Ujasusi - Umoja namba 97

Mbona namba naambiwa siyo sahihi
 
Bado masaa machache kufika mkuu
Mkuu Kwanza nikupongeze kwa uandishi, maana kuandika tu Ni kipaji tosha kabisa

Pili, nikupongeze Sana kwa mchoro wa hadithi, umejitahidi kuweka madhari halisi hapa nakupa 8/10

Tatu hadithi yenyewe umetumia njia ya masimlizi, nafsi ya Kwanza umoja inadhani ulihitaji Sana kueleza ww binafsi kuliko wahusika, (Sina uhakika Kama umeelewa) na kwa nyakati fuln ukajikuta unamasimlizi marefuuu kiasi ambacho unaporudi kwenye hadithi yenyewe unachanganya, mfano kunawakati ulichanganya Kati ya suzani na zakayo Kama sikosei, na kunakipindi pia unachanganya na kumuita merina Ni mtoto wa mke wa raisi, na hii Ni kwa kuwa unasimlia zaidi.. kwenye simliz mpka Sasa nakupa 7/10

Kwenye washiriki asee umejitahidi story inawashiriki wengi Sana kunawakati sikulaum kabisa ila nakupongeza maana umejitahidi kutengeneza taswira halisi..

Japo jingine Ni wahusika kutokuvaa uhusika wao haswaaa au kumtegemea mtu 1 ndo wavae uhusika, ngoja nikupe mfn, damiani anafuatiliwa na karib watu wote kwenye hadithi hii ila akilala tu na wao wanaacha kumfuatilia as if kazi inakuwa imeisha, heb angalia gap la kutoka kisemvule mpka kesho yake mpka Damian anaenda sijui mbez kwenye ile nyumba yaan wapelezi woooote hakuna anaeshughulika nae , halafu kimbembe kikianza wooote wanaamka, na wakati nlitaraji kwa namna anavyowindwa asee Sina uhakika ila hyo nmeona weakness kwa wahusika nakupa 5/10

Jambo jingine Ni teknolojia na wanausalama wenyewe asee broo tupo karne 21 hii hadidhi iweke kuwa ya hii karne, madhari yake iko very low, yaana kwa jinsi teknolojia ilivyo humatafuti mtu kwa kumfuatilia unamtafuta mtu kwa gps, yaan hyo nguvu ilikuwepo kipindi Cha Willy gamba huko, somo hum ndani kunahadithi za karn 21 uone wanavyotia teknolojia, kwa kwel hapa pamoja na yote nakupa 4/10..

Ila kilichokizuri hadithi inacode nyingi Sana ambazo ukiwa makini utajua kuwa umeficha mambo mengi Sana kwenye maelezo yako ambayo kiuhalisia yanaonekana ila kiutendaji kunajumbe mhim mno kwangu nakupa kongole9/10..

Mkuu mengine ntasema nikimaliza hadithi, kwa ujumla mpka hapa hadithi yako nmeipa 6/10, bigup broo..
 
Shukrani sana kaka .. kwa ushauri wako .. Very nice nitalifanyia kazi
 
SEHEMU YA 76

SINGANOJR
DEAL MARRIAGE(NDOA YA DILI )
Ilikuwa ni muda wa saa mbili za usiku hivi Damiani akiwa yupo ndani ya nyumba yake maeneo nya Makongo juu , siku hio alikuwa yupo na Janeth wamekaa wakiangalia runinga , na kwa jinsi walivyokuwa wakionekana utadhania walikuwa wapenzi ,, basi wakati muvi imekolea ndipo simu ya Damiani ilipata uhai na aliichukua na kuiweka sikioni huku akiwaza anaempigia wakati huo wa usiku ni nani , kwani haikuwa kawaida kupigiwa nyakati za usiku tena na namba ngeni .
“Sabi mboneche , Stephano lamberk , Janeth bendera , Wema sufiani mmekuwa target ya U-97 na mpaka sasa watu wanaotakiwa kukamilisha vifo vyenu wapo Nchini kuweni makini .“ .
