ujenzi kwenye ardhi ya udongo mfinyanzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ujenzi kwenye ardhi ya udongo mfinyanzi

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Chum Chang, Sep 21, 2012.

 1. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Msaada au maoni ya kitaalam kuh ujenzi wa nyumba kwenye ardhi ya udongo mfinyanzi.Nimeamua kutafakari nanyi

  wenzangu wa JAMII INTELLIGENCE kwa maana ukitaka kwenda mbio lazima uagane na nyonga.Dunia hii si ya kukurupuka

  tuu kama kuna wasaa kwa anaehitaji ana budi kuwauliza wenzie nami sina budi kuuliza na kupata ushauri wenu​
   
 2. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Udongo wa mfinyanzi una tabia ya kuhifadhi maji yanayoufanya ukose ule uimara wake,pia maji yanapokauka unatanuka na wakati mwingine kusababisha nyufa nyingi nyingi.Katika uzoefu wangu wa kujenga kwenye udongo wenye asili ya mfinyanzi,nimepata matatizo yakiwemo udongo kushindwa kubeba uzito wa jengo au ufa wake kuendelea mpaka kwenye jengo.
  Nini cha kufanya?
  Kama una uwezo unatakiwa kuuondoa wote katika eneo unalojenga na kuleta udongo wa aina nyingine.
  Kama uwezo ni mdogo unatakiwa kutumia mchanga mwingi na kuuchanganya na kiasi kidogo cha mfinyanzi.Backfilling yote hakikisha inakua ni mchaga.Hakikisha unaseparate mfinyanzi na jengo kwa kutumia mchanga.
  Njia ya pili ni kuhakikisha unareinforce vizuri foundation yako kwa kutumia nondo kuepuka expansion ya clay isiambukizwe kwenye jengo lako.
  Nafikiri nimekusaidia.
   
 3. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Inategemea unataka kujenga nyumba ya aina gani bwana Chum Chang , Ghorofa ngapi ama nyumba ya kawaida (isiyokuwa na ghorofa), angalia kipi kitakuwa na gharama ndogo,

  1) kuchimba msingi wa kama mita 1.5 hadi 2, na kujenga msingi ambao pembeni yake utatakiwa kuweka material nyingine ambayo si expansive, preferably moram, msingi uwe mpana kama mita 2. kwa njia hii usitumie mchanga maana mchanga utaruhusu maji yaingie ndani na hivyo kubadilisha kiasi cha unyevu kilichomo kwa udongo. hakikisha ndani udongo wote umeuchimba na kuutoa angalau sentimeta 30 au ft 1, kisha weka udongo mwingine preferably moram hasa hasa yenye changarawe

  2) Njia ya pili unaweza kufanya kama alivyoshauri Andrew Kellei kwa kufanya replacement na udongo mzuri zaidi.

  3) Nakushauri utafute Civil engineer aangalie site yako visually atakushauri vizuri zaidi na bure (zaidi labda mtakaa sehemu kuchoma nyama na bia mbili tatu) ikiwa ujenzi ni nyumba ya kawaida (non-load bearing), ikiwa ni ghorofa itabidi umlipe
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa msada wenu...shauri nimeupata mda muafaka kwani naanza mchakato wiki ijayo..
  Nimemtafuta engineer na nategema atakayo sema na haya mlinishauri yatawezesha dhamila yangu...
   
 5. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Karibu Mkuu anytime, mimi ni Civil Engineer ukinihitaji ni PM tu nitakusaidia kadiri ya uwezo wangu.
   
 6. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Natanguliza shukran.Ahsante sana mwana jamii intelligence mwenzangu Andrew
   
 7. Capital

  Capital JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,036
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Kuna aina mbalimbali za clay. mbaya katika majenzi ni ile inaitwa 2:1 au expanding clays, hii kina chake hufikia 2m. ukijenga hapo unakuwa umeliwa. namna ya kutambua aina hii ni kwa msaada wa engineer au soil scientist. goodluck.
   
