Ujio wa Wema CHADEMA ni drama nyingine.?

Ujio wa Wema CHADEMA ni drama nyingine.?

vitus juma

Member
Joined
May 20, 2015
Posts
98
Reaction score
43
Kuna watu wengi sana wametokea kukosoa Ujio wa Wema ndani ya CHADEMA huku baadhi pia wakimuunga mkono lakini kubwa zaidi wengine imefika hatua kuilaumu chadema kumpokea kwa mbwembwe dada yetu Wema Sepetu.

Wanaoponda uamuzi huo hawampondi Wema kama Wema bali wanaponda ile nafasi yake yaani Usanii wake na wanapomponda na kumdharau Wema inamaana pia wanaidharau tasnia yake hii inamaana katika nchi hii kunamakundi yakijamii yanahaki na heshima kuliko mengine.

Nashangaa sana ni Kwanini jamii inadharau kada ya wasanii kiasi hiki hasa mmoja Wapo wawasanii anapojiingiza kwenye Siasa wanasahau Siasa inagusa kada zote za Wakulima, wavuvi, wasanii, watoto wa mitaani, wauza mitumba na makundi yote ya kijamii huguswa na Siasa.

Mi kivyangu naona CHADEMA kumchukua Wema imelamba dume, imepata faida na iendelee kuwavutia wasanii kwani hii nchi ni ya wote nawasihi CHADEMA msibague mtu hata akiwa mzibua vyoo mbebeni kwani chama cha siasa kinahitaji watu na watu wenyewe ni hawa hawa akina Wema na CHADEMA ili kiwe na wanachama lazima kiwachukue toka CCM chama tawala.

Na lengo la chama chochote ni kushika dola chadema haiwezi kushika dola kama haitawekeza nguvu zake na mbinu za kubeba wanachama toka ccm hao wanaoitwa oil chafu wabebeni na uchafu wao siku ya kupiga kura ndo hujulikana oil chafu hubeba kadi chafu ya kupigia kura au nyeupe?, nyie chadema Siasa yenu yote ili mtimize malengo ya kuwa chama dola nikuwabeba wanaccm bila wanaccm hamtapata wanachama.

Na wanao wadharau kumchukua Wema waulizeni kwenye mikutano ya kisiasa ccm huwatumia wakina nani si hao hao wasanii wa kada ya Wema mbona sijawahi ona ccm inazunguka namafundi selemara, Wakulima au wavuvi nchi nzima wakati wa kampeni zaidi ya akina Wema.

Mbona kwenye kikao chao cha kumchagua mwenyekiti pale dodoma waliwaalika wasanii na wakajitambulisha na wakajazana kupiga nao picha mbona hawakuwaalika madereva boda boda pale. Ni Sku ile pale dodoma kwenye ukumbi wa ccm walimpa maick Jackline wolper akawatangazia wajumbe wa mkutano kuwa amehamia ccm rasmi toka chadema na wakampigia makofi Kwanini hawakumpa nafasi ile mfugaji wa uko Igomaa chunya atangaze amehama ila wakampa msanii?

Kama wanacheka Ujio wa Wema kama msanii, Kwanini waliwaalika wasanii pale ikulu kuwapa Shukrani kwa mchango wao? Mbona hawakuwaita wavuvi wa rufiji pale ikulu zaidi ya wasanii?.

CHADEMA bebeni hao wasanii wanamchango mkubwa mikutano ya kampeni ya wadau haifanyiki bila hao ndani ya ccm DIAMOND anaushawishi wakujaza uwanja kuliko mtu yeyote.

USHAURI WANGU
Mrejesheni Zitto na Dr Slaa kundini haraka huu ndo muda muafaka wakuwepo kwao kuliko wowote ule.
By vitus Juma.
 
Huu ndiyo ukweli!! Ambao kambi ya wakina MsemajiUkweli hawapendi kuusikia!! Tupo tunamnyorosha kule uwani! Ameanzisha ka thread uchwara
 
Wema kasahulisha wote kuhusu ngada, kweli chadema ni kama toilet paper, unafuta uchafu na kuitupa.
 
ujio wa wema chadema hauna tofauti na mwanaume ambaye hapewi penzi na mwanamke hadi atoe mshiko, na bado mwanaume huyo anaona ni sawa tu tena anafurahi!
jiulize kwann wema atimkie chadema baada ya kupata dhahma ya bangi.....kwamba kama sio bangi angeendelea kubaki huko ccm.
 
Back
Top Bottom