Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato: Serikali yatangaza tenda

Hakuna namna lazima uwanja ujengwe tu,wewe shida yako nini sasa Chato ni nyumbani kwa Rais lazima Huduma muhimu zote zipatikane hakuna namna ni lazima.

Rais hawezi kuishi kama RAIA wengine wa kawaida ana mambo yake ya msingi ktk kutekeleza majukumu yake akiwa kazini na akiwa mapumziko ni nyumbani kwake Chato.

Ndiyo Serikali makini inavyojali viongozi wake.
Tumekosa vipaumbele
 
Tumekosa vipaumbele
Vipaumbele vipo jamani mbona mmekazana tu na uwanja wa Chato kama vile ni kosa la uhaini.

Maamuzi sahihi nyumbani kwa Rais lazima kuwe na njia muhimu za usafiri especially ya anga.
 
Kama unajengwa chato tatizo n nn huyo n rais lazima mazingira yanayomzunguka yawe sala na rahisi kuyafikia pale inapobidi unataka akiwa leave aendeshwe na gari hadi chato usalama wake itakuwaje pili huo uwanja utakuwa n kwa manufaa yake au wananchi wanaotaka kupata huduma kwenye maeneo hayo kingine ujue chato ipo geita au ukanda wa migodi hvyo itakuwa rahisi kuwakaribisha na kuwalazimisha wenye migodi kutumia uwanja huo kwasababu ya usalama wa madini yetu na kuacha kutumia viwanja vyao binafsi ambavyo wanatorosha madini kila kukicha.

Saa zingine tuwe tunafiri kichadema na kiccm ili kupata maana njema na sahihi
 
Nyumbani kwa Rais Hakuwezi tu kufanana na RAIA wengine eti kisa Demokrasia haiwezekani hizo siasa za wakati ule sio za Leo ndugu jua hilo.

Rais atajengewa tu compound yenye hadhi yake ukiwepo na huo uwanja wa ndege hakuna namna.

Lazima Rais apate heshima ya hadhi yake.Hata wewe ukichaguliwa utafanyiwa hayo ni haki yako kama Rais huwezi kuishi kiajabu ajabu tu hata hueleweki.haiwezekani.Lazima uwe na makazi bora.

Nashukuru kaka kwa maelezi yako, hakuna mwenye shida na compound yenye hadhi ya rais bali ni uwanja mkubwa utakaoligharimu taifa wakati utakuwa ni wa matumizi ya muda tu. Naomba niulize ujenzi wa kiwango hicho cha uwanja uko kikatiba, kisheria ana kikanuni? Isije ikawa wapambe mlijitengenezea mazingira ya 10% maana ndio zenu.

Hivi mnapokaaga kwenye vikao vya kukitukuza cheo cha rais mpaka kupitisha miradi ya hivi huwa hamuoni aibu wangalau hasa ukizingatia huduma duni za hospital, maji, umeme nk kwa walio wengi? Ulikiona kilichomkuta Gaddaf na bado alikuwa na hivyo viwanja vya kiwango cha juu tu maana mnajifichia kwenye kisingizio cha usalama? Kwenye hili tuwaambie ukweli tu hamjafanya sawa, na ninaomba nieleweke sisemi hivi kupinga hicho cha Magufuli bali nasema kwa marais wote wajao wajengeeni viwanja vya kiasi kulingana na atakapopenda kuishi kiwe kidogo tu.
 
Tusiweke mada ili tu kubeza kazi za Rais.Wilaya nyingi tu zina viwanda vya ndege tena vikubwa mfano Wilaya ya Kilombero mji wa Ifakara kuna uwanja mkubwa tu na ndege za ukubwa wa kati huwa zinatua.

Kwanini Chato kama Wilaya tena anakotoka Rais uwanja usijengwe,huo ni ufinyu wa mawazo kwa sisi watanzania.Rais anaenda kupumzika,anaenda kikazi Chato,lakini Wanainchi wa Chato wana haki ya kuwa na uwanja pia.