“Wewe ni nani ?”
“ Tiii.. tii “ Simu ilikatwa pale pale na kumfanya Damiani azidi kushangaa ,lakini sauti alioiskia ni sauti aliokuwa akiikumbuka vyema , sauti hii ni sauti aliosikia alipopiga simu kwa namba alizokuwa amepewa na Bruno , na mtu huyo ndio huyo aliekuwa akimpa maelekezo .
“ Kuna nini ?” Aliuliza janeth .
“U-97”
“Wamefanya nini ?”
“ Unawajua ?”
“Ndio nishawahi kusikia taarifa zao kutoka kwa baba , ila bado sijawajua vizuri , lakini ninacho jua mpango wa MZALENDO ni kuitoa huu umoja hapa nchini”
“Baba yako alikuambia nini kuhusu huu umoja ?”
“ Hakuniamba maneno mengi , ila alisema niwe makini , ndio hapo nilipo anza kufatilia umoja huu na niligundua baadhi ya mambo kabla hata ya kuja hapa Tanzania .
“Mama yako ,, mimi , wewe na Sabi ndio targeti yao kwa sasa na wau walioandaliwa kwa ajili ya kutupoteza duniani washafika Tanzania , ndio ujumbe niliopewa sasa “
“Hata mama yangu ?”
“ Ndio , inabidi tumtahadharishe juu ya hili “
“ Nitampigia simu “
“ Hapana mpigie Sabi simu atapeleka ujumbe “ Aliongea Damiani na hapo hapo mawasiliano yalifanyika kwa Sabi .
******
“ Vipi Sam “
“ Safi , yaan leo nina furaha tunywe tulewe “.
“Furaha gani tena ?”
“ Vijana washaingia nchini “
“ Vijana gani ?”
“ Boko haramu “
“ Unamaanisha kwa ajili ya kukamilisha lile jambo ?”
“Ndio “
“ Hapo safi , inabidi swala hili lifanikiwe mapema “
“ litafanikiwa “
“ Unazungumziaje mtoto wa raisi kuolewa na mtoto wa tajiri Mahmood ?”.
“Ni fursa kwetu”
“Kivipi ?”
“Ndio nilivyoambiwa na wakuu kwamba ni fursa kwa Umoja wetu “
“ Unamaanisha ni fursa dhidi ya Umoja wetu “
“ Ndio nilivyoambiwa “ aliongea Sam na kumfanya Kimbona ashangae kwani yeye aliona jambo hilo lingempa raisi nguvu , lakini ilikuwa nje ya mategemeo yake .
Na hio ni baada ya kutoka ikulu na kwenda kupata bia , na mazungumzo hayo yalikuwa yakifanyika ndani ya Casino la las vegas Posta karibu na hospitali ya Aghakhani.
“ vipi marie , hajaonekana bado ?”
“Vijana wanakisia huenda yupo mateka ndani ya lile jumba kule kibaha “
“ Unamaanisha lile jumba Ambalo damiani alionekana akiingia “
“ Ndio na nina uhakika huo , kwani Marie alipotea kwenye harakati hizo , japo jambo hii linanifikirisha yule ni jasusi wa CIA kukamatwa kizembe ni kosa kubwa “
“ una mpango gani sasa ?”
“ Wa kumtoa pale , kuna kitu kinaendelea pale , na hili swala nataka nimshirikishe mheshmiwa “
“unamaanisha mheshimiwa raisi ?”
“ Ndio , Hisia zangu zinaniambia hivyo “
“ lakini si vijana waliona magari ya Ikulu ndani ya hilo eneo , je kama muhusika mkuu ni Raisi mwenyewe”
“Lakini pia kumbuka moja ya watu ambao wapo kwenye Death notice ni Madam wema na Damiani , mheshimiwa yeye anamtafuta Damiani kwa hali na mali Inawezekanaje akawa anahusika na magari yale yalionekana mahali pale “
“ hapo umeongea , huenda yote yale ni mipango ya Wema , na kwa maelezo hayo nina uhakika kuna jambo kubwa linaendelea hapo , lakini mimi naona jambo hili tusilipeleke moja kwa moja kwa Raisi , kwanini tusimshirikishe Suzzane kwani ndio mshirika wake mkuu , na kumbuka pia yeye ndio anahusika kumfatilia Damiani “
“ hapo kweli Inabidi nionane nae “.Aliongea kimbona
Kulivyokucha tu kimbona hakutaka kuchelewesha mambo alimtafuta suzzane , na suzzane alimwambia kimbona kwamba anakuja kwenye ofisi yake , haikuchukua muda mrefu suzzane alifika .
