Uhuru wa vyombo vya habari

Uhuru wa vyombo vya habari

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
Trump amekalia kiti moto!

Ndio jamaa hahemi kina anachofanya vyombo vya habari vinaripoti. Kawekewe tume za uchunguzi, wapelelezi wa kujitegemea, majaji wa kupinga amri zake. Maazimio yake hayapiti bungeni. Yaani tafrani tupu.

Lakini pamoja na yote hayo huwezi kumtaja kiongozi mmoja ukafananisha upinzani wake kwa Trump na upinzani wa wapinzani wa rais Magufuli.

Huyo Hillary kapotea sijui yuko wapi. Mara moja moja vyombo vya habari vikiibua kali ya Trump anaweza na yeye akaleta neno moja la kumcheka Trump.

Hakuna kiongozi wa upinzani ambaye anaitisha kikao na waandishi wa habari au wananchi akawaambia wananchi mbona siku hizi mmezubaa hamfanyi fujo. Hakuna kiongozi anayefanya kikao kisichoeleweka ni darasa la shule au mkutano wa siasa na kuwaambia wananchi wote wenye akili timamu wampinge Trump.

Vyombo vya habari vya Tanzania badala ya kutafuta habari kwenye vyanzo vinasubiri viletewe habari na viongozi wa upinzani.

Kama Magufuli ameajiri jamaa zake serikalini hiyo ilikuwa ni stori ya wiki nzima kwenye vyombo vya habari. Na vilitakiwa vitoe ushahidi. Stori ya hivyo ikiletwa na kiongozi wa upinzani hatujua ukweli wake.

Kama ni stori ya Acacia waandishi walitakiwa wafike kwenye machimbo waripoti kinachoendelea. Kama rais wa Acacia alikuja Tanzania waandishi wangeweza kumuhoji. Kama boeing imetuuzia ndege kanyaboa, boeing wanajulikana walipo. Habari kamili itafutwe. Waandishi wa habari huenda vitani kutafuta habari.

Rais anapoamua lake ni haki ya wanaompinga kumpinga bungeni wakishindwa basi.

Obama kapitisha ndoa za jinsia moja. Hakukutokea mpinzani aliyesimama kuwaambia wananchi waipinge serikali kwa juhudi zote. Acha watoto wanaopewa mimba shule. Leo hii bunge la Marekani linajadili kufuta sheria ya afya za wananchi wa hali ya chini lakini ni kwa hoja.

Tunapoiga tujue tunachoiga na maadili na mipaka yake.
4ea648218d559fc8cdb2205ba27e202a.jpg
 
unataka vifungiwe, tatizo nani atamfunga paka kengere! Usije niulize paka ni nani, huu ni msemo wa kiswahili
 
Marekani sio sawa na Tanzania mkuu.

Tanzania, rais wa nchi ni mungu. Anaabudiwa kuanzia bungeni, mitaani hadi mahakamani.

Mihimili haipo huru kama mahakama na bunge kulinganisha na marekani.

Wasomi wa marekani wanasimamia kile kilicho sawa na wanachoamini ni sawa. Wasomi wa tanzania ni waganga njaa. Wanasubiri kufukuzwa na sio kujiuzulu.

Wananchi wa marekani wanajua haki zao. Wananchi wa tanzania wengi ni mamburula.
 
Usichukulie wamarekani wote wamesoma. Historia imewafanya viongozi wao watambue vurugu za kisiasa mwisho wake wanakosa wote.
 
Back
Top Bottom