Uhuru wa Zanzibar tarehe 10 desemba 1963

Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,173
Points
2,000

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,173 2,000
Naikumbuka siku hii kama jana vile.

Nilikuwa na umri wa miaka 11 na vitu viwili vitatu ndivyo vilivyonasa kwenye kichwa changu.

Kwanza ni kumuona Mzee Abdulrahman akitoka nyumbani kwake kashika sanduku anaingia kwenye taxi anawaaga majirani kuwa anakwenda uwanja wa ndege safari Zanzibar kwenye sherehe za uhuru.

Mimi na mwanae somo yangu Mohamed Kitunguu tuko barazani kwake na rafiki zetu wengine tunacheza.

Ilikuwa mchana Mtaa wa Gogo moja ya mitaa mifupi sana Kariakoo.

Kitu cha pili kinachonikumbusha siku hii ni nyimbo ya Sal Davis, "Ayayaa Uhuru," ambayo kutwa nzima ilikuwa ikipigwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC)ikihanikiza sherehe za uhuru wa Zanzibar na Kenya.

Kwetu sisi watoto tunanyanyukia kuingia "teens,"muziki wa Sal Davis ulikuwa ukitutia wazimu.

Tunamsikia Sal Davis akiimba na radio katika kila nyumba mitaa ya Dar es Salaam zimefunguliwa, "full blast," "Ayaayaa uhuru, ayaayaa Kenyatta, Nyerere, Obote, Shamte..."

Sikumbuki vyema maneno ya nyimbo hii mpangilio wake lakini majina ya viongozi wa Afrika Mashariki yanatajwa na kwa Zanzibar jina la Waziri Mkuu Mohamed Shamte linasikika.

Sauti ya Unguja nayo ilikuwa imefungulia vinanda vya taarab ilmuradi mji ulikuwa furahani.

Katika umri wangu ule mdogo wa miaka 11 sikuweza kutambua kuwa ukubwani Sal Davis atajakuwa rafiki yangu mpenzi na nitakuwa jirani yake milango ya "appartments"zetu zikiangaliana mimi nikiwa mpangaji wake na wake zetu watakuwa mashoga.

Si haya tu nitamkalisha Sal Davis kitako na tutaandika mswada wa maisha yake na mengi tutafanya pamoja nyumbani kwake kwengine Zanzibar na Mombasa Nyali Beach.

Turudi kwenye uhuru wa Zanzibar na nyimbo ya Ayaayaa Uhuru na Waziri
Mkuu wa kwanza wa Zanzibar Mohamed Shamte.

Sal Davis amenieleza kuwa wakati nyimbo yake hii iko juu kabisa kwa kupendwa kote Afrika ya Mashariki, mapinduzi yakatokea Zanzibar na serikali ya Mohamed Shamte ikapinduliwa.

Nyimbo yake kwa kuwa ilikuwa imemtaja Waziri Mkuu wa Zanzibar Mohamed Shamte ikapigwa marufuku Tanganyika na Zanzibar.

Kipindi hiki mauaji makubwa yalikuwa yamepita Zanzibar na baadhi ya viongozi wa iliyokuwa serikali ya Zanzibar wakawa vifungoni.

Baadhi ya viongozi hawa waliofungwa na kutumikia vifungo vyao katika jela za Tanzania Bara nilikuja kufahamiananao kwa karibu sana ukubwani kwangu na nilijifunza mengi kutoka kwao.

Ilikuwa katika Mtaa huu wa Gogo unapokutana na Mtaa wa Mchikichi kwenye baraza ya nyumba ya akina Abdul Kigunya kulipokuwa na barza maarufu ya kucheza bao ndipo kwa mara ya kwanza nilipomuona Abdallah Kassim Hanga.

Hii ilikuwa mwaka wa 1964 na muungano wa Tanganyika na Zanzibar tayari.

Hanga akija hapo kila jioni tena akitembea kwa miguu akija kucheza bao.

Sifa zake kama mmoja wa viongozi wa mapinduzi zilikuwa zimeenea na picha zake katika gazeti la Ngurumo na Mwafrika zilikuwa hazipungui.

Nasi kwa ule udadisi wa kitoto tukimuona pale tutajisogeza kwenda kumshangalia hadi tujazane na wakubwa watuone kero watufukuze.

Haikunipitikia kamwe kama siku itafika nitatafiti historia ya mzalendo huyu pamoja na historia ya "pop star,"mkubwa kupata kutokea Afrika ya Mashariki Sal Davis na nitaandika historia zao.

Inasikitisha tu kuwa katika uhuru wa Zanzibar na mapinduzi yaliyofuatia Hanga aliuawa kikatili na katika utafiti nilikujakujua mengi yaliyopitika.

Si yeye tu.

Marafiki wawili wa baba yangu Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala na wao hawakusalimika.

Nimeishi katika historia hii na ndani yake nimejifunza mengi.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
12,028
Points
2,000

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
12,028 2,000
Mkuu Mohammed naomba kujua, kwa maoni yako, mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa halali? kwa kuangalizia uhalali wa serikali ya Shamte.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,845
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,845 2,000
Red...
Maoni yangu mimi yana umuhimu gani?
Kwa nini uwaulizi swali hili Wazanzibari wenyewe?
Kwanza kabisa asante sana kwa maelezo mafupi juu ya uhuru wa Zanzibar kisha na mambo mengine yaliyofuata ambayo unayajua kwa undani kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu.
Pili natoa maoni yangu binafsi juu ya namna ulivyoshuhulikia swali la Red Giant. Binafsi naandika kuwa , Mkuu, umemuonea Red...! Red, kauliza swali la msingi sana... na msingi wa swali lake umetokana na namna ulivyotoa madokezo mbali mabali juu ya kikichotokea kabla na baada yauhuru wa Zanzibar na mapinduzi ya waziri Mkuu Shamte! Ni kwa madokezo yako Red... amepata hoja ya kuuliza swali lake.
Naungana naye(Red..) kuomba maoni yako juu kujua uhalali ama uharamu wa kupinduliwa Shamte.

Karibu, Mkuu.
 
Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,173
Points
2,000

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,173 2,000
Mohamed Said, natamani sana kusikia habari za Abdala Kasim Hanga, ni nini hasa kilichompata? nimekumbuka Nyerere alivyomzodoa pale mnazi mmoja kwenye mkutano? tafadhal tueleze kisa chake
Laki...

Ingia hapo:
 
Mohamed Said

Verified Member
Joined
Nov 2, 2008
Messages
13,173
Points
2,000

Mohamed Said

Verified Member
Joined Nov 2, 2008
13,173 2,000
Kwanza kabisa asante sana kwa maelezo mafupi juu ya uhuru wa Zanzibar kisha na mambo mengine yaliyofuata ambayo unayajua kwa undani kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu.
Pili natoa maoni yangu binafsi juu ya namna ulivyoshuhulikia swali la Red Giant. Binafsi naandika kuwa , Mkuu, umemuonea Red...! Red, kauliza swali la msingi sana... na msingi wa swali lake umetokana na namna ulivyotoa madokezo mbali mabali juu ya kikichotokea kabla na baada yauhuru wa Zanzibar na mapinduzi ya waziri Mkuu Shamte! Ni kwa madokezo yako Red... amepata hoja ya kuuliza swali lake.
Naungana naye(Red..) kuomba maoni yako juu kujua uhalali ama uharamu wa kupinduliwa Shamte.

Karibu, Mkuu.
Tujitegemee,
Maoni yangu mie yana umuhimu gani wakati wenye nchi yao wapo?

Kwa nini mimi nimwasemee?
Mie nani?
 
dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Messages
2,809
Points
2,000

dos.2020

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2009
2,809 2,000
CCM wanawafanya watanzania wajinga kwa kutuaminisha uhuru wa Zanzibar wa 1963 ulikua batili. Ila kwa bahati mbaya wapo wengi wanaomini ujinga huo.

Dunia nzima iliutambua na inaendelea kuutambua uhuru huo isipokua CCM tu
 
bopwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2013
Messages
1,700
Points
2,000

bopwe

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2013
1,700 2,000
Naikumbuka siku hii kama jana vile.

Nilikuwa na umri wa miaka 11 na vitu viwili vitatu ndivyo vilivyonasa kwenye kichwa changu.

Kwanza ni kumuona Mzee Abdulrahman akitoka nyumbani kwake kashika sanduku anaingia kwenye taxi anawaaga majirani kuwa anakwenda uwanja wa ndege safari Zanzibar kwenye sherehe za uhuru.

Mimi na mwanae somo yangu Mohamed Kitunguu tuko barazani kwake na rafiki zetu wengine tunacheza.

Ilikuwa mchana Mtaa wa Gogo moja ya mitaa mifupi sana Kariakoo.

Kitu cha pili kinachonikumbusha siku hii ni nyimbo ya Sal Davis, "Ayayaa Uhuru," ambayo kutwa nzima ilikuwa ikipigwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC)ikihanikiza sherehe za uhuru wa Zanzibar na Kenya.

