Msuruhishi
Senior Member
- Jun 18, 2008
- 103
- 38
kashfa ya mr jairo ya uchangishaji wa sh billion moja ili kugharimia uwasilishwaji wa bajeti ,jambo hili linatatiza sana. uchunguzi wa kina ufanywe ni kwa nini mr jairo alifikia hatua hiyo. wabunge wa ccm mshikamano mlioonyesha kwenye makadirio ya bajeti ya wizara ya nishati kama ingekuwa kwa maswala yote nchi ingepiga hatua. wabunge wa ccm mkumbuke nchi ina mgao wa giza kwa sababu ya mikataba tata kam Iptl; Richmond n.k ni vizuri muwashughulikie wahusika wote mnawajua . changamoto kwa wabunge nyinyi ndiyo wasimamizi wa serikali ,shughulikieni suala la elimu ambayo inashuka kila siku,bodi ya mikopo iongezewe fedha ili iweze kukopesha wanafunzi wengi,sasa pigeni kelele fedha za rada ziingizwe mfuko wa elimu ili tuweze kusomesha wataalamu wa kutosha kama madaktari,waalimu na mainjiniaKatika hotuba ya 'kuahirisha' kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini'u Waziri Mkuu Pinda alitumia lugha ambayo siyo yake tunayoifahamu; hasa pale alipozungumza kuhusu barua ya Jairo iliyoibuliwa na Mh. Beatrice Shelukindo. Kwa lugha rahisi, Waziri Mkuu alisema Katibu Mkuu Jairo ni wa kufukuzwa tu ila yeye hana madaraka na hilo. Alituaminisha kuwa kama Rais Kikwete 'asingekuwa hewani", njiani kwenda Sauzi, angempa taarifa tu na Raisi angetamka amri ya kumfuta kazi Jairo. Tukumbuke kuwa kabla ya kumteua Jairo kuwa Katibu Mkuu, Jairo huyo alikuwa mtu wa karibu sana na Rais huyo, kama Msaidizi wake mkuu katika Ofisi Binafsi (Private Office) ya Rais. Sasa Rais yuko njia panda. Amfukuze Jairo mtu wake wa karibu kiasi hicho? Asipomfukuza, Pinda atawaambia nini Watanzania?
Mkuu huyu Pinda hana uwezo kisheria completely kumfukuza kazi Jairo. Yeye si mamlaka iliyomwajiri. Rais ndo mwenye mamlaka hayo. Naye atakachokifanya atatengua uteuzi wa Jairo endapo kweli anakusudia kumwondoa. Ama wakati wa Mwinyi kulikuwa na msemo, "kumstaafisha kwa manufaa ya umma".Pinda wala sio jasiri madaraka alikuwanayo alikuwa na uwezo wa kumfukuza kazi Jairo! Ebu jiulize Pinda lini alishawahi kumfukuza kazi mtu, ata hawo walio chini yake
Nasikia Pinda alilia sana baada ya kikao cha kumwuumbua Jairo