Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,748
Makala hii inapatika kwa ukamilifu wake kwenye kitabu changu kipya cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-
Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-
Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457
Au bofya link hapa chini kunitumia ujumbe moja kwa moja whatsApp
UJASUSI SEBULENI KWETU
“Uongo ndio hali halisi ya akili ya binadamu, na akili ya bindamu imejazwa kwa uongo. Tunaishi katika nyakati ambazo mstari unaotenganisha uongo na ukweli ni mwembamba sana kiasi kwamba imekuwa vigumu kutenganisha uongo ni upi na ukweli ni upi. Kipo kikundi cha watu ambao wamedhamiria kwa dhati kabisa kuhakikisha tunaishi gizani na kamwe tusiujue ukweli. Andishi hili ni zawadi yangu kwa kila mtu mwenye kiu ya kutaka kuanza kutoa tongotongo machoni aanze kuona uhalisia wa dunia ambayo tunaishi ndani yake.”
- Habibu B. Anga “The Bold”, April 2018
Gari aina ya Suzuki Samurai illikuwa imepaki kando ya barabara ya Old Bagamoyo maeneo fulani kwenye barabara inayochepuka kwenda Namanga kukaribia kabisa makutano ya barabara Morocco. Mahala hapa ambako walikuwa wamesimamisha gari walikuona wanaona majengo ya ubalozi wa Marekani mbele yao. Ndani ya gari kulikuwa na vijana wawili wa makamo. Wa kwanza alikuwa Hamisi na wa pili alikuwa ni mwenzake waliyependelea kumita ‘Ahmed Mjerumani’. Kuna maelekezo fulani hivi ambayo Hamisi alikuwa anampa Ahmed Mjerumani kuhusu jengo la Ubalozi.
Jengo hilo la ghorofa tatu ambalo asili yake lilijengwa na Waisrael mwanzoni mwa miaka ya sabini kabla ya kuuzwa kwa Wamarekani katikati mwa miaka ya sabini baada ya Tanzania kuvunja mahusiano ya Kidiplomasia na Israel kufuatia vita ya Israel na Waarabu mwaka 1973. Katika eneo hili kulikuwa na majengo matatu. Kulikuwa na jengo lenyewe la ubalozi na pembeni yake umbali wa kama mita mia moja hivi kulikuwa na jengo la makazi ya kuishi ya balozi. Eneo la mbele ya ubalozi kulikuwa na jengo lingine la ghorofa nne ambalo likuwa linajengwa. Majengo yote haya ya ubalozi yalikuwa ndani ya uzio wa ukuta wenye vyuma juu ambao ulikuwa unapakana kwa umbali wa futi ishirini na tano kutoka kwenye barabara inayokatisha hapo kwenda eneo la Namanga. Mbele ya majengo ya ubaloni kwenye geti la kuingilia kulikuwa na vizuizi viwili vya ukaguzi ambavyo vyombo vya usafiri kama magari yalikuwa yanakaguliwa kabla ya kuingia ndani ya ubalozi.
Hamisi na Ahmed Mjerumani baada ya kusimama pale walipo kwa dakika kadhaa waling’oa gari na kuendesha kuifuata barabara inayoelekea Namanga. Kama dakika kumi tena baadae gari ile ile aina ya Suzuki Samurai ilipita tena nje ya ubalozi na ilipoifikia Old Bagamoyo Road ilisimama tena kwa muda wa kama dakika tano hivi na kisha kuondoka kufuata makutano ya barabara ya Morocco na kisha kupinda kona kufuata barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kuelekea maeneo ya katikati ya mji.
Hakuna ambaye alikuwa amegundua kitu hiki kwa wakati ule wala kutilia shaka gari ile aina ya Suzuki kukatiza na kusimama mbele ya ubalozi wa Marekani mara mbili kwa siku ile, lakini kumbe chini kwa chini kulikuwa na mpango wa hatari zaidi ambao ulikuwa unaelekea kutimilika, mpango ambao ungekuja kusababisha hata kubadilishwa kwa mbinu nyingi za utendaji wa shirika la ujasusi la CIA na kusababisha tukio ambalo litakumbukwa vizazi na vizazi.