Ni Aibu anakotoka Rais eti kusiwe na uwanja wa ndege,Rais akipata dharura yoyote ile akiwa mapumziko Chato watu wa Usalama watamtoaje hapo Chato nyumbani???

Matatizo ya Huduma ya afya siyo ya Leo wa Jana na hayawezi kuisha over the night Serikali itaendelea kuyatatua kadri inavyoweza.
Kweli akili hii ni ya Jembe na Nyundo,wenzetu wanatumia trekta wewe jembe,msumbari wanang'olea nyundo ya seremala ww unatumia ya kubomolea vibanda vya machinga kazi unayo kufikia maendeleo. Kilimo kwanza balaa la njaa. Bora angejenga Hosptal ya rufaa na kuweka T. Scan au Shule ya A kubwa na ya kisasa ili kutengeneza fursa kwa wanachato. Hii unainyima Geita taa za barabarani unapeleka Chato,badala ya kuweka mizani Bwanga unapeleka Chato. Na bado bandari tutaiamisha Mwanza na kuipeleka Chato ngoja tulete Meli.
 
Tuwe na malalamiko ya kikweli jamani ila hizi chuki binafsi sio njema,sioni kama kuna tabu kwa rais kujenga kiwanja cha ndege chato je kama angejenga katika mkoa mwingine badala ya chato tungemsifia au ? Tupazeni sauti katika mambo ya msingi ndio kulisaidia taifa letu lkn chuki hazita tusaidia kitu.Asanteni
 
M
Nashukuru kaka kwa maelezi yako, hakuna mwenye shida na compound yenye hadhi ya rais bali ni uwanja mkubwa utakaoligharimu taifa wakati utakuwa ni wa matumizi ya muda tu. Naomba niulize ujenzi wa kiwango hicho cha uwanja uko kikatiba, kisheria ana kikanuni? Isije ikawa wapambe mlijitengenezea mazingira ya 10% maana ndio zenu.

Hivi mnapokaaga kwenye vikao vya kukitukuza cheo cha rais mpaka kupitisha miradi ya hivi huwa hamuoni aibu wangalau hasa ukizingatia huduma duni za hospital, maji, umeme nk kwa walio wengi? Ulikiona kilichomkuta Gaddaf na bado alikuwa na hivyo viwanja vya kiwango cha juu tu maana mnajifichia kwenye kisingizio cha usalama? Kwenye hili tuwaambie ukweli tu hamjafanya sawa, na ninaomba nieleweke sisemi hivi kupinga hicho cha Magufuli bali nasema kwa marais wote wajao wajengeeni viwanja vya kiasi kulingana na atakapopenda kuishi kiwe kidogo tu.
Mimi nakuelewa sana ila don't compare our President na tawala zingine kama ulivyozitaja kila nchi na syndicate zake.You don't know why Gaddafi killed by his own people!!?

Tanzania tuna bahati moja kubwa sana Serikali iko makini sana na external forces/ interest.

Pamoja na matatizo ya maji,umeme,dawa na mengine lakini si kigezo cha kutoamua kufanya maamuzi mengine in between.

Process ya development ni step by step lazima tukubali tu.

Na kama tukiendelea kulalamika tu kila kukicha basi tutafika mahali hakuna kitakachofanyika maana kila jambo likifanyika utaulizwa huku hakuna maji,sijui hakuna shule then hatutafika.

Ethiopian airline unaona Leo iko dunia mzima ni maamuzi magumu ya viongozi kuipunguzia Wizara ya afya na kilimo bajeti then wakanunua ndege.

Maendeleo hayaji tu kirahisi you have to sweat a bit
 
Hii habari akiiona anatamani Jf ifutwe kabisa lakini kashachelewa, hii dhambi ya ubaguzi na laana ya kula rambi rambi sina hakika kama atasalimika mtu ..to hell is for ...
 
BIG UP MAGUFULI KWA KUJALI ZAIDI UWANJA CHATO KULIKO elimu ya watoto wetu, wafanyakazi wa serikali, madawa hospitalin. NI HERI WATANZANIA WAWE NA MAISHA MAGUMU LAKIN UWANJA WA NDEGE UJENGWE CHATO TU.
Maisha magumu tz yameanza leo baada ya kuanza kujengwa uwanja?
 
