwa wa Hatari wa Ebola unatuweka kila mmoja wetu katika Hatari.
Tafadhali saidia kuelimisha kwa kutuma msg hii kwa kila mtu unayemjua.

EBOLA NI NINI???

Ni Ugonjwa wa unasababishwa na Kirusi kinachoshambulia mfumo wa damu.
Ni Ugonjwa unaotambulika kwa kisayansi kama HAEMORRAGHIC FEVER.
Kwasababu unasababisha muathirika kutoka damu katika sehemu zote za mwili,na mara nyingi mgonjwa anatokwa damu mpka kufa.

Ebola ni mgonjwa unaenea kwa kiasi kikubwa kwa kuambukiza kwa njia ya kugusa.
Kugusa maji maji ya mwili ya muathirika wa Ugonjwa huu kama vile Damu,Jasho,Mate,Shahawa au maji mengine yatokayo mwili ghairi ya hayo.
Ebola SI UGONJWA UAMBUKIZWAO KWA NJIA YA HEWA KAMA WENGI WANAVYOFIKIRI.

HATARI YAKE
Ni Ugonjwa unaoongoza kuuwa duniani.
Asilimia 90% ya watu wanaopata Ugonjwa huu hupoteza Maisha.

NITAJUAJE KAMA NIMEATHIRIKA

1)Homa kali
2)Maumivu ya kichwa
3)Kuharisha
4)Kuwapiga
5)Uchovu
6)Maumivu ya Misuli na Maungio
6)Maumivu ya Tumbo
7)Kupoteza hamu ya kula

Ikumbukwe hizi ni dalili za Magonjwa mengi si kila Mtu mwenye Dalili hizo au baadhi yake ndio isimwe ana EBOLA

Ukijiona na Dalili hizo wahi haraka kupata matibabu.

TUNAJILINDA VIPI???
1)Osha mikono yako kwa sabuni fanya hivi mara kwa mara.
2)Epuka kushikana shikana na watu kusiko lazima.
3)Safisha mazingira yanayokuzunguka NB Panya pia wanaweza kubeba Ugonjwa huu.
4)Ripoti haraka mara unapojihisi umeambukizwa.
5)Toa Elimu kwa wengine juu ya Ugonjwa huu.
 
Tafadhari fafanua hii dalili ya "kuwapiga"
 
safi kwa taarifa, ila tunaiomba selikali yetu itoe elimu juu ya ugonjwa huu hasa mipakani.
 
Tuwe makini na wageni wanaoingia kutoka Afrika magharibi, wahusika tunawaomba chonde chonde.

Ikiwezekana zuieni hakuna ndege kuingia kutoka kwenye nchi zilizokumbwa na gonjwa hilo hatari
 
Nlifkr hiyo kutoka damu ni internal bleeding.....
 
Tuwe makini na wageni wanaoingia kutoka Afrika magharibi, wahusika tunawaomba chonde chonde.

Ikiwezekana zuieni hakuna ndege kuingia kutoka kwenye nchi zilizokumbwa na gonjwa hilo hatari

Kuna shirika moja limesitisha hiyo i think ni british ila sina uhakika....
 
Dah!ugonjwa mbaya sana huu,Mungu ibariki Tanzania.
Huu ugonjwa ni nashawishika kufikiri janja ya wazungu tu.., Eti wanasema ugonjwa hauna tiba....mbona wao wanajitibu na kuacha waafrika ndo tufe? Anyway, Mungu atatunusuru..
 
Back
Top Bottom