Uhusiano kati ya Korea Kusini na Kaskazini: Nini chanzo cha Uhasama uliopo kati ya Mataifa haya

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
583
1,478
Korea Kaskazini iliilipua ofisi yake yenye mahusiano na Korea Kusini huko Kaesong.

Tukio hilo lilitangulizwa na tahadhari ya siku kadhaa na saa chache baada ya kutoa vitisho vingine kuhusu hatua ambazo majeshi yake yanaweza kufanya katika eneo la mpaka , jambo ambalo linaweza kushtua dunia nzima.

Ofisi hiyo ilikuwa muhimu sana na ilikuwa ishara inayowakilisha maridhiano ambayo nchi hizo mbili zilikubaliana mwaka 2018 mbali na kwamba ilitumika kama chombo cha mawasiliano cha mataifa hayo wakati wa vita.

Wakati ambao waliiharibu ofisi hiyo kulikuwa hakuna watu kwa sababu ya mlipuko wa corona.

Awali Korea Kusini ilikata mawasiliano yao yote na Korea Kusini.

Mbinu ambayo ilitumika katika miaka miwili iliyopita iliweza kuweka historia ya mkutano kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un mwaka 2019.

Mkutano huo ulileta matumaini kuwa Korea kaskazini itaondoa mpango wake wa kinyuklia na kuleta mabadiliko ya kuondolewa kwa vikwazo lakini hakuna kilichotokea au kufanyika na baada ya hapo mkutano uliofuata ulitangazwa zaidi.

Picha iliposambazwa na jeshi la Korea Kusini kuhusu kulipuliwa kwa ofisi ya kaesong


Miezi ya hivi karibuni , kumekuwa na uvumi kuhusu hali ya uchumi na afya kutokana na virusi vya corona, licha ya kwamba Korea Kaskazini ilithibitisha kuwa hakuna maambukizi ya corona.

Uvumi huo ulitokea pia kuwa hali ya afya ya kiongozi wa Korea Kaskazini si nzuri baada ya kutoonekana hadharani kwa wiki kadhaa na ikadhaniwa kuwa dada yake, Kim Yo-jong ,angechukua nafasi yake.

Lakini kwa nini Korea Kaskazini imeamua kuchukua hatua ya sasa na hii ina maana gani?

ramani ya eneo la kaseong


Propaganda
Katika taarifa iliyotangaza mlipuko mkubwa , maafisa wa Korea Kaskazini,chombo cha habari cha KCNA kilihusisha tukio hilo na watu wanaopinga propaganda za Korea Kaskazini upande mwengine wa mpakani na wanajeshi.

wanaharakati wakiandaa vobofi vya ujumbe wa Korea Kaskazini 2012

wanaharakati wakiandaa vobofi vya ujumbe wa Korea Kaskazini 2012

Muandishi wa BBC huko Korea Kusini bi. Laura Bicker anakumbuka kuwa Korea Kusini iliahidi kukabiliana na uzinduzi wa propaganda ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in pamoja na Kim Jong-un.

Ingawa Seoul ilikuwa inajaribu kuwakamata wanaharakati, kwa kudai kuwa shughuli zao zinahatarisha wakazi wa maeneo ya mpakani, propagamda hizo zimeendelea kuingizwa nchini Korea kaskazini kupitia mpaka huo..

Hata hivyo hil limeonekana kutumika kama sababu tu ," alisema Bicker.

Mtaalamu wa utungaji sera nchini Korea alikubaliana na suala hilo.

"Korea Kaskazini inahisi kuwa Trump amewasaliti, " alisema Van Jackson, mwandishi wa kitabu cha On the Brink: Trump, Kim, na tishio la vita ya Nuklia.

Korea Kaskazini inahisi imesalitiwa na Trump ka kuwa haikupata kitu baada ya mkutano wao

Korea Kaskazini inahisi imesalitiwa na Trump kwa kuwa haikupata kitu baada ya mkutano wao Wataalamu waliainisha sababu tatu ambazo zilisababisha kile ambacho kilitokea:

 Moja ni hisia za kusalitiwa kwa Korea Kaskazini kufuatia mkutano na Trump ambao ulishindwa kuzaa matunda: "Kim alienda kwenye mikutano hiyo akiwa anatarajia kupata unafuu katika upande wa vikwazo vya kiuchumi lakini hajapata chochote.

 Sababu ya pili, uchumi wa Korea Kaskazini uko kwenye msukumo mkubwa kutoka kutokauwa kwa biashara ya kutosha na China kutokana na mlipuko wa virusi vya corona na msukumo wa Marekani kupitia vikwazo mahitaji ya kuongezeka kwa vigezo katika hatua hiyo.

 Na sababu ya tatu, ni majukumu ya dada yake Kim Jong-un ambaye anakzaia kutengeneza njia ya kuchukua madaraka yeye mwenyewe: "Anahitaji kuonyesha kuwa ana nguvu na uwezo mkubwa wa kutawala mbele ya viongozi na wanajeshi wa zamani wa Korea Kaskazini.

Kwanza vitisho vya hivi karibuni vilitolewa na dada yake mdogo Kim Yo-jong, ambaye amekuwa maarufu sana tangu kuchaguliwa katika ngazi za juu za chama cha wafanyakazi cha Wakorea.

"Ukweli ni kwamba dada yake Kim Jong-un amekuwa mstari wa mbele kuongeza mvutano, na kudai kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kumpa sifa dhidi ya maadui wa nchi hiyo', alisisitiza Profesa Andray Abrahamian , kutoka chuo kikuu cha George Mason huko Korea Kusini.

Abrahamian alitoa angalizo kuwa maamuzi ya Korea kaskazini yanahusisha siasa za ndani licha ya kwamba anaamini kuwa hawezi kuwa na uhakika wa kile ambacho kinaendelea.

Profesa anakumbuka kuwa majukumu makubwa ya Kim Yo-jong tangu mwanzo ni kukutanisha nchi mbili zielewane.

Kim Yo-jong alijipatia jukumu muhimu katika kujenga uhusiano na Seoul akiwa pamoja na rais Moon jae-in


"Uongozi sasa unaonyesha watu kuwa ni mtu ambaye hawezi kuchezewa na mataifa ya kigeni .

"Kama ni kweli kuwa Korea Kaskazini imeachana na mpango wa kuharibu uongozi wa Korea Kusini pamoja na Marekani katika kutekeleza miradi ya Korea basi hawana kikubwa cha kupoteza."

Bodi ya kikanda
Kama mwandishi wa BBC mjini Seoul anavyokumbuka Pyongyang pia imekasirika kuwa Seoul haipambani na Marekani na kusisitiza kubaki na kuimarisha uchumi na kuingia katika miradi ya pamoja ya Marekani na Umoja wa mataifa .

Kim jong un na Moon jae-in
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionKim jong un na Moon jae-in
Ikikabiliana na vitisho vya mwisho na mlipuko wa ofisi ya mawasiliano , Korea Kusini imeandika taarifa kwa kujiamini kuwa kama Korea Kaskazini itaendeleza hali hiyo basi hali haitakuwa nzuri.

Uharibifu wa ofisi umeondoa matumaini ya mataifa hayo kuwa na mahusiano yoyote ya Amani.
 
siasa bwana__ hapo wamepiga picha wana tabasamu kabisa. .kumbe mioyo yao imejaa,chuki dhidi ya wao wenyewe

kim ana mvizia moon

moon nae ana mvizia kim

urafiki wa mashaka kati ya simba na swala
ama kati ya binaadamu na mbuzi
 
siasa bwana__ hapo wamepiga picha wana tabasamu kabisa. .kumbe mioyo yao imejaa,chuki dhidi ya wao wenyewe

kim ana mvizia moon

moon nae ana mvizia kim

urafiki wa mashaka kati ya simba na swala
ama kati ya binaadamu na mbuzi
Na ndio mambo yanaenda sasa.. usikute wanatuektia tu hawa wanalipua ofisi isiyokuwa hata namlinzi..😅
 
Back
Top Bottom