Mapema mwaka 1998, Dar es Salaam Tanzania
Kama ilivyo kawaida yake katika siku zote, alikuwa amewasili katika baiskeli yake aina ya ‘phoenix’ ambayo haikuwa mpya sana lakini pia ilikuwa bado haijachoka sana. Tofauti na siku zote ambazo amekuwa akiwasili msikitini hapo katika muda wa ibada tu, leo alikuwa amefika msikitini mapema mno kama muda wa saa nne asubuhi kwa kikao maalumu. Hakikuwa kikao hasa tukiongea kwa usahihi zaidi bali alifika hapo msikitini ilia aje kuchukuliwa na jamaa anayeenda kwa jina la Hamisi.
Baada ya kusimamisha baiskeli yake mahali sahihi kabisa pale msikitini akasogea mpaka kwenye benchi lililo karibu nje ya msikiti na kuketi.
“Fupiiiii.!” Sauti ya mtu ilimuita akiwa anakuja kuelekea pale ambako alikuwa amekaa. Hamisi alikuwa amewasili.
Baada ya kusalimiana na kujuliana hali waliongozana mpaka barabarani ambako Hamisi alikuwa amepaki gari. Ilikuwa nigari aina ya Nissan Atlas toleo la mwaka 1987 lakini ikiwa katika hali nzuri kabsia. Wote wawili walikwea ndani ya gari na kwenda moja kwa moja mpaka maeneo ya Kariakoo katika mgahawa wa kimanga na kuanza kupata vitafunwa kwa juisi ya matunda.
Hamisi na ‘Fupi’ waikuwa na vitu kadhaa ambavyo vilikuwa na mfanano mkubwa. Fupi ni mzaliwa wa visiwa vya Zanzibar na alihamia hapa Dar es Salaam akijihusisha na biashara ndogo ndogo lakini sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa ameitoa kuwa kama ‘tabligh’ ambapo alikuwa anasafiri sehemu mbalimbali za nchi kufanya mihadhara na kulingania imani ya Kiislamu. Hamisi naye alikuwa ni mzaliwa wa kisiwani Pemba kijiji cha Mdimuni katika familia ya hali ya chini kabisa. Umasikini huu katika familia yao ulitokana na baba yake kufariki kipindi Hamisi akiwa mdogo kabisa. Licha ya umasikini huu lakini Hamisi alilelewa katia malezi mema kabisa ya hofu ya Mungu na upendo kwa majirani zao. Hivyo hata sasa ukubwani mwake, Hamisi alikuwa ni mtu mcheshi, mwenye heshima na aliyejawa na upendo. Alihamia hapa Dar es Salaam kumfuata kaka yake na ambaye alikuwa anamiliki duka maeneo ya Kariakoo ambapo baada ya Hamisi kuwasili Dar es Salaam kazi yake ilikuwa ni kuuza duka la kaka yake. Lakini kwa sasa Hamisi alikuwa anaishi maisha ya kujitegemea na kitendo cha kuendesha mpaka gari kilifanya awe moja ya vijana wa kuigwa mtaani.
Baada ya kupata vitafunwa kwa juisi na mazungumzo ya hapa na pale, Hamisi alikwenda moja kwa moja kwenye suala ambalo limemfanya kumuomba Fupi waonane. Hamisi hakuongea maneno mengi sana bali alimueleza fupi kwamba anataka kumpa kusudi la maisha yake, amshirikishe kwenye suala la muhimu zaidi ambalo hatokuja kupata fursa tena ya kushiriki kwenye maisha yake yote… akamuueleza kwa kifupi tu,
“Nataka ushiriki katika Oparesheni Al-Aqsa..!”