“Ndio Kimbona nadhani una jambo la muhimu la kuniambia “
“ Ndio Suzzane “.
“Kuna mtu nilimpa kazi kwa ajili ya kumfatilia Damiani , lakini mtu huyo amepotea mpaka sasa haonekani “
“ Ni nani huyo “.
Kimbona hakuongea mengi alimpa faili linalomuhusu marie na kisha Suzzane alianza kulisoma na aliishia kutoa macho , kwani hakujua kuwa Kimbona anaweza kukod jasusi wa CIA .
“kwa hio unataka nikusaidiaje ?”
“Nataka ukamtoe sehemu ambayo naamini anashikiliwa “.
“Ni sehemu gani ?”
“Kibaha kwa mathiasi , kuna jengo ambalo Damiani alionekana akiingia pamoja na Madam wema “ aliongea kimbona na kwa suzzane alionekana hakushituka kabisa .
“Najua unazungumzia kambi N “
“ unaifahamu ?”
“ Ndio naifahamu vyema , ni sehemu yenye ulinzi mkubwa sana , na ipo chini ya jeshi “
“kama ipo chini ya jeshi unadhani kwanini mke wa raisi akaingia ile sehemu , na vipi kuhusu damiani ?”
“hayo yote nayafanyia uchunguzi ,”
“ mheshimiwa anajua juu ya hili ?”
“ bado sijamueleza chochote , mpaka nitakapo kamilisha uchunguzi wangu” .
“hakikisha uchunguzi wako ukikamilika unanipa taarifa na pia nataka umtoe Marie ndani ya eneo hilo “
“hayo ni mambo ya kisualama wa Nchi , nadhani nitakalo kusaidia ni kumtoa huyu Marie , lakini jambo hili lazima mheshimiwa alijue “.
“hakuna shida suzzane , lakini kumbuka unayoyafanya yote sio kwa ajili ya mheshimiwa tu bali kwa ajili ya U-97 “.
Suzzane alijikuta akipandwa na hasira ila hakutaka kulionyesha hilo mbele ya Kimbona Zaidi ya kunyanyuka na kuondoka.
*****
Upande wa NLT siku hio damiani alifika kwenye kampuni yake kwa ajili ya kuendelea na majukumu kama kawaida , kwani walikuwa mbioni kutangaza bidhaa yao mpya ambayo ingeambatana na ufunguzi wa kampuni .
Wakati akiendelea na majukumu yaka ndipo alipo ingia secretary wake na kumuambia kuna mgeni anahitaji kuonana na yeye , na Damiani hakujifikiria sana aliruhusu mgeni huyo aingie , na hapo ndipo Damiani alipokutana na sura ambayo hakuwa akiijua vyema , sura hii haikuwa nyingine bali alikuwa ni mwana Matinde ,Mkurugenzi mstaafu wa TISS , Damiani alimkaribisha vyema na kisha walisalimiana na kujitambulisha .
“karibu sana mheshimiwa “
“ Asante , jambo lillilonileta hapa sio la kiofisi Zaidi bali ni swala binafsi “
“ hakuna shaka karibu sana na kusikiliza “
“Najua ndani ya kampuni unafahamika kwa jina la Stephano lamberk , lakini kihalisia wewe ni Damiani rabani “ aliongea mkuu huyu na kumfanya damiani ashangae kidogo kwani siku zote Damiani akiingia ndani ya kampuni yake kikazi , huwa anakuja kama Stephano , yaani akiwa amevalia FULL BODDY MASK .
“Huna haja ya kushangaa Damiani ,nimekuwa moja ya watu ambao nilikuwa nikikufatilia kwa muda mrefu sana tokea kifo cha mama yako “.
“kwanini ulikuwa ukinifatilia mheshimiwa “ Damiani alijibu baada ya kuvuta pumzi na kuzishusha .
“Nadhani unaweza ukajiuliza nimefahamu vipi siri yako ya kuvaa ngozi ya kizungu , lakini mtu ambae ananifanyia kazi ya kukufatiia ni Zakayo “ aliongea na hapo Damiani alijikuta akitaka kutoa tusi , ashajua jasusi mpenda pesa ashauza taarifa zake .
“Endelea mheshimiwa”.
“Nataka unidokeze juu ya nyaraka ulizoachiwa na Bruno , kwanini mheshimiwa raisi anazitafuta sana”
“kwanini nikwambie juu ya hilo mheshimiwa ?”
“Kwasababu mimi ni moja ya wanausaama walioaminiwa na mheshimiwa Bendera , na nafanya yote haya kwa ajili ya usalama wa Nchi hii , na nayajua mengi ambayo pengine huyajui “.
“ mheshimiwa najua wewe ni mwanausalama na ni jambo la kawaida sana kwako wewe kuwazia usalama wa taifa , lakini pia hata mimi kama raia mwema ni kawaida kuwazia jambo la usalama wa nchi yangu , lakini bado sina sababu ya kukwambia nini bruno kaniachia”Matinde alijikuta akikaa kimya kwa muda kwani aliona kabisa mtu anaeongea nae hamwamini mtu na hilo alilitegema .
“Kwa nafasi yako ni sahihi kutoamua kuniambia na nililifahamu hilo kabla ya kuja, lakini naamini kupitia hili utaniamini “Aliongea matinde na kisha alitoa bahasha flani ndogo kabisa za kuhifadhia barua na kisha alimkabidhii.
Ilikuwa ni barua ilitoka kwa raisi Bendera kwenda kwa Matinde , barua hio iilikuwa ikimpa maelekezo ya Matinde kumtafuta Damiani .
Damiani alijikuta akianza kukumbuka baadhi ya mambo , alikumbuka mambo mengi hususani yela alioambiwa kuwa mheshimiwa Bendera alikuwa akimjua vyema na kumfatilia kwa ukaribu , barua hio ilikuwa na sahihi kabisa ya mheshimiwa Bendera marehemu .
“Nadhani mpaka hapo unaweza kuniamini na unaweza ukajua ni sababu gani nilikuwa nikikufatilia kwa muda mrefu , ni maagizo niliopewa kama ulivyosoma katika hio barua “.
“Nimekuelewa muheshimiwa, lakini kwanini unataka kujua ni kipi bruno ameniachia , maana ni vitu ambavyo havihusani kabisa na mheshimiwa Bendera wala Henry”
“Mimi na wewe tuna adui mmoja Damiani “
“ Adui yupi “
“ U-97”
“Sina uadui na huo umoja mimi dhumuni langu kuu ni kulipiza kisasi kwa wale waliohusika na kifo cha mama yangu “
“ na watu hao ni nani kama sio U-97, na kama ni hao jua swala hilo hauwezi ukalifanya peke yako na ndio maana niko hapa , wote sisi ndio tuliongoza mapambano ya kuutoa umoja huu ndani ya nchi hii , lakini kwa sasa unarudi kwa kasi Zaidi hapa nchini jambo mbalo linaonyesha juhudi zetu tulizozifanya wakati wa uongozi wa bendera zilikuwa bure “
“kwa hio mheshimiwa unaamini kwa kukuonesha nyaraka hizo unaweza ukautokomeza umoja huu?”
“ Dhumuni langu ni kutaka kujua ni kwanini mheshimiwa raisi anataka nyaraka hizo , fikiria mambo yote yaliotokea nyuma hadi kifo cha Danny , unafikiri ni kwanini ?”
