Uingereza yawapa tahadhari raia wake wanaosafiri kwenda Tanzania

Uhalisia hakuna huo ugonjwa ila wanayao tu wangeyasema ili wote tujue.hata kama kweli nchi hii inamatatizo mengi lakini haiwezi kuficha jambo lahatari kama hilo.nipo pamoja na serikali ktk hili
 
Hahaha mabeberu wanatuonea wivu donor country sio

Huku tunapewa ArV zao kila mwezi

Waondoke hawa wasitubabaishe tutatumia mitishmba 😅😅
Swali la msingi la kujiuliza ni kwanini wana uchungu na Afrika sana kuliko kawaida. Hapa ndipo napopata funzo kwamba ukiona mfugaji anampenda sana mfugo wake si kwamba ni upendo wa agape bali anampenda kwa kuwa anajua ni kitoweo anayetembea!
 
Hahaha so una maomi gani mkuu
 
Ma mbwa hawa watatuzushia na kutuletea maginjwa ya kila aina kweli hii ni vita ya kiuchumi na mabeberu
 
Serikali ya Uingereza imetoa tahadhari kwa raia wa nchi hiyo wanaosafiri kuelekea nchini Tanzania juu ya ''uwezekano'' wa kuwepo Ebola katika taifa hilo la mashariki mwa Afrika

Kulingana na taarifa tahadhari hiyo ya Uingereza mtu mmoja alifariki dunia nchini Tanzania mwezi wa Septemba 2019. Imeongeza kuwa inaonekana kuwa huenda kifo chake kilikuwa huenda kina uhusiano na Ebola. Serikali ya Uingereza kupitia wavuti wake pia imewaarifu raia wake kuwa shirika la afya duniani WHO clinaendelea kuchunguza na limetoa taarifa.

''Ubalozi wa Uingereza jijini Dar es Salaam inawasiliana na maafisa wa Tanzania na mashirika ya afya ya kimataifa, tahadhari hii itafanyiwa marekebisho pale taarifa mpya zitakapopatikana. ''Mnapaswa kufuatilia taarifa mpya kuhusu mabadiliko yoyote kwenye Mtandao wa Afya kuhusu safari na kituo na mitandao ya WHO'', imeongeza taarifa hiyo.

Tahadhari hii ya Uingereza imekuja baada ya taifa la Marekani pia mwishoni mwa juma kuwaonya raia wake kuchukua tahadhari ya kiwango cha juu wakati wanapozuru nchini Tanzania kufuatia wasiwasi wa ugonjwa wa ebola, ikiitaka nchi hiyo ya Afrika mashariki kutoa habari kuhusu visa vya ebola nchini humo kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

''Wanaozuru Tanzania wanapaswa kuwa waangalifu sana'' , idara ya maswala ya kigeni ilisema siku ya Ijumaa katika tahadhari yao ya usafiri kufuatia kifo kinachohusishwa na ugonjwa huo mjini Dar es salaam.

Tanzania ilikana ripoti hiyo ikisema kuwa hakuna visa vya ebola vilivyoripotiwa, lakini kwa sasa serikali hiyo ipo katika shinikizo kali kutoa ufafanuzi kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Chini ya kanuni za Afya za Kimataifa, makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama, nchi zinalazimika kuiarifu WHO mara tu zitakapokuwa na milipuko ya magonjwa makubwa ya kuambukiza ambayo yanaweza kuwa hatari kwa majirani zao na ulimwengu mpana.

Serikali za Afrika mashariki pamoja na zile za Afrika ya kati zimekuwa katika tahadhari ya kiwango cha juu kutokana na uwezekano wa maambukikizi ya ugonjwa huo kutoka DR Congo ambapo takriban watu 2,100 wamefariki kufuatia mlipuko wa ebola.

Mataifa ya Tanzania na DR Congo yanapakana na mto ulioyatenga.

Katika hatua isio ya kawaida, Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki iliyopita lilisema kwamba, kinyume na kanuni za afya za kimataifa, Tanzania ilikuwa ikikataa kutoa maelezo ya watuhumiwa.

Siku chache mapema, mkuu wa Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa alisafiri kwenda Tanzania kwa agizo la waziri wa Afya wa Marekani Alex Azar, ambaye pia alikuwa amekosoa nchi hiyo kwa kutotoa habari.

WHO ilisema kwamba, licha ya kwamba ina wasiwasi kuhusu ukosefu wa uwazi, haina ushahidi wa kuwepo kwa Ebola nchini Tanzania, lakini ilikatiza hatua za adhabu na kusisitiza kwamba ilitoa ushauri wa kutosafiri nchini humo mbali na vikwazo vya kibiashara.

Siku ya Jumanne Tanzania ilifanya mazungumzo na mwakilishi wa ndani wa shirika la afya duniani WHO kuhusu madai yake.

Katikati ya mwezi Septemba, waziri wa afya alisema serikali ilichunguza kesi mbili za ugonjwa usiojulikana , lakini hawakupata ugonjwa huo.
 
Kama. IPO mbona hatuambukizani ili vifo viwe shuhuda?
Hawa wanampango wa kuleta vi ebora chini ya uchunguzi.
Fukuzeni kabisa
 
wanakoua watu SA wanaona kupo salama huku ndio hakupo salama ni wakupuuzwa hawa mabeberu...
 
Wangese wameshafikiria njia sahihi ya kuwaua wa TZ ni kuwaletea EBOLA wanaanza kwa kuwapa taarifa watu wao nililiona hili kitambo sana
 
Hivi majuzi, ubalozi wa USA ulitoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini. Na ikasemekana kuwa kuna mwanamke mmoja alifariki kwa ugonjwa wa Ebola.

Leo tena, Uingereza na wao wametoa tahadhari kwa raia wao wanaotaka kuja Tanzania kwa kuwaambia kuwa kuna tishio la Ebola hapa nchini.

Hili swala kwa upande wangu naliangalia kwa namna mbili.

•Kipropaganda
Marekani na Uingereza ni washirika wa karibu sana, huenda kuna propaganda wanataka kueneza hapa nchini, au wanataka kuuleta huu ugonjwa hapa nchini, then baadae tutaenda kuwaomba msaada wa fedha za kupambana nao, hapo na wao ndio watakuja na terms zao kwamba ili watusaidie lazima na sisi tuwape rasilimali zetu. Nadhani wanalenga zaidi RASILIMALI zetu.

Kwanini huu ugonjwa hauwapati wazungu?
Kwanini Africa tu.

Hoja nyingine ni hii,
•Huenda ugonjwa upo kweli, ila serikali inaficha.
Kumbuka Marekani na Uingereza ni moja ya nchi zenye intelligence ya hali ya juu sana, so wakati mwingine wanapotoa tahadhari kama hizi huwa hawakurupuki, inawezekana ikawa huu ugonjwa upo mamlaka zetu zinapuuzia au zinajua ila zinaficha ukweli.

Ni vyema kama upo tujue, ili sisi raia tuanze kuchukua tahadhari mapema.
 
Back
Top Bottom