Uhuru wa wachunguzi huru

Uhuru wa wachunguzi huru

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,070
Reaction score
136,458
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.
 
The UK has a budget of $1.04 trillion. The US has a budget of over $3.8 trillion. They can easily afford the cost of sending Scotland Yard or FBI for few weeks to conduct an independent investigation. Also, to receive money for services rendered to a poor third world country would be shameful for U.K. or U.S.
 
Jambo la muhimu waruhusiwe kwanza wafanye huo uchunguzi.

Kitendo cha serikali kukataa huo uchunguzi huru unaleta picha gani ilihali vyombo vyetu vya usalama hadi sasa havijafanikiwa kukamata hao wasiojulikana japo namba za Nissan Patrol zimetajwa.

Uchunguzi huru uruhusiwe, matokeo yana sehemu mbili(positive & negative) na hayaepukiki
 
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
 
Huu ugumu unaouweka hapa kuhusu uchunguzi huru ni mwendelezo wako wa kuhakikisha muhusika anayefahamika hatajwi hadharani kwani kwako ni jambo litakalokufedhehesha sana.

Simply huna jipya zaidi ya jitihada zako za kuhakikisha ukweli haufahamiki. Usipoteze muda kile ulichoona ni sahihi kumkuta Lissu kimemkuta full stop.
 
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.
Kila mtu mwenye akili anajua kilichotokea kwa hiyo hata ukijaribu kuisafisha vipi ccm ni kazi bure, ccm wananuka damu za watu
 
Kuna mda hutumiagi akili. hilo Ni changamoto? Ata mashahidi wangekuwa wamekufa upepelezi ungefanyika na wahusika wangepatikana think out of box.
We ndo hujatumia akili! anachomaanisha huo upelekezi ungekuwa huru kiasi gan kwa maana ungeweza kuegemea kwa upande uliowaleta na kuwalipa, ungeanza hapo kujadili
 
Mkuu uwezo wa wanaccm kufikiri vizuri ni mdogo sana ndiyo maana wakikosa nguvu ya hoja wanakimbilia kwenye matusi na mauaji
 
We ndo hujatumia akili! anachomaanisha huo upelekezi ungekuwa huru kiasi gan kwa maana ungeweza kuegemea kwa upande uliowaleta na kuwalipa, ungeanza hapo kujadili

Una moyo!

Majitu mengine wala hayahitaji kueleweshwa.

Ni ya kuyaacha tu.
 
Mi nadhani suala la nani anayelipa sio ishu naamini kwa sababu watakaokuja ni professionals watafanya kazi accordingly na isitoshe watatoa vielelezo ku back up their findings!
 
Back
Top Bottom