Uingereza na Israel hawana katiba sisi mishipa ya shingo inatutoka

Mheshimiwa Waziri wa sheria ameongea mengi wakati akitoa hotuba ya majumuisho ambayo huwa ni majibu na maelezo kwa yale yote yanayokuwa yameulizwa au yanawatatiza wabunge.

Ameongea mengi lakini yaliyonigusa zaidi ni pale aliposema kuwa Israel na Uingereza hawana katiba zilizoandikwa ambazo wanazotumia kama rejea halisi ya uongozi wa mataifa yao.

Mheshimiwa Kabudi akaenda mbali zaidi na kuelezea kuwa Zanzibar kuanzia mwaka 1964 mpaka mwaka 1979 haikuwa na katiba yoyote ile ya maandishi.

Maisha ya kisiasa ya Israel na Uingereza yanakwenda kama kawaida, wao wanazo mila na desturi ambazo kwa umoja wao wamekubaliana ndizo ziwe mwongozo wa kisiasa na kijamii. Hapa Tanzania wajuaji wanajaribu kila kukicha kutuambia kwamba bila ya katiba mpya basi maisha ya taifa yanakuwa na matatizo!.

Gwiji wa sheria labda kasahau kuiongelea Rwanda ambayo tangu Kagame aingie madarakani imekuwa ikizidi kujijengea heshima kimataifa pasipo kuweka msisitizo kwenye masuala ya katiba mpya.

Profesa Kabudi akaieleza jamii yetu kwamba hata huo utungwaji wa katiba yetu uliofanywa kwa mara ya kwanza na Waingereza, ulifanyika katika mtazamo wa dharau ndani yake!. Kwamba tuwaandikie hawa jamaa taratibu za kiutawala kwani wao wenyewe hawawezi kujiandikia.

Maana yake ni kwamba kadri taifa linavyozidi kukua kiumri na kupata watu wenye uwezo wa kuhoji kwa kina juu ya maisha yao ya kila siku, ipo haja ya kuipitia kwa undani hata katiba hii ambayo imejaa chembechembe za ukoloni.

Pia profesa Kabudi kaongelea namna ambavyo mheshimiwa rais asivyofunga safari za nje za mara kwa mara, sawa sawa na maoni ya wananchi wakati wa upatikanaji wa rasimu ya katiba ya Warioba.

Lipo fundisho kubwa kupitia namna ambavyo mheshimiwa waziri wa sheria Prof Kabudi alivyoongea bungeni, nalo ni kwamba wanaharakati wetu wanayo tabia ya kufaidika na jamii pana kutokuwa na taarifa nyingi kuhusu masuala ya katiba. Labda hufanya hivyo kwa nia binafsi lakini watambue kwamba wanachokiongea sio sawa na maneno ya kwenye misahafu.

Israel na Uingereza hawajaweka mkazo kwenye katiba zilizoandikwa lakini maisha yanakwenda kama kawaida.

Haya ndo madhara ya ubashite

Back to school kijana
 
Upumbavu wa kijinga kabisa jirani yako akiwa na TV chogo wewe hutakiwi kununua flat sio?

Nnahisi kwa sababu wanajua wana watawala Watu wa aina gani Tanzania ,ndio sababu ya wao (Watawala)kuongea kama wana harish..
 
Mheshimiwa Waziri wa sheria ameongea mengi wakati akitoa hotuba ya majumuisho ambayo huwa ni majibu na maelezo kwa yale yote yanayokuwa yameulizwa au yanawatatiza wabunge.

Ameongea mengi lakini yaliyonigusa zaidi ni pale aliposema kuwa Israel na Uingereza hawana katiba zilizoandikwa ambazo wanazotumia kama rejea halisi ya uongozi wa mataifa yao.

Mheshimiwa Kabudi akaenda mbali zaidi na kuelezea kuwa Zanzibar kuanzia mwaka 1964 mpaka mwaka 1979 haikuwa na katiba yoyote ile ya maandishi.

Maisha ya kisiasa ya Israel na Uingereza yanakwenda kama kawaida, wao wanazo mila na desturi ambazo kwa umoja wao wamekubaliana ndizo ziwe mwongozo wa kisiasa na kijamii. Hapa Tanzania wajuaji wanajaribu kila kukicha kutuambia kwamba bila ya katiba mpya basi maisha ya taifa yanakuwa na matatizo!.

