Uhusiano kati ya katiba mpya na maendeleo ya taifa letu.

king Chuga

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
510
52
Ndugu zangu, wanajamii wenzangu, naomba kujua ni vipi katiba mpya inaweza kuchangia upatikanaji wa huduma bora kama za afya, elimu , barabara na mambo yanayofanana na haya.
Kwa upeo wangu naona katiba mpya inalenga zaidi mgawanyo wa madaraka, mfumo wa siasa nk.
 
umri wako tafadhali mkuu, nyie ndio mnaturudisha nyuma kama hadi hapo ulipo hujui mahusiano ya katiba na maendeleo!
 
Kupitia katiba mpya
Madaraka yatapunguzwa ili aliye jumba jeupe asiamue kwenda jenga kwao airport, benki

Itasaidia barabara kujengwa hata wasipoungwa mkono
 
umri wako tafadhali mkuu, nyie ndio mnaturudisha nyuma kama hadi hapo ulipo hujui mahusiano ya katiba na maendeleo!
Mjibu swali umri wake unahusiana vip na hoja yake?
Mnapopandikiza dhiki zenu za kisiasa na madaraka muwe pia wakweli kwa nafsi zenu.
 
Mjibu swali umri wake unahusiana vip na hoja yake?
Mnapopandikiza dhiki zenu za kisiasa na madaraka muwe pia wakweli kwa nafsi zenu.

Ona sasa unavyokuja na chuki zako kwenye mambo ya msingi, nina sababu ya msingi kumuuliza umri!

Anavyoelekezwa mtoto wa chekechea ni tofauti na mwanafunzi wa chuo, japokuwa wote wanafundishwa ila kuna mbinu za ziada.
 
Ndugu zangu, wanajamii wenzangu, naomba kujua ni vipi katiba mpya inaweza kuchangia upatikanaji wa huduma bora kama za afya, elimu , barabara na mambo yanayofanana na haya.
Kwa upeo wangu naona katiba mpya inalenga zaidi mgawanyo wa madaraka, mfumo wa siasa nk.
Katiba licha ya mgawanyo wa madaraka, inaleta Amani ya kweli, kwamba kila mtu anaridhika na jinsi nchi na masuala yake yanavyoendeshwa, kwa haki na uwajibikaji, hapo nguvu itawekwa katika shughuli za maendeleo na ustawi wa jamii, ikiwa imehakikishwa kuwa kitakachopatikana kutokana na maendeleo (kodi), nacho kinatumiwa kwa nidhamu na haki kwa wote.
 
Back
Top Bottom