Fupi alielewa Al-qsa ni nini lakini hakuelewa moja kwa moja maana halisi ya kile ambacho Hamisi alikuwa anamueleza kwa mafumbo japo alihisi.
Watu hawa wawili ambao ninawaeleza hapa ni vijana wa miaka ishirini na nne wote wawili, ambao muda huu unaposoma maandishi haya wanatumikia vifungo vya maisha nchini Marekani wote wawili katika gereza hatari zaidi la Supermax ADX Florence. Vijana hawa walikuwa ni Ahmed Ghailani ambaye marafiki zake walipenda kumuita jina la utani la ‘Fupi’ na Halfan Hamisi Mohamed ambaye maswahiba zake walimuita ‘KK Mohamed’.
Kama ambavyo nimeeleza awali kwamba Mohamed alikuwa ni mcha Mungu na mtu mpole sana na mkarimu, lakini kulikuwa na siri kubwa sana nyuma ya pazia katika maisha yake ambayo watu walikuwa hawaijui, hata ndugu zake na rafiki zake wa karibu. Ilikuwa ni siri ambayo watu wachache sana waliijua kuhusu uhalisia wa maisha ya Hamisi. Ni vijana hawa wawili ambao wiki chache mbele walikuja kushiriki kwenye tukio ambalo lilikuja kuitikisa dunia na ulimwengu wa ujasusi na kuwafanya CIA kuhaha kama wamechanganyikiwa. Lakini swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni namna gani vijana hawa wadogo wawili kutoka visiwani Zanzibar waliweza kushiriki kwenye moja ya matukio adhimu ya kihalifu kuwahi kutokea kwenye historia?
Ili tuweze kuelewa vizuri kile ambacho kilitokea tunapaswa kurudi miaka kadhaa nyuma…
Ilikuwa ni mwaka 1994 ambapo Hamisi kwa mara ya kwanza alijenga ukaribu na moja ya waumini kwenye moja ya msikiti maarufu katikati ya mji wa Dar es Salaam. Muumini huyo ambaye wengi walimzoea kwa kumuita jina la utani la “Bwana Somba” au “Bwana Samaki” alikuwa ni mkazi wa mji wa Mombasa na alikuwa anakuja Dar es Salaam mara kadhaa kutokana na shughuli zake za uvuvi. Alikuwa anamiliki boti ya kisasa kabisa ya uvuvi ambayo ilikuwa inafanya shughuli hiyo katika ukanda huu wa pwani ya Afrika mashariki. Majina halisi ya huyu “Bwana Somba” alikuwa anaitwa Mohamed Sadiq Odeh, na kabla ya shughuli hii ya uvuvi Odeh aiwahi kufanya kazi kwenye moja ya kampuni za usafirishaji bidhaa yenye ofisi zake hapa Tanzania hivyo alikuwa na marafiki wa kutosha tu na ndio maana mara kwamara akiwa kwenye shughuli zke za uvuvi alipendelea kufika Dar es Salaa na kufanya ibada kwenye msikiti ule ule ambao Hamisi naye alikuwa anakwenda kuswali.
Hamisi na Odeh walijenga urafiki mwaka huo huo 1994 na kuanza kuwa karibu. Kutokana na urafiki wao huu ndipo ambapo Odeh alifanikiwa kumshawishi Hamisi kujiunga katika ‘mtandao’ ambao Odeh alikuwa anafanya nao kazi. Alimweza kuwa yeye ni mwanachama wa mtandao ambao wenyewe wanauita Al-Qaida. Kipindi hicho Al-Qaida hakiwa inajulikana kama ilivyo sasa. Odeh alimueleza Hamisi kwamba mtandao wao huo una lengo kuu la kupigania imani na kupambana na wale wote ambao walikuwa wanaonekana ni wapinzani wa dini yao. Kutokana na Hamisi kuwa mwenye mahaba sana na dini ilikuwa rahisi kabisa kwake kushawishika kuingia katika mtandao huo wa wapigania imani kama ambavyo wenyewe walijipambanua.
