Ujerumani yapiga marufuku matumizi ya iPhone

Ujerumani yapiga marufuku matumizi ya iPhone

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
Ujerumaini imeamua kupiga marufuku simu zote za "smart" aina ya iPhone baada ya afisa mmoja wa zamani wa kijasusi wa Marekani Edward Snowden kufichua kuwa, simu aina hiyo zilitumika kufanyia ujasusi mazungumzo ya simu ya viongozi wa nchi 35 duniani.

Kabla ya hapo ilibainika kuwa, Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA ulikuwa unadoya na kudukua mazungumzo ya simu ya Kansela wa Ujerumaini, Angela Merkel tangu mwaka 2002, ujasusi ambao umeikasirisha mno Bundestag (bunge la Ujerumani).
Huku hayo yakiripotiwa, wabunge wa vyama viwili vikuu katika bunge la Ujerumani wamepasisha sheria inayowapiga marufuku wabunge wa nchi hiyo na viongozi wote wa ngazi za juu serikalini kutumia simu ambazo hazina kinga ya kufanyiwa ujasusi yaani simu zisizo na chujio la kudhibiti mawasiliano na barua.
Imebainika kuwa machujio hayo hayawezi kufanya kazi kwenye simu za "smart" aina iPhone zinazotengenezwa na shirika la Apple la Marekani na hivyo kuwapiga marufuku wabunge na viongozi wa ngazi za juu wa Ujerumaini kutumia simu hizo maarufu.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kutofanya kazi programu hizo zinazokusudiwa na wabunge wa Ujerumaini ambazo zinachuja mazungumzo na barua katika simu ya iPhone kumetumiwa kama kisingizio tu bali ukweli wa mambo ni kuwa shirika la Apple lina makubaliano ya siri na Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA yanayoruhusu mawasiliano yote ya simu za iPhone na data za simu hizo pamoja na vifaa vingine vya Apple zikiwemo kompyuta zipitishwe kwenye chujio linalowasilisha taarifa zake moja kwa moja kwa wakala huo wa kijasusi wa Marekani.

source: http://kiswahili.irib.ir/habari/mch...ujerumaini-yapiga-marufuku-matumizi-ya-iphone
 
Kwa wenzetu Privacy ni kitu muhimu sana katika uhai na maisha ya kila siku.... Haki yao!! ukichokoza yatakukuta.
 
uyo dogo amelipa taifa lake asara sana, inasikitisha kwa mmarekani kufanyia nchi yake yote hali,
 
sisi watuache tu na iPhone zetu maana kipindi kile Obama amekuja tulimwachia ikulu yote ikawa ya kwao nina imani wanatujua hadi ndani
 
Sisi tuliwakabidhi ikulu yote nini iphone bana!!

eti iPhone wakati kwetu wamefika hadi chumbani kwa mkuu wa kaya na nina mashaka kama hawajaacha kamera zao kule
 
Nchi tepetepe kama yetu kila kitu ni sawa tu, hata dawa feki tunabishana na wauzaji wanashinda kwa logistical errors tu za kisheria
 
sasa mbona akina sie ndio hatuna hata cha kuficha. good for them (the super powers).
 
Hawa wajerumani nao siemens zao wameweka wapi??? waendelee kukohoa nasisi tunaponea humo humo
 
...wakusanye hizo Apple zao,walizozisusa,watuletee tu Bongo,sisi hatuna hiyana,kama pipa la taka tu..
 
Aaah, wote ni wale wale tu. Watajuana wenyewe, sisi na rais wetu hatuna cha kuficha
 
Back
Top Bottom