Ujinga wetu Watanzania katika baadhi ya matendo yetu

Ujinga wetu Watanzania katika baadhi ya matendo yetu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Watanzania tunaweza kuwa tunauana wenyewe kwa wenyewe bila kujua kwa tamaa za kupata hela zaidi kwenye bidhaa nyingi.

Tunajiua kwa kuharibu soko, pia tunajiua kwa madhara ya bidhaa na huduma feki kwa kuchakachuaa.

Ukienda buchani, utauziwa nyama ya leo, ukichanganyiwa kwa siri na kiasi ya jana. Ukienda kununua mpunga unaweza kuuziwa na mchanganyiko wa pumba. Ukinunuaviungo vya pilau utachanganyiwa na vitu feki, hkinunua dawa za binadamu usipopata feki utapewa zilizopita muda,bukienda kununua tiketi ya basi ziendazo mkoani,unaweza kuoneshwa basi jipya,lakini kesho ukasafirishwa na basi la zamani

Ukifikia baadhi ya nyumba za wageni, ukitoka ukaacha mizigo yako, ukikabidhi funguo kama sheria inavyotaka,unaweza kuta wamepekua mizigo yako. Ukiwa safarini, unaweza kuuziwa nyama ya kuku au ya mnyama kama ng'ombe ya jana au sio nyama halisi, mfano badala ya kuku ukauziwa ndege pori.

Ukienda soko la kuku unaweza kuuziwa kuku waliokufa kwa matatizo,kama magonjwa ama mambo mengine, mara nyingi tumekula nyama za wanyama waliokufa kwa magonjwa bila ssis kujua,badala ya kuvifukia kwa amri za mabwana afya, watu wamekua wakivileta sokoni kwa siri

Mambo ni mengi sana tunafanyiana sisi watanzania wenyewe kwa wenyewe bila kujali hivyo vitu au huduma atavila au ataipata mwanao,mama yako baba yako,kaka yako,dada yako,ndugu yako,rafiki yako n.k
tubadilike ,tutafute pesa kwa nji halali,wema na uungwana.
 
Kila kitu ni ujanja ujanja tu, na umeshakuwa utamaduni.
 
Back
Top Bottom