Gwiji wa sheria labda kasahau kuiongelea Rwanda ambayo tangu Kagame aingie madarakani imekuwa ikizidi kujijengea heshima kimataifa pasipo kuweka msisitizo kwenye masuala ya katiba mpya.

Profesa Kabudi akaieleza jamii yetu kwamba hata huo utungwaji wa katiba yetu uliofanywa kwa mara ya kwanza na Waingereza, ulifanyika katika mtazamo wa dharau ndani yake!. Kwamba tuwaandikie hawa jamaa taratibu za kiutawala kwani wao wenyewe hawawezi kujiandikia.

Maana yake ni kwamba kadri taifa linavyozidi kukua kiumri na kupata watu wenye uwezo wa kuhoji kwa kina juu ya maisha yao ya kila siku, ipo haja ya kuipitia kwa undani hata katiba hii ambayo imejaa chembechembe za ukoloni.

Pia profesa Kabudi kaongelea namna ambavyo mheshimiwa rais asivyofunga safari za nje za mara kwa mara, sawa sawa na maoni ya wananchi wakati wa upatikanaji wa rasimu ya katiba ya Warioba.

Lipo fundisho kubwa kupitia namna ambavyo mheshimiwa waziri wa sheria Prof Kabudi alivyoongea bungeni, nalo ni kwamba wanaharakati wetu wanayo tabia ya kufaidika na jamii pana kutokuwa na taarifa nyingi kuhusu masuala ya katiba. Labda hufanya hivyo kwa nia binafsi lakini watambue kwamba wanachokiongea sio sawa na maneno ya kwenye misahafu.

Israel na Uingereza hawajaweka mkazo kwenye katiba zilizoandikwa lakini maisha yanakwenda kama kawaida.
Kutokuziandika ina maana hawana? mhhh
halafu wao wana taratibu walizojiwekea ambazo wanaziheshimu je sisi tuna uadilifu huo?
maandishi tu tunashuhudia yakibadilishw kila uchao sembuse tusiandike!!!!!!
mimi sijamuelewa tunataka tuandike sababu hatuaminiani watatugeuka hawa
 
Nimeelewa kua UDSM ni makutano ya vilaza kweli
Yaani kumbe uncodified constitution sio katiba
Sasa Israel na Uingereza wanaendeshaje serikali yao? Kabudi aisee bad egg
 
Acheni ufala kile Chama sijuw kimerogwa na Nanii? Uki compare uchumi wa TZ na US vi green vinatoa povu oooo sio levo zetu Leo wenyewe ndo Wakwanza ku compare TZ na superpower kama UK yan ndo reference... Kile chamaa ni cha mizimu .
 
Siamini sana katika katiba,tunahitaji zaidi nidhamu binafsi,kuwajibika na kujithamini kwanza na mambo mengine mengi yatawezekana tu.Tunasheria nyingi mno na wala hatuzifuati.Tunalalamika kuliko kutenda,
Kaka umeandika pointi za maana sana. Ule ujinga wetu wote ulioachangia mpaka ATC ikafa, ulisababishwa na katiba mbovu?

Mashirika yote ya umma yaliyobinafsishwa enzi za Mkapa, chanzo chake ni vifungu vya katiba?.

Uzembe wa kushindwa kutumia rasilimali za kipekee kama wanyama na ardhi yenye rutuba na mvuto, chanzo chake ni katiba na vifungu vyake?.

Uvivu wetu na kutokubali kwetu kuwajibika, tunadhani sababu zake ni vifungu vya katiba. Poor we Tanzanians.
 
Huwezi fananisha nchi kama Israel na TZ mwishoni mwa mwaka jana Waziri mkuu aliitwa kuhojiwa na polisi kisa alipokea zawadi kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa nchini kwao Waziri mkuu wa UK alijiuzulu kisa alishindwa kwenye kura za maoni BREXIT.Tanzania tunaweza kufanya hayo??
 
Tunayapokea sana. Lakini Professor mzima unatuambia kuwa Uingereza haina Katiba, tutakukatalia, tena sana. Tumesoma haya mambo tena kwa sana tu. hata wewe soma tu utayajua. Ukiwa na nia utayajua. Equation kama hii inaweza kukupa taabu kidogo maana it is too abstract to comprehend!
View attachment 501534

Lakini hii ukiwa na nia utaelewa:

Britain’s unwritten constitution

Unlike most modern states, Britain does not have a codified constitution but an unwritten one formed of Acts of Parliament, court judgments and conventions. Professor Robert Blackburn explains this system, including Magna Carta’s place within it, and asks whether the UK should now have a written constitution.