Tumeingia cha kike wenyewe tukubali kuchuchumaa,, wajenge tuu. Wakitaka na bandari sawa, kambi ya jeshi ok, chuo kikuu yote sawa. Maneno maneno ya nini sasa?
Ni sawa na unapata ujauzito unashangaa wakati ulikubali mwenyewe kukutana kimwili na wanaume.
Tumeingia choo cha kike kivipi kwa kumchagua ama?
 
Baba wa Taifa hakujenga uwanja Butiama..kwa sasa tuna viongozi wabinafsi sana..kwa nini huo uwanja haukujengwa Makao Makuu ya Mkoa pale Geita?
Baba wa taifa alitawala lini? Unashindwa hata kutofautisha nyakati? Kwahiyo aendelee kulalia kitanda cha baba wa taifa atumie gari la baba wa taifa na vifaa vya ofisi atumie vya baba wa taifa alivyoviacha ikulu?
 
Tusiweke mada ili tu kubeza kazi za Rais.Wilaya nyingi tu zina viwanda vya ndege tena vikubwa mfano Wilaya ya Kilombero mji wa Ifakara kuna uwanja mkubwa tu na ndege za ukubwa wa kati huwa zinatua.

Kwanini Chato kama Wilaya tena anakotoka Rais uwanja usijengwe,huo ni ufinyu wa mawazo kwa sisi watanzania.Rais anaenda kupumzika,anaenda kikazi Chato,lakini Wanainchi wa Chato wana haki ya kuwa na uwanja pia.

Ni Aibu anakotoka Rais eti kusiwe na uwanja wa ndege,Rais akipata dharura yoyote ile akiwa mapumziko Chato watu wa Usalama watamtoaje hapo Chato nyumbani???

Matatizo ya Huduma ya afya siyo ya Leo wa Jana na hayawezi kuisha over the night Serikali itaendelea kuyatatua kadri inavyoweza.

Butiama international airport.
 
Hata kila kijiji kukijengwa Airport, mi binafsi sina shida; shida inakuja hivi: Je ni kipaumbele kwa Taifa kuwa na uwanja kila kijiji/wilaya tena wa kiwango cha ukubwa huo?
Sio kipaumbele bali ni mpango wa kawaida tu kwani kila kitu kipaumbele? Kama ni hivyo bajeti zote za wizara zina miradi ya maendeleo na ya kijamii ndani yake yote hiyo ni kipaumbele?
 
Nyerere aliondoa akaacha uwanja wa ndege wa Musoma. I thought uwanja ule ungeendelezwa ili kurahisisha safari za watalii mbuga za Serengeti, Ngorongoro na Manyara. Huko kuna vyanzo anuai vya mapato. Huko Chato sijui kuna nn hadi uwanja ujengwe???
Kuna rais wa nchi
 
Yatupasa tuache ukipofu na tuache wendawazimu wa kuamini ni lazima Rais ajenge uwanja wa ndege nyumbani kwake anakotoka.Tukumbuke mwisho wa siku yule ni Rais wa Tanzania.Leo hii nipo Butiama hapa,hakuna uwanja wa ndege zaidi ya ule wa musoma.Mwalimu ndiye aliyelikomboa taifa hili na kama angelitanguliza ukwao ikulu ingekuwa Dar?
Tuache wendawazimu wa kusifia kila kinachofanyika mwisho wa siku tukiendelea hivyo Rais atakuja kuchaguliwa kikabila na kikanda ili alete maendeleo anakotoka.
Hakika sisiemu ni janga kwa taifa la Tanzania coz inaanza kutubagua kwa ukanda over.
Uwanja haujajengwa kwa sab ni kwake umejengwa kwa sab unastahili kujengwa kama viwanja vilivyopo katika wilaya zingine nchini. Kwakuwa chato ametokea rais basi kusiendelezwe kwa namna yoyote simply because ametokea rais? Hizo wilaya zingine nchini ambazo zina maendeleo makubwa kuna rais aliyetokea huko?
 
Back
Top Bottom