Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Rubani anawafikia abiria, badala ya kutuliza mvutano na kuweka mazingira ya wahusika kuzungumza kwa kusikilizana, anaamua kuungana na upande mmojawapo. Bila kujali upande alioungana nao uko sahihi kiasi gani; anajikuta amekuwa sehemu ya mvutano. Dakika kadhaa baadae, ndege inaanza kuyumba, anataka arudi kwenye chumba cha kuongozea ndege lakini kila akitaka kuondoka hawezi. Upande mmoja umemshika kulia mwingine kushoto na kila mmoja anavuta kwa nguvu zake zote. Fikiria ni nini kitaenda kutokea?'
Katika mfano wa hapo juu, haimaanishi kuwa hao wanaomvuta rubani hawana akili, au sio watu muhimu, au wamechoka maisha au wanavutiwa na kitakacho wapata, la! Inakuwa ni ‘confusion’ kuna mazingira mivutano ikiachwa ikifikia hatua fulani, wahusika wanaweza kushindwa kurudi kwenye hali ya kawaida hata kama wanatamani kurudi, wanashindwa kwa sababu ya ‘confusion’.
Viongozi wa dini angalau ndio watu wanaoweza kuwaunganisha wanasiasa wanaoshindwa kuelewana kwenye mambo kadhaa ya msingi ambayo maelewano ni muhimu. Viongozi wa dini wanaweza kuwaita na kuwaunganisha viongozi wa siasa ambao hawawezi kukutana wenyewe na kuzungumza kwa sababu mbalimbali.Hii ni kwa sababu katika eneo la imani, wao ndio wenye nguvu zaidi na wanaweza kusikilizwa.
Ni vyema yanapotokea mambo yenye utata viongozi wa dini wachukue nafasi ya upatanishi ‘Mediation’ ambapo moja ya nguzo kufanikiwa katika ‘mediation’, ni kuwa mtu wa kiasi na haki ili kuaminiwa na pande zote. Hatari ya kuchagua upande ni uwezekano wa kupoteza kuaminika na kushindwa kuziunganisha pande zinazohusika pale inapohitajika kufanya hivyo.
Vile vile tunawashauri viongozi wa kisiasa wasiwashawishi viongozi wa dini kuwa upande wao bali wawaache wawe ‘mediators’ pale inapobidi. Kwa jicho la haraka unaweza kudhani kwamba kuwashawishi kuwa upande wako ni jambo jema lakini ukweli ni kwamba ijapokuwa inaweza kukupa furaha ya muda lakini ni hatari kweli. Kuwashawishi kuwa upande wako ni sawa na kumshawishi rubani kwenye ndege awe upande wako wakati unavutana na abiria wenzako kwenye ndege (bila kujali uko sahihi au la!). Kama akikubali, janga litakalokuja kutokea hata wewe halitakucha.
Kama kuna atakayekereka na hoja hii basi anisamehe kwani sijalenga kumkwaaza. Nawashukuru sana kwa jinsi ambavyo mmeelewa.