diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
UJENZI wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam unaohusu barabara ya kadhaa ikiwemo ya Kilwa, utaanza rasmi Machi mwaka huu baada ya mkandarasi kupatikana na kusaini mikataba.
Mradi huo mkubwa utarahisisha usari kwa wakazi wa maeneo hayo na jirani na hivyo kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa na miundombinu ya uhakika ya usari kwa wakazi wake. Akizungumza kuhusu kuanza kutekelezwa kwa mradi huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wengi, Osa Mtendaji Mkuu wa DART, Ronald Lwakatare alisema baada ya wakandarasi kupatikana muda wowote kuanzia sasa watabakidhiwa eneo la mradi ili kuanza utekelezaji huo Machi mwaka huu.
“Ni kweli mradi wa BRT awamu ya pili unaanza kutekelezwa hivi karibuni na hiyo ni baada ya wakandarasi kupatikana na kusaini mikataba, ipi mikataba miwili kwa sababu wakandarasi pia ni wawili, mmoja ni wa majengo na mwingine ni wa barabara,” alisema Lwakatare.
Alifafanua kuwa mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara hiyo ya mabasi ya BRT ni Kampuni ya China iitwayo Sino Hydro Cooperation na mkandarasi mshauri ni Kampuni ya BOTEK inayoshirikiana na kampuni ya kizalendo ya APEX ambao walisaini mkataba Desemba 10, mwaka jana.
Katika ujenzi huo wa barabara utahusisha pia madaraja ya juu mawili (yovers), vituo vya kupakia na kushusa abiria 29, daraja moja la watembea kwa miguu na ujenzi wa kituo kimoja kikubwa cha abiria. Lwakatare alisema jumla ya gharama katika mkataba huo wa ujenzi wa miundombinu ya barabara ni Sh bilioni 189.43 na ujenzi wake utachukua muda wa miaka mitatu .
Barabara zitakazohusika kwenye mradi huo ni pamoja na Kilwa, Kawawa, Sokoine, Gerezani, Bandari na Chang’ombe ambazo zina urefu wa kilometa 20.3 Kuhusu mkataba wa ujenzi wa majengo ya mradi huo ambayo ni pamoja na karakana moja,vituo vikuu viwili na barabara za kuunganishia vituo tatu (feeder roads).
Alisema mkandarasi wa ujenzi huo wa majengo ni Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) na mwandisi mshauri ni kampuni Inter Consult na kwamba gharama ya ujenzi ni Sh bilioni 44.82 na kwamba miundombinu hiyo itajengwa kwa miaka miwili. Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Lwakatare alisema unafanywa chini ya uangalizi na usimamizi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ambao wamehusika kutangaza na kuchagua wakandarasi.
“Sisi ni watendaji lakini tunashirikiana na Tanroads kwenye hili na wao ndio wasimamizi wakuu wa utekelezaji wa mradi huu ambao unasubiriwa kwa hamu na wananchi wengi,” alisema Lwakatare. Alisema kwa kuanza wametangaza kuondoa daladala katika kituo cha gerezani Kariakoo kuanzia Februari 9, mwaka huu ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya BRT.
Aidha, wamiliki wa daladala hizo wamepewa mwongozo mpya na Mamlaka ya Udhibiti wa Usari wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) wa utaratibu wa kutumia vituo vingine vilivyotangazwa na kuomba watoe ushirikiano ili kuepusha usumbufu.
Akizungumzia ulipaji dia kwa wamiliki wa maeneo yaliyochukuliwa kupisha mradi huo awamu ya pili, Lwakatare alisema wale wote waliopaswa kulipwa dia wameshalipwa na wamebaki watu wachache ambao walikuwa na mambo ya kisheria ambayo hata hivyo yameshamalizika na watalipwa. “Hela ya kulipa dia yote ilitolewa na wahusika halali takribani 104 wameshalipwa stahiki zao na wachache waliokuwa na kesi zimeisha na hivyo mradi utaanza kutekelezwa mapema,” alieleza.
Aidha, Lwakatare ametoa rai kwa wale wote wanaotakiwa kuondoka kupisha mradi huo wafanye hivyo na watoe ushirikiano ili ujenzi wake uende vizuri na pia wazingatie njia salama wanazoelekezwa kupita wakati wa utekelezwaji wa mradi ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.
Awamu ya kwanza ya mradi huo ilizinduliwa Januari mwaka 2017 na Rais John Magufuli ambapo mradi huo ulitekelezwa kwenye Barabara ya Mogorogo, kuanzia eneo la Kivukoni hadi Kimara yenye urefu wa kilometa 20.9 Sambamba na barabara hiyo pia mradi huo ulitekelezwa kwenye Barabara ya Morocco inayounganishwa barabara ya Morogoro kwenye makutano ya taa za Magomeni. Hata hivyo awamu ya tatu ya mradi kama huo utahusisha barabara ya kwenda Gongolamboto yenye urefu wa kilometa 23.6 na ujenzi wake kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Osi wa Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, utatekelezwa mwaka wa fedha 2018/19.