Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mheshimiwa Waziri wa sheria ameongea mengi wakati akitoa hotuba ya majumuisho ambayo huwa ni majibu na maelezo kwa yale yote yanayokuwa yameulizwa au yanawatatiza wabunge.
Ameongea mengi lakini yaliyonigusa zaidi ni pale aliposema kuwa Israel na Uingereza hawana katiba zilizoandikwa ambazo wanazotumia kama rejea halisi ya uongozi wa mataifa yao.
Mheshimiwa Kabudi akaenda mbali zaidi na kuelezea kuwa Zanzibar kuanzia mwaka 1964 mpaka mwaka 1979 haikuwa na katiba yoyote ile ya maandishi.
Maisha ya kisiasa ya Israel na Uingereza yanakwenda kama kawaida, wao wanazo mila na desturi ambazo kwa umoja wao wamekubaliana ndizo ziwe mwongozo wa kisiasa na kijamii. Hapa Tanzania wajuaji wanajaribu kila kukicha kutuambia kwamba bila ya katiba mpya basi maisha ya taifa yanakuwa na matatizo!.
Gwiji wa sheria labda kasahau kuiongelea Rwanda ambayo tangu Kagame aingie madarakani imekuwa ikizidi kujijengea heshima kimataifa pasipo kuweka msisitizo kwenye masuala ya katiba mpya.
Profesa Kabudi akaieleza jamii yetu kwamba hata huo utungwaji wa katiba yetu uliofanywa kwa mara ya kwanza na Waingereza, ulifanyika katika mtazamo wa dharau ndani yake!. Kwamba tuwaandikie hawa jamaa taratibu za kiutawala kwani wao wenyewe hawawezi kujiandikia.
Maana yake ni kwamba kadri taifa linavyozidi kukua kiumri na kupata watu wenye uwezo wa kuhoji kwa kina juu ya maisha yao ya kila siku, ipo haja ya kuipitia kwa undani hata katiba hii ambayo imejaa chembechembe za ukoloni.
Pia profesa Kabudi kaongelea namna ambavyo mheshimiwa rais asivyofunga safari za nje za mara kwa mara, sawa sawa na maoni ya wananchi wakati wa upatikanaji wa rasimu ya katiba ya Warioba.
Lipo fundisho kubwa kupitia namna ambavyo mheshimiwa waziri wa sheria Prof Kabudi alivyoongea bungeni, nalo ni kwamba wanaharakati wetu wanayo tabia ya kufaidika na jamii pana kutokuwa na taarifa nyingi kuhusu masuala ya katiba. Labda hufanya hivyo kwa nia binafsi lakini watambue kwamba wanachokiongea sio sawa na maneno ya kwenye misahafu.
Israel na Uingereza hawajaweka mkazo kwenye katiba zilizoandikwa lakini maisha yanakwenda kama kawaida.