Uingereza Kuzibania Viza Za Wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingereza Kuzibania Viza Za Wanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 11, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Serikali ya Uingereza imetangaza mpango wake wa kupunguza idadi ya wanafunzi wanaopewa viza za kusoma nchini humo.
  Serikali ya Uingereza imetangaza kuweka sheria na masharti magumu katika utolewaji wa viza za uanafunzi.

  Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Alan Johnson amesema kuwa masharti magumu yameongezwa katika maombi ya viza za uanafunzi kwa wanafunzi toka nchi zote duniani.

  Mojawapo ya masharti yaliyoongezwa katika uombaji wa viza za uanafunzi ni kwa mwanafunzi anayeomba viza kutakiwa awe anaongea kiingereza fasaha.

  Miongoni mwa sheria ziliongezwa ni kama vile kuwazuia wanafunzi wenye viza za muda mfupi kuwaleta Uingereza jamaa zao kama vitegemezi (dependant) wao.

  Sheria mpya zimewekwa kufuatia waziri mkuu wa Uingereza kutaka masharti ya utolewaji wa viza yaangaliwe upya kufuatia tukio la mwanafunzi wa Nigeria aliyemaliza masomo yake nchini Uingereza kujaribu kuilipua ndege ya Marekani bila mafanikio.

  Sababu kubwa ya kuwekwa kwa sheria hizi ni kupunguza idadi ya wanafunzi toka barani Afrika na Asia ambao hujishughulisha zaidi na kufanya kazi kuliko masomo yao.

  Awali mwaka mmoja uliopita Uingereza iliongeza ugumu katika utolewaji wa viza za wanafunzi kwa kuwataka wanafunzi watoe vithibitisho vya kuweza kujilipia ada yote ya masomo yao na pia kuwa na uwezo wa kifedha kukimu gharama za maisha yao nchini Uingereza.

  Wiki iliyopita, Uingereza ilisimamisha kwa muda kupokea maombi ya viza za wanafunzi kutoka maeneo ya kaskazini mwa India, Nepal na Bangladesh. Hatua hiyo ilitokana na idadi kubwa kuliko kawaida ya maombi ya viza za uanafunzi toka maeneo hayo.

  Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imesema kuwa kutokana na masharti mapya ya utolewaji wa viza za wanafunzi, idadi ya wanafunzi watakaopewa viza itapungua sana lakini hata hivyo wizara hiyo ilikataa kutoa tathmini zao.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,402
  Likes Received: 2,024
  Trophy Points: 280
  Zamieni mwende bila viza. Wabongo bwana, kwani lazima kwenda huko? Kama vyuo vikuu tunavyo hapa ukiona maandamano yamezidi mlimani nenda SAUT au Idodomya.

  Au ikishindikana rudi kijijini kalime mbigiri na kunywa ulanzi. Ninachosema ni hivi tukae kwetu hata kama ufisadi unatuzidia. Waswahili mmekasirika utadhani kunyimwa viza ya UK ndo wazazi wamekufukuza kwenu. Kama vipi nenda uarabuni. Kazi ipo!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,621
  Likes Received: 23,753
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wameongeza sharti hilo, dawa yake ni ndogo tuu, kufanya mtihani wa Kiingereza pale British Council.
   
 4. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,259
  Likes Received: 28,903
  Trophy Points: 280
  hizo ni siasa tu uchaguzi unakuja hakuna jipya hapo hasa nilipo weka red,hilo la kiingereza sio tatizo...hilo linawasumbua wanaotaka IRAQ,AFGHANSTAN huko sio TZ

  na kuhusu dependant sio watz wengi ambao ni wanafunzi wanaleta dependant,watz wanasoma kozi ndefu hivyo wataqualify kuleta ndugu iwapo watataka,watawabana watu wanaokuja kusoma english kozi sio watz

  na vithibitisho vya kuweza kujilipia tunatoa tangu zamani hamna jipya hapo siasa tu uchaguzi unakuja
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...