“hilo hata mimi sijui kwasababu nyaraka hizo hazijamzungumzia kabisa “
“Lakini unajua kuwa mheshimiwa ni mwanachama wa U-97”.Damiani alishangaa .
“kuna Umuhimu bwana Damiani kuniambia nyaraka hizo zinahusu nini “
“Nyaraka hizo zinahusu juu ya malii za Bruno basi hakuna lingine linalomuhusu mheshimiwa Henry” aliongea Damiani , japo kamsilikilza sana bwana huyu ila hakuwa akimuamini moja kwa moja , tabia yake ya kutoamini watu ndio ili,mfanya kumshuku kila mtu aliekuwa akimsogelea .
“una uhakika ?”
“ Ndio “.
“Kama ni kweli naomba nikupe nasaha , najua unataka kulipiza kisasi llakini kumbuka sana watu ambao unapambana nao sio watu bali ni shirika hivyo swala hili huwezi kulifanya mwenyewe , ukihitaji msaada wowote kutoka kwangu nipigie na hii “ alimpa kadi na kisha aliaga na akaondoka .
******
“Patrick kwanini uliongea maneno yale mbele ya mheshimiwa ilihali unajua kabisa mimi na wewe sasa hivi hatuna mahusiano na hilo lipo wazi”
Aliongea merina kwa msisitzo kabisa huku akionekana amechukizwa na kitendo cha Patrick , huo ni wakati ambao Merina na Patrick kama walivyo ahidiana walikutana ndani ya peacock hotel .
“Sina nia mbaya juu ya hilo Merina , wewe ndio hutaki kunielewa ,kwanini unakuwa mgumu kunipa nafasi merina nakupenda lakini hutaki kuliona hilo “
“Patrick hilo tushaliongea sana tu na nishakueleza juu ya hisia zangu juu yako na siwezi kujilazimisha nipo hapa kwa jambo moja tu nataka umwambie mheshimiwa kuwa mahusiano yetu yashakwisha isha .
“Unaamini Stephano lamberk au Damiani anakupenda kama ninavyo kupenda mimi” .
Merina alijikuta akipatwa na mshangao hakujua kama na Patrick alikuwa akijua kuwa Stephano lamberk ndio Damiani .
“Unamaanisha nini ?”
“Huna haja ya kuwa hivyo Merina najua kila kitu kwamba Stephano ndio Damiani na kwa ninavyo ona kabisa Stephano hakupendi kama ninavyokupenda mimi “
“ una uhakika gani juu ya hilo Pat , na hata kama hanipendi hilo ni juu yangu , swala lililonileta hapa nataka umwambie mheshimiwa kwamba mahusiano yetu yameisha , ukishindwa nitafanya hivyo “.
“ siwezi kufanya hivyo merina , nishamhakikishia baba nitakuoa “
“na mimi siwezi kujilazimisha kuolewa na wewe”
“Huna jinsi kama unampenda Damiani inabidi uolewa na mimi “
“Unamaanisha nini?”
“Nadhani unajua ninacho maanisha Merina “
“Damiani anaishi kama Stephano lamberk unafikiri ni kwasabu gani , jibu ni kwamba yupo hatarini kuna watu wanamtafuta na ni wewe wa kumlinda kwasasa vinginevyo nitaweka ukweli wazi “
“ Unataka nini Patrick “ Aliongea Merina maana aliogopa sana Damiani kuingia kwenye matatizo zaid na zaidi
“Najua hunipendi Merina , ila nataka tufunge ndoa “
“Nini ?”
“Ndio , njia pekee ya damiani kuwa salama , kwani mpaka sasa najua maadui zake wote”
Merina alijikuta akivuta pumzi na kuzitoa kwa kasi na kumwangalia Patrick ,na alimuona Patrick kama mtu ambae anamaanisha kwa kile anachokiongea , hakujua ajibu nini maana alijiona kama yupo kwenye mtego , aliwaza mambo mengi kwa wakati mmoja , kwanzia Janeth kuwa na mahusiano na Damiani na mengine mengi kwanzia siku ambayo wamekutana mpaka kufikia wakati huo.
