ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Astute ni nyambizi mpya kabisa zinazotarajiwa kuanza kazi kwenye jeshi la majini la Uingereza kuanzia mwaka 2018.
Nyambizi hyo inaendeshwa kwa nguvu za nyuklia pia inatajwa kua ni nyambizi kimya sana kuliko zote jambo linalofanya kua ngumu kujulikana ama kuonekana na adui.
Inaarifiwa kwamba nyambizi hii ina uwezo wa kukaa ndani ya maji hadi miaka 25 bila ya kutokeza juu labda kwa ajili ya kuongeza hifadhi ya chakula au mahitaji mengine kwa wafanyakazi wake.Japo ina uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa hadi miaka 25 lakin mahitaji ya chakula hufanya kukaa kwa hadi miezi mitatu tu kwa ajili ya kuongezea hifadhi ya chakula kwa wahusika. Pia ina uwezo wa kubeba wanajeshi maalum(special forces) kuwapeleka sehem husika na kutoka ndani ya nyambizi hiyo bila kulazimika kuja juu ya maji.
Japokua nyambizi hii inaendeshwa kwa nguvu za nyuklia lakini silaha zake hazihusiani kabisa na ubebaji au mashambulizi ya nyuklia(hazibebi makombora ya nyuklia) bali katika mashambulizi ya kawaida kama kuwinda na kuzilipua nyambizi nyingine. Silaha zake inajumuisha makombora ya kulipua meli,mashambulizi ya makombora ya cruise(Tomahawk), nk.
Nyambizi hii inayotarajiwa kuanza kazi mwakani bado taarifa zake nyingi zimefichwa(siri) ikiwemo ni umbali gani inaweza kuzama chini ya maji japo kwenye majaribio iliweza kwenda chini umbali zaidi ya mita 300(300m).