Uhusiano wa CUF na CCM hauna tatizo - Lipumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhusiano wa CUF na CCM hauna tatizo - Lipumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema uhusiano baina ya chama chake na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuunda serikali moja ya kitaifa visiwani Zanzibar, haukifanyi chama hicho kuwa CCM B kama inavyodaiwa.
  Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo jana akipinga kile alichokiita madai ya viongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwamba wamekuwa wakiita CUF kuwa ni CCM B katika mikutano na maandamano yao waliyoyafanya katika mikoa mbalimbali nchini.
  Wananchi mbalimbali pia kupitia vipindi mbalimbali vya mijadala hususani vile vya televisheni, wamekuwa wakitoa maoni ya kuishutumu CUF kwa kushirikiana na CCM kujaribu kudhohofisha nguvu za CHADEMA bungeni huku wakionyeshwa kukerwa na kitendo cha wabunge wa chama hicho wakiongozwa na Mbunge wao wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kuliomba Bunge libadili kanuni ili kuidhohofisha CHADEMA.
  “Mimi nasikitika sana na kauli zao katika mikutano yao mingi na maandamano wamekuwa wakisema kuwa sisi CUF ni CCM B. Lakini wanasema hivyo kwa sababu tumeingia katika serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar…Wazanzibari wenyewe ndio waliamua hivyo na sasa wanaishi kwa amani kutokana na hilo”, alisema Profesa Lipumba.
  Aliongeza kuwa Katiba ya Zanzibar inaruhusu hata CHADEMA kushiriki katika serikali ya mseto endapo tu itashinda asilimia tano visiwani humo na ndiyo maana wao wameamua kushirikiana na CCM.
  Katika hatua nyingine, Lipumba alielezea kushangazwa kwake na safari za Rais Jakaya Kikwete kwamba amekuwa akisafiri kila kukicha na kushindwa kusimamia mambo ya ndani ya nchi.
  “Matokeo yake kila kukicha kunatokea madhara yakiwamo ya milipuko ya mabomu Gongo la Mboto, gharama za umeme na kupanda kwa gharama za maisha,” alisema Lipumba.
  Mwenyekiti huyo pia alitoa salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Japan kwa maafa makubwa yaliyowakumba na kuwaombea kwa Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hicho kigumu.
  Wimbi la wananchi kukimbilia kwa wingi ili kupata tiba kwa mchungaji Ambikile Mwasapile wilayani Loliondo ni kutokana na serikali kutokuwa na huduma bora za afya katika hospitali mbalimbali.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotokea hapa nchini, mwenyekiti huyo alisema kwamba kwa sasa taifa liko katika giza la machafuko na kwamba kuna mengi zaidi yanaweza kutokea, kwa kuwa wananchi wamechoka, wamekata tamaa na ubovu wa utendaji wa serikali kwa sasa. “Wananchi wamechoshwa na utendaji na ubovu wa serikali kwa sasa, huduma za afya za serikali ni mbovu, hivyo wananchi wameamua kukimbilia kwa mchungaji kwa wingi ili waweze kupata tiba kwa kuona kwamba hiyo ndiyo njia mbadala kwao,” alisema Lipumba. Aidha, mwenyekiti huyo aliendelea kubainisha kwamba kitendo cha wananchi kukimbilia ili kupata tiba Loliondo ni kutokana na viongozi wa serikali kutokuwa waadilifu, jambo linalosababisha serikali kutowajali wahudumu wa afya na kusababisha migomo kila kukicha kwa kuwa viongozi wengi wanakimbilia kupata tiba nje ya nchi ikiwamo Afrika Kusini na India, jambo ambalo raia wa kawaida anashindwa kumudu gharama za tiba hizo.
   
 2. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  ZANZIBERI CUF CHAMA TAWALA,TANGANYIKA ETI NI CHA UPINZANI. CDM TUNYOMWIKE (TUMESHAWASHITUKIA CUF). HATA SIKU MOJA HATUWEZI KUWA KAMBI MOJA. NEVER.:embarassed2:
   
 3. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mfa maji huyo...
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Mwenye busara angeliona hilo (BOLD) na yule anaetaka vyenginevyo basi anafaa apimwe akili (unless ametumwa na mtumwa ni mtumwa hajiwezi mbele ya Bwana wake)
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Haya ni matakwa yenu mlipolazimisha kuwa Wazanzibari wasiwe huru kuunda vyama vyao vya siasa.
   
 6. k

  kany Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 20, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hata waeleze kwa maneno gani! Kueleweka ni vigumu mno. Wanajamii mnasahau jinsi mheshimiwa (Lipumba) alivyokuwa na furaha siku ya kutangazwa matokeo utadhani alishinda yeye hadi akaamua kumkabidhi mkulu ilani ya chama chake!!!!!
   
Loading...