Uimara wa Milango ya Mabasi ya Mwendokasi

Uimara wa Milango ya Mabasi ya Mwendokasi

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Posts
2,018
Reaction score
1,108
Kwa wanaoishi kule njia ya Kimara ndo watumiaji hashwa wa mabasi ya mwendo kasi.

Shida ya mabasi haya nikujaza sana watu hadi milango inashindwa kufunga maana mlangoni hakuna wakumwambia mtu mwingine asiingie bali kila mtu kufosi kuingia hata kama nafasi hakuna.

Ma driver wa mabasi haya wao ni kulazimisha tu milango ifunge kwa nguvu na kuwapa wasiwasi abiria ndani haswa wa mlangoni.

Lakini sio kwamba abiria wanapenda kujazana kama kuku bali ni shida ya mabasi kuchukua masaa mengi hadi saa moja kuona lingine.

Sasa nashauri kuwepo na wasimamizi katika vituo vya mwendokasi ili waangalie usalama na idadi ya abiria wanaoingia lasivyo siku milango ikiachia na kubwaga watu itakuwa majanga.
 
Mkuu acha kabisa kuzungumzia hiyo milango.

Kuna siku huo mlango ulinibana nikiwa nalazimisha kuingia kukiwa na nyomi ya kufa mtu.

Sintokaa nisahau hiyo siku.
 
Mwendokasi ni shida sana inabidi wahusika walifanyie kazi ni wazo zuri
 
Mkuu acha kabisa kuzungumzia hiyo milango.

Kuna siku huo mlango ulinibana nikiwa nalazimisha kuingia kukiwa na nyomi ya kufa mtu.

Sintokaa nisahau hiyo siku.
nimecheka jamani nisamehe ilikuaje? Ulibanwa wapi??
 
Kwani daladala zimefungiwa?? Mnaona mwendo kasi imejaa mnan'gan'gana tu kujijaza....yawakute ya kuwakuta
 
Mwendokasi ilitakiwa watu wakae level seat tu Kama wa ku simama abiria wasizidi 6 lkn kwa sababu ya urohoo wa kupata pesa ndomana wanajaza abiria mithili ya nyanya kwenye tenga!

Ova
 
nimecheka jamani nisamehe ilikuaje? Ulibanwa wapi??

Nilibanwa mkono nilihisi utakatika. Toka siku hiyo hata hayo mabasi yakiwa hayana mtu sitaki kupakia. Hayo mabasi nimeamua kuwaachia wanafunzi na watumishi wa umma sio mimi.
 
Nunua ka passo mkuu.

Mkuu kupakia mabasi ya umma haimaanishi huna lako la binafsi. Tunapakia mabasi ya umma kama hayo kutoka na aina ya shughuli tunazofanya. Wakati mwingine parking ni changamoto kulingana na mahali unapoenda. Mambo ya aina hii unapikia gari la umma bila kupenda.
 
Transport management ni taaluma ya mtu, lakini si ajabu wasimamizi wa mradi wamechaguliwa kwa mujibu wa makabila yao.

Kuna mabasi nengine kadhaa tulitangaziwa kwa mbwembwe kuwa yako bandarini ya kwamba yenyewe ni more superior kwa haya yaliyopo, hivi yalishaingia kazini?
 
Nilibanwa mkono nilihisi utakatika. Toka siku hiyo hata hayo mabasi yakiwa hayana mtu sitaki kupakia. Hayo mabasi nimeamua kuwaachia wanafunzi na watumishi wa umma sio mimi.
Pole Sana Ndugu yangu
.
Serikali ya wanyonge inasubiri hayo mabasi yamwage watu barabarani ndio IAMUKE na KUUNDA TUME

Viongoz wengi wa Umma ni shithole kabisa

Vitu vya kawaida kabisa sijui tunasubiri Hadi DG awe Mzungu ndio tufanye vyema
 
halafu madereva huwa wana sifa wanawahi kufunga milango hata kama kuna watu bado wanashuka.
 
Nilibanwa mkono nilihisi utakatika. Toka siku hiyo hata hayo mabasi yakiwa hayana mtu sitaki kupakia. Hayo mabasi nimeamua kuwaachia wanafunzi na watumishi wa umma sio mimi.
hahahaha pole sana
 
Mkuu kupakia mabasi ya umma haimaanishi huna lako la binafsi. Tunapakia mabasi ya umma kama hayo kutoka na aina ya shughuli tunazofanya. Wakati mwingine parking ni changamoto kulingana na mahali unapoenda. Mambo ya aina hii unapikia gari la umma bila kupenda.
Daah mimi hua nakomaa mwanzo mwisho mpk kieleweke lkn iwe isivyo nahakikisha sipandi gari za umma mkuu.
 
Back
Top Bottom