comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Salaam JF
JENGO la kisasa la kituo kitakachokuwa na teknolojia ya kumwezesha mtu kuwakaribia wanyama wakali kama simba, mamba, faru na nyati kupitia uhalisia nadharia maarufu kama ‘3D virtual reality’ umeanza na unatarajiwa kukamilika mwaka 2018.
Serikali kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), kwa ushirikiano na nchi ya Korea Kusini kupitia Taasisi yake ya uhusiano wa kimataifa (Koica) umeanza ujenzi wa kituo hicho kitakachojulikana kama ‘Serengeti Media Center,’ eneo la Seronera, ndani ya hifadhi ya Serengeti, ambamo ‘safari,’ za nadharia kutembelea mbuga maarufu nchini zitakuwa zinafanyika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema kupitia miwani maalumu ya kuwezesha watu kupata picha za uhalisia wa pande tatu (3D) na filamu za wanyamapori zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, watalii na hata wananchi wa kawaida watakaotembelea Serengeti wataweza kutumia teknolojia hiyo kuwakaribia wanyama kwa ukaribu zaidi.
Profesa Maghembe alisema runinga kubwa ya zaidi ya inchi nane kwa tano pamoja na miwani maalumu itawawezesha watu kuwatembelea mamba ndani ya mto Mara, simba na wanyama wengine wakali kupitia video maalum.