Singidan
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 881
- 941
Wapo vijana wengi sana wenye mawazo bunifu mikoani ambao kwa namna moja au nyingine wakiwezeshwa mawazo yao, naamini Tanzania itaweza kutatua changamoto mbalimbali. Tatitzo la taasisi hii ya sayansi na teknolojia (COSTECH) Wamekuwa wakiishia Dar tu, Wamekuwa wakiami Dar tu ndiyo kuna vijana wabunifu, sikuwahi kuona program zozote ambazo zinakuza mawazo ya vijana ya kiteknolojia mtaani. Wamekuwa wakiishia tu pale Buni Hub. Sasa ni vipi wasiofahamu au wasioweza kufika huko Dar? Inaniuma sana kuona serikali ikishindwa kuandaa sera na mfumo ambao utahusika na KUKUZA NA KUENDELEZA VIJANA WABUNIFU NA MAWAZO YAO.