Kwetu sisi watoto tunanyanyukia kuingia "teens,"muziki wa Sal Davis ulikuwa ukitutia wazimu.

Tunamsikia Sal Davis akiimba na radio katika kila nyumba mitaa ya Dar es Salaam zimefunguliwa, "full blast," "Ayaayaa uhuru, ayaayaa Kenyatta, Nyerere, Obote, Shamte..."

Sikumbuki vyema maneno ya nyimbo hii mpangilio wake lakini majina ya viongozi wa Afrika Mashariki yanatajwa na kwa Zanzibar jina la Waziri Mkuu Mohamed Shamte linasikika.

Sauti ya Unguja nayo ilikuwa imefungulia vinanda vya taarab ilmuradi mji ulikuwa furahani.

Katika umri wangu ule mdogo wa miaka 11 sikuweza kutambua kuwa ukubwani Sal Davis atajakuwa rafiki yangu mpenzi na nitakuwa jirani yake milango ya "appartments"zetu zikiangaliana mimi nikiwa mpangaji wake na wake zetu watakuwa mashoga.

Si haya tu nitamkalisha Sal Davis kitako na tutaandika mswada wa maisha yake na mengi tutafanya pamoja nyumbani kwake kwengine Zanzibar na Mombasa Nyali Beach.

Turudi kwenye uhuru wa Zanzibar na nyimbo ya Ayaayaa Uhuru na Waziri
Mkuu wa kwanza wa Zanzibar Mohamed Shamte.

Sal Davis amenieleza kuwa wakati nyimbo yake hii iko juu kabisa kwa kupendwa kote Afrika ya Mashariki, mapinduzi yakatokea Zanzibar na serikali ya Mohamed Shamte ikapinduliwa.

Nyimbo yake kwa kuwa ilikuwa imemtaja Waziri Mkuu wa Zanzibar Mohamed Shamte ikapigwa marufuku Tanganyika na Zanzibar.

Kipindi hiki mauaji makubwa yalikuwa yamepita Zanzibar na baadhi ya viongozi wa iliyokuwa serikali ya Zanzibar wakawa vifungoni.

Baadhi ya viongozi hawa waliofungwa na kutumikia vifungo vyao katika jela za Tanzania Bara nilikuja kufahamiananao kwa karibu sana ukubwani kwangu na nilijifunza mengi kutoka kwao.

Ilikuwa katika Mtaa huu wa Gogo unapokutana na Mtaa wa Mchikichi kwenye baraza ya nyumba ya akina Abdul Kigunya kulipokuwa na barza maarufu ya kucheza bao ndipo kwa mara ya kwanza nilipomuona Abdallah Kassim Hanga.

Hii ilikuwa mwaka wa 1964 na muungano wa Tanganyika na Zanzibar tayari.

Hanga akija hapo kila jioni tena akitembea kwa miguu akija kucheza bao.

Sifa zake kama mmoja wa viongozi wa mapinduzi zilikuwa zimeenea na picha zake katika gazeti la Ngurumo na Mwafrika zilikuwa hazipungui.

Nasi kwa ule udadisi wa kitoto tukimuona pale tutajisogeza kwenda kumshangalia hadi tujazane na wakubwa watuone kero watufukuze.

Haikunipitikia kamwe kama siku itafika nitatafiti historia ya mzalendo huyu pamoja na historia ya "pop star,"mkubwa kupata kutokea Afrika ya Mashariki Sal Davis na nitaandika historia zao.

Inasikitisha tu kuwa katika uhuru wa Zanzibar na mapinduzi yaliyofuatia Hanga aliuawa kikatili na katika utafiti nilikujakujua mengi yaliyopitika.

Si yeye tu.

Marafiki wawili wa baba yangu Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala na wao hawakusalimika.

Nimeishi katika historia hii na ndani yake nimejifunza mengi.
Zaidi ni kule kufungwa Tanganyika kwa walokua mawaziri wa serikali ya Zanzibar.
Kisheria haikua sahihi na Ukweli wale hawakua na makosa yoyote kustahiki kufungwa bara na wengine kuuliwa.
Hii inathibitisha kuwa Zanzibar hawakufanya Mapinduzi bali walipinduliwa tena na kuingizwa kwenye nakma nyengine kubwa kuliko ya Muingereza na Maarabu
 
Forum statistics

Threads 1,380,548
Members 525,822
Posts 33,774,377
Top