Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 40,359
- 62,617
- Nipo hapa mjini nashangaa shangaa mazingira,ila nimefikia kwenye hotel x;Siku 2 zilizopita chumba kilichojirani na chumba changu alikuja mgeni mmama mtu mzima....sasa baada ya kutoka kwenye mihangaiko yangu na kurudi hapo hotelini,na nilipoanza kufungua chumba yule mmama akaniita;akaniambia kijana huu mlango wangu haufungi vizuri hebu jaribu kuufunga....nikatoa ushirikiano ukafungika.
- Jana usiku nipo restaurant napiga bia kwenye muda wa saa tano....akaibuka tena na kuomba nimpe offer ya bia nikafanya hivyo;leo nikaamua niende viwanja vya nje,wakati naagiza mahitaji yangu muhudumu akaniomba tukae meza moja,nami nikamkubalia;bahati mbaya na yule mmama alikuwa kwenye hicho kiwanja....baada kama ya dakika kadhaa yule mmama akaja kutupa salamu na kusema jirani upo huku;mi kwa sababu niko mchangamfu nikamjibu nimekuja kubadilisha mazingira....yule muhudumu akashangaa na kuniuliza,umemjuaje huyu?
- Nikamuambia tuko naye hotel moja....jibu alilonijibu ni kuwa huyo mtu anatoka mkoani na huwa anakuja mjini kwa ajili ya kuuza k,na huwa anachukua vyumba kwenye mahotel na akimpata mtu lazima alipe garama zote.Hapo ndipo nikajua katika haya maisha kila mtu ana mikakati yake.Anatumia mapenzi kama fursa,we mwanaume kuwa makini.