Ujenzi wa lami Tarime umeyeyuka?

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
375
1,000
Miezi ya hivi karibuni mkandarasi alikuwepo site akifanya marekebisho ya barabara Tarime Nyamwaga kiwango cha lami ,pia Kwa upande wa Tarime vijiji mkandarasi huyo alikuwa ameanza kupanua barabara na kulima kwa ajili ya lami

Kwa masikitiko makubwa mradi umeyeyuka na mkandarasi ameondoa mashine site

Waitara mbunge wa Tarime vijijini tena ni naibu waziri wa miundombinu yupo tu hakuna kinachoendelea .

Mjini Kembaki yupo hakuna kinachoendelea hakuna kinachoendelea, ukumbuke wabunge wote ni wa ccm na waziri yumo

Soko la zamani wakabomoa, kipindi cha Esther Matiko wakasema hawawezi kulijenga kwa sababu ni CHADEMA sasa hivi ni CCM hatuoni mchakato wowote,imekuwa maegesho ya magari

Wananchi wa Tarime tunataka kujua mradi wa barabara Tarime mjini Nyamwaga mpaka Serengeti nini kimetokea umeyeyuka na mkandarasi kuondoka?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom