Uingizwaji wa bidhaa feki na madhara yake kwa Tanzania

Regulator

Member
Feb 17, 2016
22
17
Uingizwaji wa bidhaa feki inchini Tanzania inabidi litangazwe kama janga la kitaifa na linahitaji juhudi za kimakusudi kukabiliana nalo. Ebu angalia jinsi TFDA na TBS wanavyoteketeza bidhaa feki au zilizoisha mda wake wa matumizi. Swala la kujiuliza hizi bidhaa feki zinapitia bandari gani? na je mpaka zinakuja kugundulika kuwa feki zimeumiza watanzania wangapi? Nani wa kuwajibishwa kwa hili? Je mtandao huo haujulikani?
Leo tuna bandari nyingi sana bubu zinazotumika kupitishia bidhaa za magendo na feki zinajulukana kabisa. Sasa kwa nini kisiundwe kikosi maalum cha kukabiliana na janga hili la uingizwaji wa bidhaa za magendo na feki kitakacho jumuisha vyomba vyote vya usalama? Leo tumeshuhudia jinsi sukari, mafuta, matairi ya magari, spare party za magari na nk vinavyoingizwa inchi kwa njia zisizo halali hizi si kwamba ni hatari tu kwa maisha ya watanzania pia ni hatari kwa ustawi wa uchumi wetu kumbuka hazilipiwi kodi hizi.
My take
Mamlaka husika hima shughurikieni hili msifurahihie tu kukama na kuteketeza hizo bidha feki wakati tayari zimeshatumiwa na watanzania wengi zuieni kabisa zisiingie inchini Tanzania siyo dampo la bidhaa feki
 
Back
Top Bottom