Ujenzi wa daraja la Ubungo: Serikali itoe ufafanuzi wa hela iliyotumika katika ujenzi huo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Katika pitapita yangu mitandaoni,nimekutana na habari iliyoibuliwa na Bwana mmoja huko twitter kuhusu gharama ambazo serikali imetumia katika kugharamia ujenzi wa huo mradi ambapo muhusika ametoa nyaraka inayoonekana ni nyaraka iliyoandaliwa kwa ajili ya kujadiliwa Bungeni ikionyesha fedha zilizotengwa na serikali kwa ajili ya kugharamia huo miradi.

Kama nyaraka hiyo ni ya kweli(sio feki), basi serikali itakuwa ilitenga jumla ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Ubungo interchange(nyaraka inaaonyesha zimetengwa bilioni 10).

Lakini mradi huu tunasoma kuwa utajengwa kwa mkopo wa Benki ya dunia ambapo utagharimu bilioni 200.7 bila VAT(kwa mujibu wa gazeti la Habari leo mtandaoni la tarehe 04/04/2019).Nitaweka link hapo chini.

Mkanganyiko huu ndio umenifanya kutafuta habari zaidi kuhusu gharama ambazo serikali imechangia na ndio nikakutana na hilo gazeti la HabariLeo ambapo limeandika kuwa serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kulipa fidia wananchi na kwamba mradi huo unagharamiwa kwa mkopo kutoka benki ya Dunia.

Cha kujiuliza hapa ni hiki:kama serikali ilitoa bilioni 1.2 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi waliotakiwa kupisha huo mradi,hiyo bilioni 10 inayoonekana katika hiyo document ya Bunge inayoonyesha zilitengwa bilioni 10 kwa ajili ya mradi huo zilitumika kufanya kazi gani?

Kama hiyo document ni feki,kwanini serikali au Bunge wasikanushe?

Zitto wewe kama mbunge na member wa JF,tusaidie kuhusu hiyo nyaraka na ukiweza tupe ufafanuzi wa hiyo bilioni 10 kama ilipitishwa na Bunge kama ilivyo au kama kulikuwa na makosa ya wakati waanaandaa hiyo document na baadae wakarekebisha.
 
UFIPA bana kwa habari za kuokoteza?? kwa vichwa vibuyu kama hivyo mnataka na kwenda Ikulu! Eti Mange na Kigogo ndo sources za taarifa zenu
Unasema habari za kuokoteza wakati jamaa ana nyaraka nyingi tu na kila siku anazivujisha?
 
Leta source yako kutoka kwa manda do bayyo
UFIPA bana kwa habari za kuokoteza?? kwa vichwa vibuyu kama hivyo mnataka na kwenda Ikulu! Eti Mange na Kigogo ndo sources za taarifa zenu
 
Tatizo lenu nyinyi mmekazania kusikiliza tiibiiciii na kusoma uhuru na mzareeendo
UFIPA bana kwa habari za kuokoteza?? kwa vichwa vibuyu kama hivyo mnataka na kwenda Ikulu! Eti Mange na Kigogo ndo sources za taarifa zenu
 
Back
Top Bottom