Hata ukae pambeni, kandokando, pembezoni popote utakapokaa siasa zinakuhusu utake usitake upende usipende ujihusishe usijihusishe. Ukisema ufanye umachinga wanasisa watakupangia pa kufanyia umachinga wako utaki virungu kama mbwa koko vitakuhusu mpaka utakapo fuata anavyotaka mwanasiasa, ukienda kwenye ufugaji atakuja huko na alama kwa mifugo hutaki virungu na faini juu.
Kwenye kilimo mwanasiasa anakuja fasta kukupangia namna ya kuuza tumbaku zako korosho, kahawa, ufuta, mahindi anavotaka yeye hutaki unakamatwa kwa utoroshaji mazao.
Kwenye uvuvi atakuja huko kukupangia namna ya kuvua, atafunga ziwa au bahari kwa kipindi fulani hutaki unakamatwa kichapo fine na kifungo juu unafanya uvuvi haramu sasa ndg yangu siasa utazikwepea wapi? Siasa ni maisha yetu kwa ujumla wake. Utake usitake labda ufe, Ukisema ujiue ukikutwa kabla hujafa ukaokolewa mwanasiasa alishatunga sheria ufungwe jela kwa kutaka kujiua wakati maisha ni yakwako wewe. Hapana chezea siasa ni zaidi ya ugali bwana.