Wanajamvi kwanza natanguliza kusema kuwa mimi siyo mwana siasa wala sijawahi kugombea cheo chochote ila nimesoma elimu ya siasa, Siasa na Political science ila sijawahi jihusisha na siasa.
Visiwa vya Zanzibar/Pemba wote tunafahamu vilikuwa chini ya ukoloni wa Mwingereza na pindi vilipojitawala, waliowengi hawakukubaliana na matokeo ya kura hivyo yakatokea mapinduzi. (Kama ingekuwa bara kukataa na kuingia barabarani wee). Yalikuwa mapinduzi ya kumwaga damua ambayo kila mwenye kuweza kuingia kwenye archive ya BBC au Utube utaona kilichotokea wakati wa mapinduzi. Unaweza kuona jinsi miili yawatu ilivyokuwa ikielea baharini.
Bara tulipata uhuru kwa kalamu kama alivyoeleza marehemu Asha wakati wa katiba kuwa uhuru wao si wa kalamu. Ina maana alikuwa akitunanga sisi wabara kuwa tuliupata kwa kalamu. Alisahau kuwa hao walioenda kuwapa tafu akina Okero na wengine waliandaliwa huku bara.
Ikifika wakati tukubaliane kuwa Ili bara iwe huru na salama inahitaji Zanzibar na Pemba salama. Je salama kwa kuwa chini ya CCM au salama kwa kuwa na serikali inayokubalika? Je kutumia jeshi na nguvu nyingi kulinda Muungano kutatusaidia au ndo tunajijengea maadui wengi?
Maadui gani tunawajenga kwanza: Siyo nchi za Magharibi sababu hizi nchi ndo zinaogopa Zenj kutua mikononi mwa Alkaida, Alshabab na Shia/Sunni conflict. Wenyewe wako tayari kubaki hivi tulivyo ila demokrasia ichukue mkondo wake. Kama CUF ingeshinda kihalali haiwezi kufurukuta kuanza urafiki na wakoloni wa zamani ambao hawajawahi saidia chochote tangu wafukuzwe. Wangependa haki zao za msingi ambazo tulizikataa kwenye muungano na zisingeathiri ujirani wetu kama ilivyo Uganda walijiunga Jumuia ya kiislam na walifaidi wakati wa Rais wa Libya kabla hajauawa.
Je Zanzibar/Pemba iko tayari kukataa misimamo ya alkaida, Alshabab na ISS pamoja na migongano ya kiitikadi kati ya Shia na Sunni? Naamini Zanzibar/Pemba wanaweza kuwa huru kama wakiaminiana na wale mazalia ya watumwa kuamini kuwa utumwa hakuna tena na ile chuki na woga wa kusemana tuliowachinja 64 walati wa mapinduzi watatugeuka hali wakijua kuwa wao ni wengi hawana cha kuogopa bali jenga taifa jipya lenye kujitegemea na usawa wa kila hali bila kuwa tegemezi wa nchi jirani ambayo imewalea mpaka mgongo umeota sugu. Nawakilisha. Kama nimesema siyo naomba kukosolewa.