For most people, especially abroad, the United Kingdom does not have a constitution at all in the sense most commonly used around the world — a document of fundamental importance setting out the structure of government and its relationship with its citizens. All modern states, saving only the UK, New Zealand and Israel, have adopted a documentary constitution of this kind, the first and most complete model being that of the United States of America in 1788. However, in Britain we certainly say that we have a constitution, but it is one that exists in an abstract sense, comprising a host of diverse laws, practices and conventions that have evolved over a long period of time. The key landmark is the Bill of Rights (1689), which established the supremacy of Parliament over the Crown following the forcible replacement of King James II (r.1685–88) by William III (r.1689–1702) and Mary (r.1689–94) in the Glorious Revolution (1688).

From a comparative perspective, we have what is known as an ‘unwritten constitution’, although some prefer to describe it as ‘uncodified’ on the basis that many of our laws of a constitutional nature are in fact written down in Acts of Parliament or law reports of court judgments. This aspect of the British constitution, its unwritten nature, is its most distinguishing characteristic.

Should the UK have a written constitution?
The question then arises in this 800th anniversary year — should the UK now take steps to codify all its laws, rules and conventions governing the government of the country into one comprehensive document, ‘a new Magna Carta’? The case for a written UK constitution has been debated at our universities and by politicians of all parties for several decades and has been the subject of a House of Commons committee inquiry during the 2010–15 Parliament. If a written constitution for the future is to be prepared, it must be one that engages and involves everyone, especially young people, and not simply legal experts and parliamentarians. Some of the mystique and charm of our ancient constitution might be lost in the process, but a written constitution could bring government and the governed closer together, above all by making the rules by which our political democracy operates more accessible and intelligible to all.
ukisoma vizuri hilo bandiko mkuu utagundua mtoa mada ndio kaamua kulipotosha

hakuna mahali kabudi kasema Uingereza haina katiba ila kasema haina iliyoandikwa japo nahisi ana agenda sawa na aliyonayo mpotoshaji wetu yaani kutuaminisha kuwa kuandika katiba si kitu cha muhimu saana!!!!!!! kaulaghai fulani hivi ka wasomi wetu wabinafsi.
 
Hatutukani ila tunatoa majibu kadiri mnavyokuja mkija kijinga mnajibiwa kijinga au unasemaje dogo?
Unasema hutukani halafu hapo hapo unasema unakuja kijinga jinga, halafu unawaita usiwajua dogo!!.

Ukijiona au ukidhani unazo akili nyingi kumbuka kuna watu wanakuona mwendawazimu tu kama wale wanaookota makopo njiani. Hayo matusi unayotukana wewe wengine tunayafahamu kabla hata baba yako hajaanza kumkonyeza mama yako. Miaka mingi sana iliyopita, ongea kistaarabu hakuna shahada za matusi zinazotolewa na chuo chochote kile duniani.
 
ukisoma vizuri hilo bandiko mkuu utagundua mtoa mada ndio kaamua kulipotosha

hakuna mahali kabudi kasema Uingereza haina katiba ila kasema haina iliyoandikwa japo nahisi ana agenda sawa na aliyonayo mpotoshaji wetu yaani kutuaminisha kuwa kuandika katiba si kitu cha muhimu saana!!!!!!! kaulaghai fulani hivi ka wasomi wetu wabinafsi.
Mkuu Sinonim pengine hujanielewa. Prof Kabudi alikuwa anajaribu kuelezea kama ni muhimu au sio muhimu kwa mchakato wa katiba kuendelezwa kwa sasa. Ndio maana akasema zipo nchi kama Uingereza ambazo zinatumia mila na desturi zao za miaka mingi na maisha yao yanakwenda kama kawaida tu.

Prof Kabudi akaongelea aina fulani ya dharau kwa namna ambavyo hata hizo taratibu zetu za kiutawala zilivyoandikiwa kwenye chapel fulani huko Uingereza badala ya kuandikiwa Birmingham.

Wengi wanaochangia uzi huu kwa njia moja au nyingine wanajaribu kupotosha kile ambacho Profesa alikiongea pale bungeni kwa faida zao wenyewe.
 
Huwezi fananisha nchi kama Israel na TZ mwishoni mwa mwaka jana Waziri mkuu aliitwa kuhojiwa na polisi kisa alipokea zawadi kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa nchini kwao Waziri mkuu wa UK alijiuzulu kisa alishindwa kwenye kura za maoni BREXIT.Tanzania tunaweza kufanya hayo??
Kwahiyo katiba itatuwezesha kufanya hivyo?
 
Mkuu Sinonim pengine hujanielewa. Prof Kabudi alikuwa anajaribu kuelezea kama ni muhimu au sio muhimu kwa mchakato wa katiba kuendelezwa kwa sasa. Ndio maana akasema zipo nchi kama Uingereza ambazo zinatumia mila na desturi zao za miaka mingi na maisha yao yanakwenda kama kawaida tu.

Prof Kabudi akaongelea aina fulani ya dharau kwa namna ambavyo hata hizo taratibu zetu za kiutawala zilivyoandikiwa kwenye chapel fulani huko Uingereza badala ya kuandikiwa Birmingham.

Wengi wanaochangia uzi huu kwa njia moja au nyingine wanajaribu kupotosha kile ambacho Profesa alikiongea pale bungeni kwa faida zao wenyewe.
ok ila mkuu unafikiri kuna sababu yeyote ya kumfanya kabudi asione umuhimu wa kuendeleza mchakato kwa sasa?
au je hiyo sababu aliyoitoa yeye ya kwamba hata Uingereza haina kwa hyo n sisi hatuna haja ya kuwa nayo kwelli unadhani inatosha!!!!
haya kipaumbele chetu sasa kiwe nin km sio katiba ambayo tumeshatumia pesa kuianza?
lakini pia kwa nini anashindwa kuona sababu za watu kudai katiba iliyoandikwa?
haon ni sababu ya viongozi wetu kutodhamin makubaliano yetu km jamii tuliyojiwekea?
 
Mkuu Sinonim pengine hujanielewa. Prof Kabudi alikuwa anajaribu kuelezea kama ni muhimu au sio muhimu kwa mchakato wa katiba kuendelezwa kwa sasa. Ndio maana akasema zipo nchi kama Uingereza ambazo zinatumia mila na desturi zao za miaka mingi na maisha yao yanakwenda kama kawaida tu.

Prof Kabudi akaongelea aina fulani ya dharau kwa namna ambavyo hata hizo taratibu zetu za kiutawala zilivyoandikiwa kwenye chapel fulani huko Uingereza badala ya kuandikiwa Birmingham.

Wengi wanaochangia uzi huu kwa njia moja au nyingine wanajaribu kupotosha kile ambacho Profesa alikiongea pale bungeni kwa faida zao wenyewe.

..maneno ya Prof yanashangaza kidogo.

..haiyumkiniki tuwe na waziri wa katiba halafu adai uandishi wa katiba au maboresho ya katiba si jambo muhimu.

..angekuwa ni Prof wa uhandisi au utabibu ningeweza kumuelewa au hata kumvumilia, lakini huyu ni Prof wa sheria.

..Pia kusema kwamba Waingereza walituachia nyaraka mfano wa Katiba ambayo iliandikwa ktk chapel/kanisa huko Uingereza hakuna tija kwetu. Cha msingi ni kuangalia maudhui/ contents za nyaraka hiyo.

..Kuna mikutano ya tume ya maoni ya katiba ilifanyika nje chini ya miti. Je ni halali kukejeli maoni yaliyopatikana ktk mikutano hiyo?

..Jambo lingine ni Prof kukemea wanasiasa wanaoutaja vibaya mhimili wa mahakama.

..Hivi Prof haoni kwamba mhimili huo kukubali kutumika kisiasa ndiyo kumesababisha ushambuliwe na wanasiasa wa upinzani? Na wanaounajisi (maneno ya Jaji Luanda)mhimili wa mahakama ni
watumishi wa wizara sheria anayoiongoza Prof.Kabudi.

..kuna mazonge-zonge mengi ktk wizara ya sheria, Prof alitakiwa ashughulike nayo, badala ya kufungua darasa la sheria bungeni.
 
Wana UNWRITTEN constitution, haimaanishi kuwa hawana a body of rules that governs their state!
 
Back
Top Bottom