 8. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,314
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280

  Ushauri wako ni mzuri sana,lakini penye red hapo juu vipi kama huyu mtaalamu hatumii hivyo vitu?
   
 9. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nikuhakikishie ndugu yangu robert josephat kuwa hawa jamaa zangu nikiwemo mimi mwenyewe ni wadau wazuri sana wa hivyo vitu walau kimoja wapo lazima anatumia.

  Anyway nilitaka kuonyesha kuwa Civil engineer si complicators wa malipo kwa mambo madogo madogo yanayowahusu wanajamii moja kwa moja, wanaweza kusaidia kwa malipo ya kindness.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Namuheshimu sana huyu jamaa anayeuliza ili apate kujua. Kwa sababu ya kudharau ujuzi wa watu, kuna majengo yamejengwa na kukamilika bila kuwa nanviwango vinavyostahili sehemu nyingi tu kwenye nchi yetu. Inabidi tuwe tunahamasisha watu waanze kutumia wataalamu kuepuka matatizo ya kujenga chini ya viwango.
   
 11. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Capital kinachosumbua kwenye expansive soils ni moisture variation, endapo mtu ataweza ku-control mosture variation, clay or expansive soil si tatizo, ugumu upo kwenye ku-control variation ya moisture, udongo mbaya kabisa ni silt type, kwa kuwa huu ukiwa hauna maji au ukiwa na maji strength yake ya kubeba mzigo ni ndogo. I stand to be collected
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,703
  Likes Received: 2,383
  Trophy Points: 280
  Yaani hii kitu acha, bro wangu ana kajumba chake maeneo ya mbezi makabe yaani hata hajafikisha mwaka tangu ahamie ,nyumba kama kibwaya cha mzaramo jinsi ilivyo rarukararuka!Ila nashukuru huu uzi maana na mimi nina kaeneo maeneo hayo hayo sijakaendeleza tutatafutana nikishamaliza kula urojo zenji.
   
 13. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #13
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Karibu Mkuu.
   
 14. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2017
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  mkuu naomba ushauri wsko nina site ambsyo uns mchanga mwingi je inafaa kwa ujenzi wa nyumba?
   
 15. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #15
  Jan 23, 2017
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Inafaa kabisa Mkuu ndio maana kuna majengo maeneo ya ufukweni ambapo ni mchanga mwingi.

  Kikubwa lazima uhakikishe unakua na msingi imara ambao kama ukipata mawe ni mazuri, ila ukikosa uhakikishe unapata kokoto nzuri za zege.

  Mtafute mtaalamu akaangalie eneo iliajue kama huo mchanga unaweza kuwa easily washed away iliakushauri.
  Otherwise kwenye mchanga ni kuzuri kujenga kuliko kwenye mfinyanzi
   
 16. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2017
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  ahsante mkuu
   
 17. kwenzi

  kwenzi JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2017
  Joined: Aug 25, 2016
  Messages: 638
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 180
  VP tofali za kuchoma na kujengea tope badala ya cement ni imara kweli.
  Naona huku nilipo kijijin majumba makubwa tu yamejengwa kwa tope

  Cement inatumika kwenye lipu na plasta na sakafu ya chin tu
   
 18. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #18
  Jan 23, 2017
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Inategemea ukubwa wa nyumba kwa maana ya kwenda juu kwa urefu na aina ya udongo.
  Udongo tifutifu wenye kiasi kidogo cha mfinyazi unashikamana ukipondwa.Mfinyanzi unakua kama ndio sementi yake.
  Kuepuka kupasua ufa, vijijini watu wanachanganya na nyasi.Nyasi zikishikamana na udongo nyumba inakua imara kama imejengwa kwa nondo maana hizo nyasi zinakua zimeshikamana na kuzuia mpanuko ambao husababisha nyufa.

  Cement tunaitumia kwasababu mchanga hauna tabia ya kushikamana. Cementi ni binding material tu.So ukipata udongo wenye binding properties,sementi hutahitaji.
   
 19. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #19
  Jan 23, 2017
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Karibu tena
   
Loading...