Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Balozi Waechter akina na Naibu Spika Tulia Ackson, Mjini Tukuyu, Mbeya.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter, jana akiwa mkoani Mbeya ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza Sera za Uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli kufanikisha Sera ya Viwanda.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila jana baada ya kuwa na mazungumzo na Balozi Waechter ofisini kwake, alisema kuwa, Ujerumani inaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano na kwamba itaendelea kutoa msaada kupitia sekta mbalimbali kikiwemo kilimo. Alisema, Balozi alimwahidi kushawishi Nchi yake kuja kujenga kiwanda cha mbolea mkoani Mbeya.
Aidha, alisema kuwa, "Balozi Waechter amempongeza Rais Magufuli kwa kupiga marufuku safari za nje ya Nchi zisizokuwa na tija kwa Taifa."
Chalamila alisema kuwa, "Serikali ya Ujerumani imekuwa ikimtumia mwaliko Rais Magufuli wa kwenda nchini humo lakini amekuwa akigoma na kuwaeleza kuwa, hadi aiweke sawa Nchi yake."
Balozi Waechter amepongeza amani iliyopo nchini na kusihi kuendelea kuienzi kwani ndiyo sababu kubwa inayowashawishi kuja kuwekeza hapa nchini.
Balozi wa Ujerumani akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mahiga wakati wa Uzinduzi wa Liaison Office, jijini Dodoma.
Balozi akiwa na Wawekezaji wa Kijerumani, Kampuni kubwa la BASF, ambao wameanzisha Ofisi zao Tanzania.