Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiwa anaongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amethibitisha kwamba bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda litagharimu jumla ya dola bilioni nne za kimarekani. katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa sababu kubwa mbili zimewezesha kufikia makubaliano kati ya serikali za Tanzania na uganda, sababu hizo ni pamoja na :
1. bandari ya Tanga kuwa na kina kirefu hivyo kuwezesha meli za ukubwa wowote kuweka nanga bandarini hapo na kupakia mafuta kwa muda mrefu bila mashaka yoyote,
2. Hali ya amani na usalama ni sababu kubwa ya kufanikisha ujenzi wa mradi huo tofauti na maeneo mengine ya Afrika Mashariki
Katibu Mkuu amesisistiza kwamba wafanya biashara wa kitanzania wachangamkie fursa za uwekezaji katika miradi itakayojikeza sambasamba na ujenzi wa bomba hilo, mradi unaolezwa kutoa ajira nyingi kwa watanzania.