nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,689
nameless girl Kwa hiyo sasa baada ya Mwandishi Ben R. Mtobwa kututoka, wewe ndio umerithi mikoba yake? Na unatuhakikishiaje kama hautamchakachua Joram Kiango tuliyezoea kumsoma enzi zile tukiwa sekondari tukijikusanya kikundi wakati wa free period na break huku mmoja akitusomea?
hili ni tangazo la biashara je umelipia?
Hali zenu wana JF?Kwa wale wanaopenda kusoma riwaya, napenda kuchukua fursa hii kuwatangazia ujio wa kitabu cha MIKATABA YA KISHETANI kilichoandikwa na Marehemu Ben R. Mtobwa. Kitabu hiki kinatarajiwa kutoka tarehe 1/1/2015. Riwaya hii ni mlolongo wa harakati za Joram Kiango ambavyo viliwahi kutoka kabla ya kifo cha mwandishi Ben R. Mtobwa. Baadhi ya mlolongo wa riwaya hizo ni pamoja na Tutarudi na Roho Zetu? Salamu Toka Kuzimu, Mtambo wa Mauti, Mikononi mwa Nunda na vingine vingi. Kitabu hiki kitauzwa kwa shilingi elfu kumi tu za kitanzania.
Napenda kuchukua fursa hii pia, kumshukuru saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana The Boss kwa kunishika mkono pale nilipokwama, na wale wote walionisaidia kwa jambo lolote kuhusiana na utoaji wa kitabu hiki.
N.B: Taarifa ya mawasiliano na mahala ambapo kitapatikana kitabu hiki, naomba niitoe mara tu kitabu hiki kitakapotoka otherwise PM itahusika.
Asanteni.
Mpwa wangu hongera sana kwa kazi nzuri, ila sijaelewa kitu hapa, you mean unazalisha nakala nyingine au ndio unakichapisha? Please mimi nitakua mteja wako, Vitavbu vyake vinanikumbusha mbali sana
Hiyo ni kazi yake, mimi sio mwandishi aliiandika kabla hajafariki...
Ok, asante kwa ufafanuzi huo
Karibu...
Mpwa....
Hiki ni kitabu kipya ambacho Marehemu alikiandika kabla mauti hayajamfika ila kwa bahati mbaya sana hakuweza kukitoa though alikuwa kwenye hatua za mwisho za kutoa kitabu hiki.
Nilichofanya mimi ni kuhangaikia kuchapwa kwa kitabu hiki tu...
Hope umenielewa mpwa.
Nameless, je naweza kupata vitabu vya Ben vyote alivyotunga?
No way aisee hakikisha panapomajaaliwa unanipatia copy yake. Kwa pesa yoyote Ile, thanks
Naomba haya maelezo yako yawepo kwenye thread yako hapo juu ili kuondoa utata. Thanks so much thanks
Vipi katika uzoefu wako wa vitabu je naweza kupata vile vya alfu lela ulela? Nashkuru.