OLESAIDIMU
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 19,139
- 9,525
vumbi litapitaje wakati mkanda umebana kisawasawa?
Mikanda huachia mara nyingine . . .Ukianza kudhibiti tangu juu kwenye board ni vema zaid. . .
vumbi litapitaje wakati mkanda umebana kisawasawa?
Namaanisha si mwisho wa siku zitazibwa na gypsum!
Mkuu kwani hilo box likiwepo kunashida gani?
nisaidieni vifaa vya blending na kuweka gipsam HP1 Dengue KakaJambazi Dark City
kuna vifaa vinaitwa kona, mkanda na fiba sivielewi kabisa msaaada
Pamoja na picha nzuri alizobandika KakaJambazi, hivi vifaa vipo vingi kwenye maduka ya Wachina pale Kariakoo. Wasiliana na Fundi Bakari kwa ushauri zaidi na akusaidie kuyafikia hayo maduka.
Namba za Fundi Bakari ni 0754498893 au 0718824625
Mkuu ameonyesha vizuri kabisa kwa picha. Sista kwa kifupi fiber inatumika kwenye maungio kati ya gypsum board moja na nyingine. Corner ni ile gypsum board yenye urembo inawekwa kwenye pembe, mkanda unakaa unaunganisha ukuta na gypsum board, na kunakuwa na gypsum powder inayoloweshwa na maji kutengeneza uji kuziba sehemu za fibre na kuficha misumari iliyotumika kugongelea gypsum board
Mikanda huachia mara nyingine . . .Ukianza kudhibiti tangu juu kwenye board ni vema zaid. . .
OLESAIDIMU asanteeee babi ake
karibu. . . . .ila wewe. . . .!!!!!
Nimependa haya maelezo pia nimeangalia picha husika ila naomba kujua hasara za hiyo box na je ukiwepandisha box kwa juu varanda si itakuwa juu sana!!!Ok, iko hivi,...kama nyumba yako ina veranda kwa nje (kibaraza) ambacho kitakuwa kimeshikiliwa na nguzo, basi lazima nguzo zijengwe kwa kusuka nondo na hizo nguzo zitaunganishwa na nyumba kuu kupitia kwenye linta box. Endapo utafanya hivo, ina maana baada ya linta basi itabidi kujengwa tofali ili kufikia usawa wa kupaulia. Hii itafanya kuta za nyumba kuu na kibaraza kuwa kwenye usawa ule ule wa kupaulia. Baada ya kuezekaa (endapo kibaraza hakijamiminwa zege), basi kutakuwa na uwazi unaofanana na box kuanzia pale kwenye linta hadi kwenye ceiling board.
Kwa maelezo hayo kama bado hujanielewa basi itabidi tuwasiliane nikutumia mchoro