Ujenzi wa mitambo ya kufua umeme kwenye Bwawa la Nyerere na mabadiliko ya tabia ya nchi

Benjamin10

JF-Expert Member
Dec 31, 2016
389
553
Wakuu habarini za mchana.

Hivi karibuni kuna taarifa zimetolewa na shirika la umeme kua kutakua na upungufu wa umeme.

Hii ni kutokana na ukame wa muda mrefu uliosababisha maji kupungua katika mabwawa yanayozalisha umeme.

Sasa hoja yangu ni kuwa, kwanini tunaendelea kumwaga mapesa mengi kuendelea na mradi wa kutumia maji kuzalisha umeme ingawaje tunajua tabia ya nchi ya sasa imebadilika yaani haieleweki na mvua zimekua ni haba?

Au hilo bwawa lenyewe haliathiriwi na mabadiliko ya tabia ya nchi?

Kwanini tusjikite zaidi kwenye uzalishaji usiotegemea mabadiliko ya kimazingira? Kama gesi,joto ardhi.. upepo..

Naomba kuwasilisha hoja!
 
Hapa unapaswa ujuwe sayansi iliopo kwenye kujenga mabwawa ya kuzalisha umeme ndio utaweza kuwa na jibu la swali lako, na ikifikia kipindi kuwa huo mto unaoleta maji kwenye bwawa umekauka kabisa, basi ujuwe binadamu na viumbe wengi watakuwa wamekufa kwa kukosa maji.
 
Hawa ndio waramba asali na lengo lao kuu ni kuachana na hilo bwawa la Nyerere na kuanza kuramba asali za gas na makaa ya mawe. Nchi ngumu sana hii na miafrika ndivyo tulivyo.
 
Back
Top Bottom