Ujasiri wa Pinda Umetoka Wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujasiri wa Pinda Umetoka Wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msuruhishi, Jul 19, 2011.

 1. M

  Msuruhishi Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Katika hotuba ya 'kuahirisha' kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini'u Waziri Mkuu Pinda alitumia lugha ambayo siyo yake tunayoifahamu; hasa pale alipozungumza kuhusu barua ya Jairo iliyoibuliwa na Mh. Beatrice Shelukindo. Kwa lugha rahisi, Waziri Mkuu alisema Katibu Mkuu Jairo ni wa kufukuzwa tu ila yeye hana madaraka na hilo. Alituaminisha kuwa kama Rais Kikwete 'asingekuwa hewani", njiani kwenda Sauzi, angempa taarifa tu na Raisi angetamka amri ya kumfuta kazi Jairo. Tukumbuke kuwa kabla ya kumteua Jairo kuwa Katibu Mkuu, Jairo huyo alikuwa mtu wa karibu sana na Rais huyo, kama Msaidizi wake mkuu katika Ofisi Binafsi (Private Office) ya Rais. Sasa Rais yuko njia panda. Amfukuze Jairo mtu wake wa karibu kiasi hicho? Asipomfukuza, Pinda atawaambia nini Watanzania?
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hata naye amechoka na chama chake cha magamba!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  jairo kaachia kabla hawajafanya maamuzi magumu!!!
   
Loading...