GE2025 Ujenzi Airport ya Kimataifa Pemba kugharimu TakribanIi zaidi Tsh. 490 Bilioni

GE2025 Ujenzi Airport ya Kimataifa Pemba kugharimu TakribanIi zaidi Tsh. 490 Bilioni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekabidhi rasmi eneo kwaajili ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kisiwani Pemba ambao utagharimu Euro Milioni 170 ili kufungua fursa za kiuchumi kisiwani Humo

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amemwakilishi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwaajili ya tukio hilo kubwa la kihistoria

Hemed amesema kuanza kwa mradi huo kunaenda kufungua fursa za uchumi kupitia utalii na biashara ambao utafaidisha wananchi wa kisiwa hicho

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt Habiba Hassan Omar amesema mradi huo wa Ujenzi wa Uwanja wa ndege utagharimu Euro Milioni 170 ambao utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 300,000 kwa mwaka na kuruhusu ndege kubwa kutua moja kwa moja

Aidha amesema Kampuni ya Propav itakua na jukumi pia la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 43.5 kutoka Mkoani hadi Chake Chake na kugharimu Euro Milioni 93

Amesema miradi hiyo ukiwemo wa uwanja wa ndege utatoa fursa za ajira 1000 kwa wananchi wa Pemba


 
Mkuu embu kuwa serious kiasi, unaandika unakimbilia wapi?

Toka lini Euro Million 170 zikawa sawa na Million 400 TZS??
 
Shule shule shule ! Hisabati hisabati hisabati! £170m sawa na 400m Tsh exchange ya wapi hii?
 
Barabara ya km 43.5 inajengwa kwa euro 93 ?, itakuwa ni double Way + light.

Hiyo tenda wapewa wazawa, ili kuongeza mnyororo wa PESA.

Au wazawa KAZI Yao ni kusoma maulidi.

Huu mradi ni jambo jema, lakini utatumika kifisadi
 
Back
Top Bottom