Kwa kutumia akiba yake ambayo alikuwa ameitunza kwa miaka mingi akifanya kazi dukani kwa kaka yake Kariakoo, Hamisi alisafiri mpaka nchini Afghanistan na moja kwa moja kujiunga katika kambi za Al-Qaida ambako alipatiwa mafunzo ya awali ambayo yalihusisha utumiaji wa silaha nyepesi, matumizi ya mabomu ya roketi za begani pamoja na roketi za udunguaji (Surface to air missile). Hamisi alipata mafunzo haya katika kambi ya Al-Qaida iliyopo eneo la Manakando iliyoko hapo nchini Afghanistan. Baada ya kuhitimu mafunzo haya Hamisi alikuwa ameweka nia ya kutaka kwenda Balkans au Chechnya ambako kulikuwa na vita ikiendelea kwa maika mingi. Chechya ni moja ya maeneo ya Ulaya yenye idadi kubwa zaidi ya Waisilamu na kwa kipindi hicho wapiganaji wengi wenye msimamo mkali ilikuwa ni ndoto yao kutaka kwenda huko ili kusaidia kwenye vita hiyo. Lakini eneo hili linadhibitiwa nan chi ya Urusi na kuingia si suala jepesi. Hamisi alijaribu mara kadhaa kuingia Chechnya bila mafanikio. Baada ya majaribio kadhaa ya kuingia kushindikana alikata tama na kurejea nyumbani Tanzania.
Akiwa nchini Tanzania, katikati ya miaka ya tisini viongozi wake waliwasiliana naye wakitaka aende nchini Somalia ambako kulikuwa na mapigano kati ya vikundi vya wazawa na wanajeshi wa kigeni ambao walikuwa nchini humo ‘kulinda amani’. Moja kati ya vikundiambavyovilikuwa na ushawishi mkubwa kilikuwa ni kikundi ambacho kilikuwa kinaongozwa na Mohammed Farrah Aidid. Kwahiyo Hamisi alitumwa na viongozi wake kwenda huko Somalia ili kuwa mkufunzi wa matumizi ya silaha kwa wapiganaji wa Aidid. Alikaa huko mpaka kufikiamwaka 1998. Mnamo mwezi March mwaka 1998jukumu ambalo alikuwa ametumwa na viongozi wake wa Al-Qaida kulifanya Somalia lilikuwa limekamilika na alifunga safari kurejea nchini Tanzania. Lakini katika safari yake hiyo ya kurejea Tanzania alipitia Mombasa kwa swahiba wake Odeh, “Bwana Somba” ambaye ndiye alimshawishi kujiunga na mtandao wa Al-Qaida. Akiwa Mombasa Odeh alimueleza Hamisi kwamba kuna kazi maalumu ambayo wiki chache zijazo atatakiwa waanze maandalizi ya kuifanya. Hamisi alipouliza ni ‘Kazi’ gani, Odeh alimjibu kwamba hata yeye hafahamu ni kazi gani haswa lakini amepewa maelezo hayo na uongozi wa juu. Na hivyo ndivyo ambavyo mtandao wa Al-Qaida unavyofanya kazi, ni watu wachache sana hasa hasa viongozi wa juu pekee wanakuwa wanajua masuala yote kuhusu oparesheni kabla ya kufanyika. Hii inafanyika makusudi watu wachache kufahamu ili kuepusha siri kuvuja kama ikitokea vijana wao hao wakikamatwa kabla ya oparesheni kutekelezwa.
Hamisi akarejea Tanzania kusubiri maelekezo zaidi kutoka uongozi wa juu.
Itaendelea...
Hbibu B. Anga "The Bold" - 0718 096 811
To Infinity and Beyond
SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA