Ujue mti wa Christmas (historia yake)

Ujue mti wa Christmas (historia yake)

johnsonmgaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
2,818
Reaction score
3,731
Leo nitaelezea maana ya mti wa Krismasi, unayo maana gani na pia nitaelezea kuhusu mti unaoitwa (Christmas Tree) hauna uhusiano na siku aliyozaliwa YESU kabisa bali mti huu unao uhusiano na miungu iliyoitwa Tammuz.

Kama nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron uisome kuhusu Father Christmas (neno) huyo ni mzimu wa mtu aliyeitwa Santa Claus ila usome utaelewa vizuri na wewe utaachana na kuweka midoli katika siku ya Christmas, badala ya kuiita hiyo siku ni ya YESU peke yake, mbinu za shetani kuivuruga hii siku ya Christmas na kuwapiga wanadamu upofu wajijue kama wanamsherekea YESU siku hiyo. Shetani aliwateka wakristo wa enzi hizo ambao ni wana dini wakaamua katika siku hiyo maarufu ambayo ni kukumbuka kuzaliwa kwa YESU WA NAZARETI, na kumtukuza MUNGU aliye hai, shetani akawashika wanadamu fahamu zao katika siku hiyo wakaweka mti na mti ukaitwa mti wa Christmas.

Na siri ya mti huu, zamani wapagani waliamini miungu wa mimea na ndio waliamini ndiye mungu wao, sasa wakamuingiza huyo mungu wao wakampamba katika tarehe hiyo ya Christmas ili kuiteka hiyo siku asiabudiwe MUNGU wa kweli na kila anayeweka mti huo wa Krismasi hadi leo ajielewe anaupanda ufalme wa Babeli katika moyo wake na anatekwa katika ulimwengu wa roho anakuwa anampamba mungu Tammuzi au mungu mimea pasipokujua.

Asili ya mti uitwe jina la Christmas tree ilianza Europe, France na Germany, katika biblia hakuna neno mti wa Krismasi, na cha ajabu katika ulimwengu wote watu wanapigwa upofu waliookoka, wapagani, watu wa dini hawaijui siri hii na hata wakiijua hawasemi ukweli wazi wazi ili watu wapone roho zao. Amenituma niwaeleze ukweli peupe peupe. Anayetaka apone atapona, anayekaza shingo majibu atayapata.

Huu mti unaoitwa Christmas tree nataka muelewe kwanza haina ushirikaa kabisa na siku hiyo ya kuzaliwa BWANA YESU WA NAZARETI, ila lengo la mti huo ni niungi inayoitwa Tammuz (miungu ya mimea ambayo watu waliamini ile rangi ya kijani ina nguvu katika mimea enzi hizo) hivyo pasipo kumjua MUNGU wa kweli wakaona eti aliyemzaa YESU ndie miungu ya mimea, wakati ukifikiria wewe peke yako utaona mti hauwezi kumzaa mtu, hata kumuuumba, bali mti unatawaliwa na wanadamu kama viumbe vingine.

Na pia Christmas tree siyo ishara ya kuzaliwa kwa YESU bali ni ishara ya Ashera au mhimili wa miungu ya Tammuz, na shetani alitumia mbinu kubwa mpaka akauteka ulimwengu na hadi leo watu badala ya kumpokea YESU na kufurahia katika mioyo yao wanatekwa na shetani katika ulimwengu wa roho kila aliye na huo mti iwe nyumbani, kanisani, ofisini, hotelini anakuwa amaemuabudu mungu Tammuz, na siku hiyo unakuwa umejiimarisha kwa mungu Tammuz pasipo kujua.

Ila wachawi wanajua na viongozi wa freemason, wanajua na watumishi wa uongo wanajua kabisa, wanafurahia mpigwe upofu mfe roho.
 
8293387398e4c1c1ed209ed426c50cb2.jpg
 
Leo nitaelezea maana ya mti wa Krismasi, unayo maana gani na pia nitaelezea kuhusu mti unaoitwa (Christmas Tree) hauna uhusiano na siku aliyozaliwa YESU kabisa bali mti huu unao uhusiano na miungu iliyoitwa Tammuz. Kama nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron uisome kuhusu Father Christmas (neno) huyo ni mzimu wa mtu aliyeitwa Santa Claus ila usome utaelewa vizuri na wewe utaachana na kuweka midoli katika siku ya Christmas, badala ya kuiita hiyo siku ni ya YESU peke yake, mbinu za shetani kuivuruga hii siku ya Christmas na kuwapiga wanadamu upofu wajijue kama wanamsherekea YESU siku hiyo. Shetani aliwateka wakristo wa enzi hizo ambao ni wana dini wakaamua katika siku hiyo maarufu ambayo ni kukumbuka kuzaliwa kwa YESU WA NAZARETI, na kumtukuza MUNGU aliye hai, shetani akawashika wanadamu fahamu zao katika siku hiyo wakaweka mti na mti ukaitwa mti wa Christmas. Na siri ya mti huu, zamani wapagani waliamini miungu wa mimea na ndio waliamini ndiye mungu wao, sasa wakamuingiza huyo mungu wao wakampamba katika tarehe hiyo ya Christmas ili kuiteka hiyo siku asiabudiwe MUNGU wa kweli na kila anayeweka mti huo wa Krismasi hadi leo ajielewe anaupanda ufalme wa Babeli katika moyo wake na anatekwa katika ulimwengu wa roho anakuwa anampamba mungu Tammuzi au mungu mimea pasipokujua.
Asili ya mti uitwe jina la Christmas tree ilianza Europe, France na Germany, katika biblia hakuna neno mti wa Krismasi, na cha ajabu katika ulimwengu wote watu wanapigwa upofu waliookoka, wapagani, watu wa dini hawaijui siri hii na hata wakiijua hawasemi ukweli wazi wazi ili watu wapone roho zao. Amenituma niwaeleze ukweli peupe peupe. Anayetaka apone atapona, anayekaza shingo majibu atayapata. Huu mti unaoitwa Christmas tree nataka muelewe kwanza haina ushirikaa kabisa na siku hiyo ya kuzaliwa BWANA YESU WA NAZARETI, ila lengo la mti huo ni niungi inayoitwa Tammuz (miungu ya mimea ambayo watu waliamini ile rangi ya kijani ina nguvu katika mimea enzi hizo) hivyo pasipo kumjua MUNGU wa kweli wakaona eti aliyemzaa YESU ndie miungu ya mimea, wakati ukifikiria wewe peke yako utaona mti hauwezi kumzaa mtu, hata kumuuumba, bali mti unatawaliwa na wanadamu kama viumbe vingine. Na pia Christmas tree siyo ishara ya kuzaliwa kwa YESU bali ni ishara ya Ashera au mhimili wa miungu ya Tammuz, na shetani alitumia mbinu kubwa mpaka akauteka ulimwengu na hadi leo watu badala ya kumpokea YESU na kufurahia katika mioyo yao wanatekwa na shetani katika ulimwengu wa roho kila aliye na huo mti iwe nyumbani, kanisani, ofisini, hotelini anakuwa amaemuabudu mungu Tammuz, na siku hiyo unakuwa umejiimarisha kwa mungu Tammuz pasipo kujua. Ila wachawi wanajua na viongozi wa freemason, wanajua na watumishi wa uongo wanajua kabisa, wanafurahia mpigwe upofu mfe roho.
Kakobe kapamba mitatu mikuubwaaa inangaaa hyo
 
Kama unataka arguments za kidini, unapoteza muda wako... fanya kazi zingine
 
Mbona hamna hata reference...hamna visa vinavyothibitisha hakuna quote kutoka walau hata kwenye kigazeti cha udaku....sasa unadhani kuna great thinker anayeweza amini mawazo tu kutoka akili mwako pasipo evidence wewe vipi..??
 
Kakobe kapamba mitatu mikuubwaaa inangaaa hyo
Pengine hajui au anajua,,
Hata mimi cjui nilipokuwa natafuta kwenye mitandao kwann huu mti unahusishwa na yesu ikiwa hakuna andiko ktk biblia? ndo nikajua
 
Mbona hamna hata reference...hamna visa vinavyothibitisha hakuna quote kutoka walau hata kwenye kigazeti cha udaku....sasa unadhani kuna great thinker anayeweza amini mawazo tu kutoka akili mwako pasipo evidence wewe vipi..??
Kuna andiko katka biblia linalohusu mti huu?
 
Kwa hiyo soluhisho?
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba unisamehe niliabudu miungu ya mimea bila kujua au kwa kujua narudi kwako MUNGU WA KWELI nisamehe nioshe kwa damu ya mwanao YESU WA NAZARETI, najitenga na miungu yote, sishiriki tena kuita mti uitwe jina lla Christmas wala kuinunua, najitenga na mapokeo ya miti hiyo na maroho yote. Nisaidie nikuabudu wewe katika roho siku ya Christmas na siku zote nikusifu wewe peke yako. Amen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom