Uhusiano kati ya siku ya Ijumaa na ombaomba ni upi?

Enzymes

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
4,332
3,008
Wadau naomba kujuzwa!

Tangia utotoni hadi leo hii nipo mtu mzima. Kila aombae msaada utasikia watu wanamtania "subiria Ijumaa". Na kweli ifikapo siku ya Ijumaa utakuta Ombaomba wengi sana wamejazana mijini nchi nzima, si Dar pekee!

Wengi wao ni vigumu kuwatambua kwa imani zao. Japo wapo wengine waweza kuwatambua kutokana na mavazi yao. Pia kuna changamoto ya wengine kuigiza mavazi ili tu kuvizia misaada toka kundi la imani flani!! Huenda ndilo linasadikika hutoa saaana misaada.

Hivi karibuni RC Makonda ameagiza kuwaondoa na kutowatambua ombaomba hapa Tz hasa ktk Jiji la Dar es Salaam.
Swali: Je hii siku ya Ijumaa inatambuliwa serikali kama siku ya watu kupita na kuomba misaada madukani?

Au kuna uhusiano gani kati ya siku ya Ijumaa na ombaomba Tz? Ni siku rasmi ya Serikali kwa Ombaomba?
 
Japo mimi ni mkristo, lakini kwa hili la wewe kujaribu kupotosha kwa kufananisha siku ya ijumaa (Jumaa Karim) na ombaomba....
Anyway.....
Ipo namna hii....
Siku ya ijumaa ni siku ya wenzetu wanao amini kwenye dini ya Islamic, huitumia siku hii kwao kama siku ya kuabudu. Wenzetu hawa huitumia siku hii kwaajili ya kuenda kwenye nyumba za ibada na kumuabudu muumba awa mbingu na nchi (Allah).
Na hapo huitumia siku hii kuwasaidia waiso jiweza (sio ombaomba) kwa kuwapa misaada kama sehem ya kutoa sadaka kwa kuwasaidia masikini ili Mungu (Allah) awazidishie na kuaongezea mibaraka.
Hapa nawasifu kiukweli kuliko sisi wakristo kutoa sadaka na kisha kutumwa kule Vatican kisha kurudishwa kiasi kidogo kama eti kile wanacho kiita misaada ya kutoka Roman.
Nawale wakrito wenzangu wa madhehebu tofauti na mimi hutoa sadaka na kisha wachungaji kujineemesha na kujinunulia magari ya kifahari wakati waumini wao uhangaika hata kwa kupata milo ya kutwa kwa uhakika.
 
Ahsante mkuu, Ombi langu ni swali la mwisho tu.
 
Back
Top Bottom