Ujerumani ni "Shamba la Bibi", na sisi tunangoja nini?

Ujerumani ni "Shamba la Bibi", na sisi tunangoja nini?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Nchi ya Ujerumani iliyoko Bara la Ulaya imekuwa ni kama shamba la Bibi, kila Mtu anadai fedha na analipwa!
Kuanzia Israeli wanaodai hela na wanalipwa mpaka leo ktkna na madhambi ya A.Hitler, Wanamibia walidai hela kutokana na Ukoloni wa Wajerumani ambapo waherero wengi waliuawa, sasa hivi hata nchi iliyofilisika ya Ugiriki ambayo ina madeni kibao wanataka pia walipwe na nchi hiyo ya Ujerumani kwa kuwa waklati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Hitler aliingia huko na kusababisha madhara, sasa kama kila Mtu anaidai nchi hiyo na wanalipa sisi tunangoja nini kudai na kujipatia mabilioni?

Mbona tuna kila sababu kuanzia kuuliwa kwa watu wa Lilinga, mpaka kwenye vita ya maji maji na Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ambapo Askari wetu walishiriki chini ya Mwamvuli wa Mjerumani hivyo tunaweza kuanzisha madai hawa Jamaa wana fwedha nyingi sana ndiyo matajiri wakubwa Ulaya hivyo watatulipa Tu!
 
Kwani namba kukumbushwa vita ya pili tulipigana chini ya mjerumani au muingereza? Babu yangu alipigana hiyo vita huko Barma chini ya muingereza sasa unaposema ni mjerumani nakua sielewi
 
Kwani namba kukumbushwa vita ya pili tulipigana chini ya mjerumani au muingereza? Babu yangu alipigana hiyo vita huko Barma chini ya muingereza sasa unaposema ni mjerumani nakua sielewi

Nimeongelea Vita Kuu ya kwanza na Siyo ya Pili nimesha sahihisha!
 
china nao wanavuta mpnga us kupitia lile atomic bomb
 
Hata tukilipwa zitanufaisha familia ya watu 5 tu kati ya wa Tzania mi 40
 
Safi sana ni wazo zuri,natamani viongozi wetu wangekuwa Creative kama ww nadhani tungekuwa mbali kiuchumi!bahati mbaya pamoja Kuwa na bahari,Maziwa,Mito,Ardhi,Misitu,Madini,Gas,Mafuta,bado ni OMBAOMBA najuta kuzaliwa TZ
 
Hiyo hela pengine tulishafidiwa kitambo ila ilisha pigwa!
 
Back
Top Bottom