Hivi vitu niliviona Makambako Mji Mwema kitambo sana mi mwenyewe nilikuwa bwana mdogo mno nafikiri ilikuwa '89. Jamaa walikuwa wanabebea madumu ya maji halafu wakifika kwenye mteremko wanajiachia kinoma
Mkuu ni kweli kabisa nami nimevipanda nikiwa makambako maeneo hayo hayo ya mjimwema. Kulikuwa na vijana wanazitengeneza hatari. Na tairi wanavalisha hii mipira ya baikeli halafu inawekwa na break. Basi break ikikatika na upo kwenye mteremko bora uruke