Uingereza kubadili muelekeo wa Marekani

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,369
8,072
Wanasiasa wa Marekani wanawajibu kuishawishi Uingereza kubakia EU.

Kufuatia Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya mijadala na kauli zinaendelea kutolewa kutathimini matokeo yake katika myanja tofauti ambapo Marekani imeleezea mtazamo mpya kidplomasia ndani ya Ulaya.

Balozi wa NATO wa zamani kutoka Marekani, Nicholas Burns, amesema kujitoa kwa Uingereza katika jumuiya ya Ulaya kunatarajiwa kubadili uelekeo wa Marekani na kuifanya Ujerumani kuwa kitovu kipya cha masuala ya kidplomasia ndani ya Ulaya.

Nafikiri Ujerumani imekuwa imekuwa ikiimarika ndani ya Ulaya kwa muda mrefu sasa.
Hivyo kama Uingereza ikijiondoa EU tutapata mshirika mpya, Ujerumani na haitakuwa kwamba na ubora wa ushirikiano kama wa Uingereza tu,bali tutakuwa tumepata mshirika makini zaidi ambaye ni Ujerumani.’’

Burns amesema Uingereza ilikuwa ikiiwakilisha Marekani ndani ya jumuiya ya Ulaya,hivyo
Wamarekani kuna wakati wana sahau kama Jumuiya ya Ulaya ni mdau wetu mkubwa kibiashara,mwekezaji wetu mkubwa, na Ulaya ni mkusanyiko wa asasi za kimarekani duniani na ndani ya NATO.

Hivyo Uingereza ni mwanachama muhimu ndani ya asasi hizo za Marekani.

Nafikiri wanasiasa wa Marekani wana wajibu wa kuishawishi Uingereza kusalia EU.
 
hawa US/UK hawaaminiki sana...cjui kuna nn kimejicha hapa kwe brexit....
 
Too late. Wawashawishi vipi kuendelea kubaki? Yaani waishawishi serikali ipuuze na kutupilia mbali maamuzi ya waingereza yaliyopatikana kwa njia ya kura?
Marekani ataendelea kumhitaji sana muingereza kuliko mjerumani, hasa yajapo masuala ya kijeshi.
 
Jamani napenda kuuliza watu wa UK baby.Je,Malkia ana kura ya vetto kwenye maamuzi ya wananchi?
 
Magamba yanameguka mdo mdo.
Ujerumani mtu kibao hazitaki EU sababu ya refugee crisis, wacha waendelee jidanganya. We're witnessing the genesis of a disintegration of the babylonians.
 
Magamba yanameguka mdo mdo.
Ujerumani mtu kibao hazitaki EU sababu ya refugee crisis, wacha waendelee jidanganya. We're witnessing the genesis of a disintegration of the babylonians.

germany ndo anafaidika zaidi kiuchumi na EU, kuhusu yeye kujitoa sahau labda yeye ndo akimbiwe
 
germany ndo anafaidika zaidi kiuchumi na EU, kuhusu yeye kujitoa sahau labda yeye ndo akimbiwe

Angel Merkel amekuza upinzani sababu ya hiyo issue jombaa, subiria uchaguzi wao. Na ndio maana UK anataka kutulia kwanza chaguzi za France na Germany zipite ndio wadiscuss kuhusu kujitoa.
 
Angel Merkel amekuza upinzani sababu ya hiyo issue jombaa, subiria uchaguzi wao. Na ndio maana UK anataka kutulia kwanza chaguzi za France na Germany zipite ndio wadiscuss kuhusu kujitoa.

kwenye suala la uchumi wa nchi wote wako pamoja, hiv trump pamoja na mbwembwe zote ushasikia anazungumzia kuitoa US nato?! jibu ni hapana na sababu ni US ndo mnufaikaji mkuu wa NATO. yaani ni kama EAC kwa kenya ama SADC kwa SA
 
Back
Top Bottom