DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,212
- 4,517
Salaam wanajukwaa,
Nimechukua muda kutafakari ukaribu uliopo kati ya Zitto Zuberi Kabwe na Tundu Lissu kwa muda sasa, kwa bahati mbaya sana labda ni kutokana na uelewa wangu finyu wa kisiasa ndo maana natilia urafiki huu mashaka.
Binafsi nilimpenda Zitto enzi zileee za 2007 nakumbuka alipotimuliwa bungeni kuhusu mkataba wa Buzwagi nilikuwa kati ya walionyeshewa wakati wa mapokezi yake Jangwani ila baada ya pale jamaa alikubali kuwa kwenye tume iliyoundwa na JK ya madini. Yaliyofuata wengi tunajua.
Baada ya pale kimsingi sikuweza tena kumuamini Zitto kutokana na siasa zake ndani ya CHADEMA ambapo alilenga sana kujijenga yeye na kujiona bora kuliko wenzane na chama kwa ujumla jambo ambalo lilipelekea yeye kutimuliwa baada ya njama zake kugundulika.
Zitto ameendelea kunishawishi kwamba siyo mtu wa kuaminiwa na upinzani kila siku hususani kwenye uchaguzi wa 2015 aliposhirikiana na CCM.
Leo hii Zitto anajaribu kujenga mahusiano na Lissu eti ni urafiki wenye manufaa kwa upinzani?!
Mimi mpaka kesho simuamini Zitto na najua Lissu akikubali tu ulaghai wa Zitto ndo mwisho wake kisiasa. Nafsi yangu inanikataza kuamini kwamba Zitto ana nia njema na upinzani.
Wakati utaongea.