“Nimekubali , ila sharti langu ni moja ukikubaliana na swala hilo basi nitakubali kufunga ndoa na wewe “ Patrick meno yote nje
“ jambo gani ?”
“Nataka unihakikishe usalama wa damiani , siku damiani atakapo patwa na shida yoyote inayohatarisha maisha yake basi mimi na wewe basi”
“kwa hio unataka niwe mlinzi wa Damiani ?”
“ Ndio namaanisha hivyo , kama huwezi basi hakuna ndoa na swala hili linawezekana sana kwani wewe ni mtoto wa raisi , unaweza kumwambia baba yako aweke wanausalama watakao mlinda “
“ahahahah… Merina naona hunipendi kabisa , ila kwasababu sitaki kukukosa na mimi nina sharti , hatuishii kufunga ndoa tu , ila nataka unizalie na mtoto ama watoto “.
“Ndio jukumu la kuwa mke hilo”
“ Then deal , ndoa tutafunga siku moja na mdogo wangu “.
ITAENDELEA
SEHEMU YA 77.
I AM BACK ( NIMERUDI )
Zikiwa zimepita siku kadhaa , viongozi wawakilishi wa U-97 walikaa kikao cha kusaini karatasi ya mkataba ambao ulikuwa ukihusu makubaliano ya Tanzania kutoa binadamu kwa ajili ya majaribio zidi yampango Zero , kikao hichi kilikuwa kikifanyika ndani ya hoteli ya Hyatt regency maeneo ya posta na kama kawaida Sam ndie aliekuwa akiongoza kikao hichi .
Watu waliokuwepo ndani ya hiki kikao walikuwa ni wale wale wakiongozwa na raisi mstaafu Ndalu lakini mheshmiwa Henry hakuwepo , mpango huo wa majaribio ulisomwa kwa kila mwanachama lakini pia walitoa mafanikio ya mheshimiwa Raisi kutia sahihi yake katikampango huo .
Baada ya kila mtu kuelewa hakuna hata mmoja aliepinga kutoweka sahihi katka mpango huo , kwani licha ya kusaini lakini pia mpango huo uliambatana na dau kubwa la pesa kwa kila mwanachama .
Baada ya mpango huu kusaniwa ndani ya usiku huo wa kikao siku iliofata waziri wa pesa alitangaza Tanzania kupata msaada wa matirioni ya pesa kutoka IMF huku pesa hizo zikielekezwa katika maswala ya afya.
Moja ya watu walifurahi pesa hizo kuingia nchini alikuwa ni Sam , kwani alijua pesa hizo hazikukusudiwa kuingizwa kwenye maswala ya afya bali kukamilisha mpango Zero ., bwana huyu ambae tamaa ya pesa ilikuwa imemgubika hakutaka kabisa kuwaza juu ya mpango huo ulikuwa ukihusu nini haswa , alichokuwa akiwaza ni pesa tu na sio kwake tu na kwa washilika wake pia, hakuna alifikiria kwa jicho la tatu juu ya athari za mpango huo kwa watanzania kwa ujumla.
****
Upande mwingine siku ambayo kikao cha UMOJA NAMBA TISINI NA SABA kinafanyika upande mwingine ndani ya hoteli ya Tulip kulikuwa na kikao kilichokiuwa kikifanyika , na kikao hiki kilikuwa kikiongozwa na Bwana matinde na wafuasi wake ukimtoaMerna hakuwa ameitwa kwenye kikao hichi lakini pia hakuwa mwanachama rasmi kwani alikuwa akishiriki kama mfadhili wa kuchangia upelelezi wa kupatikana kwa Damiani na jambo hilo lilikuwa lishafanikiwa kwa asilimia mia moja.
.” vipi alikutafuta ?”
“ bado hajanitafuta , ila naamini atanitafuta “
“ ni vyema akikutafuta kwani damiani ndio njia ya sisi kumtoa Henry madarakani “
“ haina haja ya kuwa na shaka juu ya hilo , nadhani kwa namna moja ama nyingine Damiani anaweza asiwe na Waraka wa mheshimiwa Bendera”
“ kwanini unasema hivyo “
“ Kama mwanausalama naamini kuna mtu mwingine anaweza akawa amekabidhiwa waraka huu , na mtu ambaye waraka huu umemlenga lazima ni damiani “
“Ni kweli kabisa , lakini kijana anaonekana japo ya kufoji barua ile ,bado hajakuamini , unaonaje tukiweza kufanya jambo la maana Zaidi kwake ili aweze kutuamini ?”
“ Nimelifikiria hilo pia , ila kwasasa nimemuweka Nurya aendelea kufatilia nyendo zake “
“Kwanini Nurya sio Zakayo ?”
“ Zakayo sio Mzalendo , zakayo anachowaza ni pesa tu na ni rahisi sana kutusaliti kama mtu atamuwekea dau kubwa”
“kama ni hivyo hakuna shida , kama Nurya kazi anaiweza basi swala hilo hatuna pingamizi nalo , lakini inabdi tuzungumzie ajenda ya pili kwa siku ya leo”
“Ni kweli , lazima tujue ni nani atashika madaraka baada ya Henry kung`olewa “.
“ mimi naamini mheshimiwa Matinde anatufaa “.aliongea kizito kabwela
“hapa hakuna anaefaa kushika madaraka kwa nchi hii “ aliongea Matinde na kuwafanya wote wamshangae
“ unamaanisha nini ?”
“mtu atakae shika madaraka inabidi sisi tumtengeneze na hawezi kutoka hapa ,kwani akitoka katika kundi letu ni ngumu kumkotrol”
“ umeongea vyema bwana Matnde “ aliongea mkuu wa majeshi Abdala .
“kwa hio mtu huyo atakuwa nani “.
“Askofu “Aliongea matinde
“ Unamaanisha askofu Jembe mbunge “. Aliuliza kizito .
“Inabidi tumuweke Jembe , na mipango yetu ya kuliongoza taifa hili kupitia yeye itafanikiwa , kwani Jembe anatamaa ya hela , na hata uchungaji wake sio wa halali kutoka kwa Mungu ni wa sadaka na nguvu za miujiza ni za kufoji.na ushahidi ninao”
“Naungana na Matinde juu ya hilo, tukifanikiwa kumuweka pale ikulu itakuwa rahisi kumuongoza kwa kila tunachotaka maana tutakuwa na udhaifu wake”
Kila mtu alikubaliana na Matinde juu ya kumuweka Askofu Jembe madarakani baada ya Henry kumuondosha .
Wakati hayo yanaendelea upande mwingine ndani ya hoteli hiyo bwana Pancho alikuwa na mashine yake ya kusikiliizia taarifa zake , na kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika kikao hicho alisikia vyema , na swala hilo kwa namna Fulani lilimuongopesha sana , ila alitabasamu kwani alikuwa amekamilisha kazi aliokuwa amepewa na mheshimiwa .
******
Patrick alikuwa amedhamiria kweli kumuoa msichana Merina , haku wa na utani hata kidogo , alikubali dili la mwanamke huyo kwa asilimia mia moja na baada ya mazungumzo yake na Merina hakutaka kukawia Zaidi , kwani aliamini akizembea kuna uwezekano wa damiani kupatwa na shida na ndoa kufa hivyo baada ya kufikiria sana hatimae swala hilo ilibidia amshirikishe baba yake , na siku tatu mbele alikuwa ashaongea na baba yake , na mheshimiwa Alikubalia na kile mwanae alichokuwa akihitaji na hivyo aliamua kumtimizia kwa kuhakikisha kuwa Damiani anakuwa salama lakini jambo hilo lilazaa linguine kwa muheshimiwa , kwani ndio siku aliokuja kugundua kuwa Stephano lamberk ndie damiani jambo ambalo lilimshangaza sana/.
Baada ya siku kadhaa ya Patrick kuongea na baba yake juu ya swala hilo agent z aliitwa ikulu tena , na mheshimiwa raisi .
“kwanzia sasa kazi zako zote ulizo nazo zimesitishwa “
“unamaanisha nini mheshimiwa ?”
“ unayo kazi moja tu kwa sasa ni kuhakikisha Damiani anakuwa saama , lakini wakati huo ukinifanikishia jambo moja “
“ jambo gani ?”
“nataka kujua nayaraka Damiani alizoachiwa na Bruno zinahusiana na nini na ili kulifanikisha hilo nataka umfanye akuamini katika mipango yake yote”
“Nimekuelewa muheshimiwa “.
“ Swala hili ni juu yangu mimi na wewe lakin pia kwa usalama wa taifa , nahitaji lifanyike kwa siri sana , mafunzo yako ya kipelelezi yalifadhiliwa na taifa , hivyo ni jukumu lako kuhakikisha taifa lipo salama kama mwanausalama”
“ nimekuelewa muheshimiwa “
Baada tu ya zakayo kumaliza mazungumzo na mheshimiwa , Suzzane na yeye aliingia ndani ya ofisi hio ya mheshimiwa kwani na yeye alikuwa ameitwa.
“Suzzane nataka kwanzia sasa uachane na kumfatilia Damiani , ila kazi yako iwe ni kuhakikisha unawajua hawa wanaojiita WAZALENDO ni kina nani na wana dhumuni gani kwangu na kwa taifa hili “
“Mheshimiwa lakini Damiani ni Stephano na tayari tuna kila sababu ya kumkamata kwanini niachane na hilo “.
“Suzzane hio kazi kwa sasa achana nayo , na swala lolote linalohusiana na Damiani naomba linifikie kabla ya kufanya maamuzi “.
“Sawa mheshimiwa “
*****
DAR ES SALAAM –JNIA
Ndege ya shirika la Emirates ilitua ndani ya uwanja huu wa kimataifa , na baada ya madakika kadhaa ya kutua , mbele ya mlango katika jengo la terminal 3 alitoka kijana mmoja wa makamo mnene kidogo na mrefu saizi ya kati huku akiwa amevalia suti yake nyeusi kabisa ya bei ghali , huku mkononi akiwa na begi .
Kijana huyu alitembea mpaka upande wa Taksi na kisha alipokelewa na kuingia na kuondoka maeneo hayo ya uwanja wa ndege , dakika kadhaa mbele alikuwa ndani ya hoteli ya nyota tano ya Seerena , alifanya utaratibu wa kawaida na kisha alipatiwa chumba , na mara baada ya kuingia kwenye chumba hiko kikubwa cha hadhi hatimae alitoa simu yake ambayo ilionekana ilikuwa imezimwa kwa muda mrefu na kisha mara baada ya kuiwasha , alitafuta namba Fulani na kisha alipiga.
“I am back “
“ welcome back Karim in Tanzania “
“Asante sana madam “
“ kazi yako ni moja , ni kuhakikisha unafanya yale ulioagizwa na marehemu kabla ya kifo chake”
“ Nimejiandaa kwa ajili ya jilo madam wala usiwe na wasiwasi “
“ safi , nikutakie kazi njema “
“ asante madam “
“ hatimae nimerudi tena Tanzania kwa mara nyingine , Mheshimiwa bendera nipo tayari kukamilisha lile ulilolianzisha chini ya mpango wa MZALENDO “aliongea kijana huyu kwa sauti yake nzito .
ITAENDELEA IJUMAA JIONI
Bado Tunaendelea Wadau Bado Sana Hatujaufahamu Vyema Umoja Namba Tisini Na Saba
Nani Anao Waraka Wa Raisi Kabla Ya Kifo Chake Unahusiana Na Niini ?.
Mpango X Ni Mpango Gani , Mpango Zero Ni Mpango Gani ??
Endelea Kujiuliza Hayo Maswali Tukisubilia Mwendelezo
Tuma 1500 kwa namba 0687151346 jina ISSAI SINGANO nikutumie mwendelezo watsapp huo ni mchango tu kwa ajili ya vocha .
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…