Ujenzi wa misingi ya uwekeziji - Sehemu ya 2

gema

Member
May 26, 2011
25
20
Tunaendelea na Ujenzi wa Miundombinu ya uwekezaji:

Ili kujua ni aina gani ya miundombinu na yenye kiwango gani unatakiwa kuijenga ni lazima kwanza ujue ni uwekezaji wa ukubwa gani unaouhitaji hapo baadaye na ni aina gani ya sekta unayotaka kuwekeza, kama ilivyo kwa ujenzi wa majengo makubwa msingi ndio unao amua urefu na ukubwa wa jengo kadhalika katika uwekezaji miundombinu unayoiandaa tangu mwanzo ndio inayoamua ukubwa wa miradi unayoikusudia.

Jana nilipata nafasi ya kuitazama vizuri treni iliyokuwa ikipita umbali kama mita tatu hivi toka nilipokuwa nikajuliza maswali kadhaa:

1. Kipi kilitangulia kati ya ujenzi wa Reli na ununuzi wa Treni na behewa zake ?

2. Kipi kinamwongoza mwenzie (amua mwelekeo) Je, ni treni ? au reli ?

3. Kipi kinaamua ukubwa na uzito wa mzigo unaobebwa je ni treni ama reli ? kama ingekuwa ni treni kuna ulazima gani wa Serikali yetu leo kujenga reli mpya kwa kiwango cha "Standard gauge " ?

Kwa maswali hayo nilijiridhisha kwamba miundombinu ya uwekezaji ni jambo la msingi kabla ya uwekezaji wowote ule, iko mifano mingi kwa wale wanaofuatilia watakua wanafahamu sababu kubwa iliyosababisha mradi wa boti ya Dar- Bagamoyo kushindwa kufanyakazi, kwa nini wakulima wanaandaa mashamba kwanza kabla ya kupanda, kwanini wanaangalia msimu wa kupanda jibu rahisi ni kuhakikisha miundombinu yote ya msingi iko sawa.

Swali ni je, katika mradi/miradi unayoianzisha sasa umeiwekea miundombinu mahususi inayoiwezesha kufika huko unakotaka ifike na kwa kiwango ulicho kusudia ? Inaweza ikafika lakini je, ni kwa kiwango standard ?

Ushauri:

1. Anza kufuatilia report za kiuchumi za World bank & IMF

2. Soma Majarida ya uwekezaji ya kimataifa

3. Soma Historia za watu waliofanikiwa sana kiuwekezaji

4. Jifunze kutengeneza mikakati/Strategies ( Angalia Clip za video za kijeshi mfano Vita ya Marekani na Japan, Israel na Misri na washilika wake, Jifunze jinsi mikakati inavyo andaliwa.

Tukutane wakati ujao !!!! - (Sehemu ya tatu)

By Allen Lupembe

Kwa makala nyingine za uwekezaji tembelea tovuti ifuatayo: Uwekezaji Tanzania
 
Back
Top Bottom