Ujenzi maghorofa ya Magomeni kuanza. TBA waahidi kuukamilisha kwa wakati

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
ZIKIWA zimepita siku 20 tangu Rais John Magufuli atoe ahadi ya ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam, Wakala wa Majengo nchini (TBA) umesema unatarajia kuanza ujenzi huo rasmi Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Elius Mwakalinga alisema kuwa tayari serikali imewapa Sh bilioni tano, kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

“Tunashukuru serikali kwa kutoa fedha tunachoweza kuahidi sisi ni kupiga kazi ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati,” alisema Mwakalinga.

Alisema kuwa baada ya Rais, kuwataka TBA kuanza ujenzi huo mara moja, na kwamba tangu Septemba 20 mwaka huu, ulianza kwa hatua za mwanzo ikiwa ni pamoja kuandaa michoro na kurejesha mipaka ya eneo hilo ambayo itasaidia katika kupanga nyumba zinazotarajiwa kujengwa.

Aidha alisema kuanza kwa ujenzi huu kunatarajia kutengeneza ajira zaidi ya 600 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa siku moja.

Aliongeza kuwa ujenzi huo, utakuwa na nyumba tano zenye ghorofa nane kila moja ambazo zitawaweka wakazi 644 waliobomolewa nyumba zao mwaka 2011, majengo mawili ya ofisi pamoja na majengo ya biashara.

Aidha, alisema nyumba hizo hazitawanufaisha wale waliobomolewa nyumba zao pekee bali hata wananchi wengine wanaweza kunufaika na nyumba hizo.

Hata hivyo, Mwakalinga alisema eneo linalotarajiwa kujengwa nyumba hizo ni ekari 13 pekee kati ya ekari zaidi ya 30 zilizopo. Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Mradi huo, Humprey Killo, alisema kwa sasa wanaendelea kutoa udongo wenye rutuba ambao hauhitajiki katika ujenzi baada ya kukamilika wataanza kuchimba misingi kwa ajili ya ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baada ya miezi 12.

Hivi karibuni wakati Rais akiweka jiwe la msingi katika eneo hilo, alisema ahadi ya ujenzi wa nyumba za kisasa katika eneo hilo, itaanza kutekelezwa ndani ya miezi miwili na ujenzi wa nyumba hizo utakamilika ndani ya mwaka mmoja, ambapo wakazi hao 644 watapatiwa nyumba za kuishi watakazoishi kwa muda wa miaka mitano bure.

Alisema wakazi hao waliotabika kufuatilia haki yao mahakamani kwa muda wa miaka mitano tangu mwaka 2012 walipotolewa kwenye nyumba hizo, watapatiwa nyumba hizo za kisasa kulingana na taarifa zao na orodha ya majina yao ambayo Rais huyo anayo.

Chanzo: Habarileo
 
Sheria ya manunuzi imekufa??? siioni wapi procurement imefanyika, tuendako ni kugumu.
 
procurement of goods and services) ingia website ya PPRA uisome sheria ndo taelewa namaanisha nini
Kwani ni nani mwenye kujenga hayo majengo? Kwani NHF inapojenga wajengo wanatangaza procurement au wanatangaza tenda ya ujenzi?
 
Kwani ni nani mwenye kujenga hayo majengo? Kwani NHF inapojenga wajengo wanatangaza procurement au wanatangaza tenda ya ujenzi?
sheria ya manunuzi inaanzia kwenye upatikanaji wa washauri wataalamu wa mradi (consultants) then wakandarasi (contractors)then subcontractors then suppliers. slikakali au taasisi yake haiwezi kuwa Cliet, alafu consultant alafu contractor alafu subcontractor alafu supliers. sheria ya manunuzi inakataza
 
  • Thanks
Reactions: MC7

Nadhani ilishafanyiwa marekebisho, hata hivyo serikali ina wataalamu wake wenye uwezo wa kusimamia na kujenga kwa kuwalipa per diem/allowances kwa nini waingie gharama ya mabilioni ya ziada ilhali kuna watu inawalipa mishahara
 
sheria ya manunuzi inaanzia kwenye upatikanaji wa washauri wataalamu wa mradi (consultants) then wakandarasi (contractors)then subcontractors then suppliers. slikakali au taasisi yake haiwezi kuwa Cliet, alafu consultant alafu contractor alafu subcontractor alafu supliers. sheria ya manunuzi inakataza
Angalia post #16 and #18 utajua kwa nini nimekuuliza hayo masuala
 
Back
Top Bottom