Ujanja wa Mfalme Juha

Abdul Amour

Member
Jun 2, 2013
5
0
Wakati Mwalimu Nyerere alipokwenda kuonana na Mzee Abeid Amani Karume kuhusu kuziunganisha Nchi mbili huru Zanzibar na Tanganyika alikuwa na dhamira ya kuitawala Tanganyika Maisha. Ili afanikiwe na dhamira yake hio alilazimika kuiweka Zanzibar chini ya himaya yake kwa maslahi yake ili isiwe mfano wa kuigwa na Watanganyika wakaweza kumuondoa katika madaraka.

Kwani ieleweke kuwa wakati nchi mbili hizo kabla na baada ya kuungana Watanganika walinyimwa haki za msingi kama vile uhuru wa matangazo ya TV ambayo kwa Zanzibar ilishazoeleka mwazoni mwa miaka ya sabiini ikiwa ni nchi ya mwanzo kwa Afrika mashariki kuwa na color TV na ni ya tatu kwa Afrika. ili aendelee kuwatawala watanganyika Nyerere alilazimika kuwaweka kizani hadi mwanzoni mwa miaka ya themanini.

Baada ya kufanikiwa kuziunganisha nchi mbili hizo aliendelea na ujanja wake wa kutaka kuifuta Zanzibar katika ramani ya dunia kwa kuandika katiba ya mwanzo na kuifanya Tanzania ni nchi moja na Zanzibar kuanza kusahaulika kama ilikuwa ni nchi ndani ya Tanzania. kwa ufupi alilazimika kuandika historia mpya ambayo iliipoteza Tanganyika hadi hii leo kutoka katika ramani ya dunia.

Katika kufanya hivo Tanganyika imepoteza Nchi, Taifa, mipaka ya nchi yake wimbo wa Taifa, bendera na alama za utaifa wa watanganika hadi kufikia hivi sasa. Rasimu ya katiba mpya inasema kuwe na Tanganyika sasa nani wa kuirejesha jee ni CCM au wadau wote wa Tanganyika? ukiondoa ukumbi wa bunge la Tanzania na ikulu ya Rais wapi wataweza kukutana kwa utendaji wa shughuli za Tangayika na jee kutakuwa na mchakato mwengine kwa watanganyika wa kutafuta katiba yao. Hamuoni kuwa Mfalme Juha kawaponza watanganyika kwa kutaka kuitoa Zanzibar katika ramani ya Dunia?
 
Hakuna atae weza labda watanganyika wenyewe wakiamua kuirejesha tanganyika yao,naamini watakapo weka uzalendo wa taifa lao la mbele huenda wakarejesha uhuru wao wa watanganyika kujiamuli,watafanya kosa kubwa kuwasikiliza wanasiasa wachumia tumbo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom