Ujenzi wa barabara stendi ya Korogwe

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
653
Kuna ujenzi wa barabara/stendi Ko gowe unaendelea hivi sasa .Hivi sasa ni miezi kibao kama sita hivi imepita kazi inayofanyika hapo haijulikani ni kazi gani.Kuna magari na makatapila yapo hapo kila siku yanazunguka tu na kusababisha msongomano wa magari na kukaribisha ajali. Haijulikani huu ni mradi gani wa ajabu ambao wafanyakazi wanazunguka tu na kazi ikiwa iko vile vile kila siku.

Kama ni serkali ndio iliopanga mradi huo kanyaboya kwa maana haufanyiwi matengenezo yeyote basi ni bora wangejipanga kwanza kuliko kwenda pale kila siku kuota jua na kupoteza muda wao na huku wakisababisha msongamano wa magari usiokuwa wa lazima.

Tunawaomba wahusika waondoe magari na vifaa vingine hadi hapo watakapokuwa tayari kujenga hiyo stendi au barabara.
 
Hizo ni tekiniki za mikataba kwa mkandarasi ili asinyang'anywe kazi maana sheria huwa kama amesaini mkataba na asionekane site kwa muda wa Siku 28 anafukuzwa ili kucheza na hiki kipengele unapeleka mitambo ili kuzugia.
 
Kongowe ziko mbili ..Ipo ya Kigamboni kama unaelekea Mbagala na ipo ya Kibaha...Sasa sijui ni ipi unaizungumzia
 
Pia nimeona hapo kataja Korogwe sasa. Sijui ni ile Korogwe ya Tanga ama ile sijui ya Sinza
 
Back
Top Bottom