Ujenzi wa jamii mpya

RICH MAVOKO

Member
Dec 10, 2013
35
0
Tanzania ni nchi yetu sote bila kujali tofauti zetu,naomba tuweke kando tofauti zetu za kivyama na tujadili ujenzi wa taifa letu kwa miaka 50 ijayo.nini kifanyike ili tanzania isonge mbele.
Tanzania kwanza,vyama baadae
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,035
2,000
Yafanyike haya yafuatayo:

turudi kwenye sera thabiti ya kilimo na kununua pembejeo na kutafuta masoko kwa ajili ya wakulima kuuza bidhaa zao.

Tutumie rasimali zetu kama mbuga za wanyama kwa kuinua uchumi wetu na kila asilimia 5 ya mapato kwa mwaka ipelekwe ktk sekta ya afya na elimu na maji.

SEKTA YA MADINI. ITUMIKE HAZINA YA BARA BARA ZOTE NCHINI. NA TUHAKIKISHE KILA WILAYA NA MAJIMBO YAKE KUNA BARA BARA ZA LAMI .

VIWANDA MAMA NA VINGINE VITUMIKE KAMA CHACHU YA KUKUZA UCHUMI NA KUAJIRI VIJANA WA KITZ.

PROTECTIONISM IN EMPLOYMENT. MAKAMPUNI YOTE YAAKIKISHE YANAAJIRI WATZ KWA ASILIMIA 95 KM HAWATAKI WARUDI MAKWAO.

KUSIWEPO NA MSAMAHA WA KODI KWA MAKAMPUNI YA WAGENI KAMA ILIVYO KWA SASA.

TUFUFUE USAFIRI WA TRENI NA PIA TUFUTE ATCL NA KUHUNDA TANZANIA AIRWAYS CORPORATIONS NA TUONGEZE NDEGE KUBWA 5 BOEING NA KUNUNUA ZILE NDOGO 6 KWA KUANZIA ILI TUWE NA UHAKIKA WA USHINDANI TUONGEZE KODI KWA PRIVATES FLIGHTS.

ELIMU. SERIKALI IHAKIKISHE ELIMU YA SEKONDARI YA CHINI INATOLEWA BURE NA ILE YA A LEVEL INAKUA SH ELFU 30 KWA MWAKA WA MASOMO, ELIMU YA JUU SERIKALI IONGEZE MKOPO KWA WANAFUNZI ILI WOTE WAPATE KWA DIV 1 AND 2.

MICHEZO SERIKALI IJENGE VIWANJA VYA MICHEZO KILA MKOA AU WATAIFISHE VILE VYA CCM NA KUVIFANYIA UKARABATI ILI TUWE NA VIWANJA VYENYE UBORA WA KIMATAIFA.

NI MAWAZO TU WADAU.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,042
2,000
Tanzania ni nchi yetu sote bila kujali tofauti zetu,naomba tuweke kando tofauti zetu za kivyama na tujadili ujenzi wa taifa letu kwa miaka 50 ijayo.nini kifanyike ili tanzania isonge mbele.
Tanzania kwanza,vyama baadae


Nadhani huu ushauri wako ungekuwa mzuri sana kwa "aliyeshikilia keki". Yeye kaing'ang'ania, kavimbiwa na hataki kugawana na watanzania wenzie badala yake kwa kutokujua anaona panya ndio wa muhimu kwake. Na bahati mbaya haonekani kuwa na uwezo na malengo ya kuoka nyingine kwa faida ya wote.

Aliyeshikilia keki siku takapoamua "kuachia" kwa faida ya wote nadhani maneno "Tanzania ni yetu sote" yatakuwa yametimia na kwa hakika tutapiga hatua kimaendeleo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom