Mwalimu Mkuu
Member
- Dec 26, 2010
- 62
- 39
Heshima kwenu Wakuu!
Nimejaribu kusikiliza wimbo wa Diamond mara kadhaa has a baada ya kusikia sakata lake na Gwajima.
Kuna vitu kadhaa nimejifunza.
1. Wa Tanzania tulio Wengi tunapenda mipasho. Tunapenda kusikiliza stories ambazo hatuhangaika kutafuta ukweli wake. Tunaamini kwasababu fulani amesema basi itakuwa kweli, kama sivyo basi ajitokeze akanushe. Si kila mtu anaweza kujitokeza mbele kukanusha. Na pia Hata ukikanusha wapo watakaosema anajitetea tu.
Well, Kuhusu wimbo wa Diamond "nimeamua kukaa kimya" Kuna mambo yananipa shida kidogo kuelewa.
1. Kwa nini Askofu Gwajima amehamaki kiasi hicho, Hata kusema atamgeuza Diamond kuwa maji? Je aliyoyasema Ni Uongo? Hakuna mgogoro kati yake na Makonda? Gwajima amewekwa ndani na Makonda na alipotoka mara kadhaa amesimama mimbarani akimshambulia Makonda. Je Kuna ubaya gani mwimbaji ambaye anatumia sanaa yake asielezee yanayotokea katika jamii yake? Au Kuna sehemu amekashifu?
2. Mtu mwingine aliyetajwa japo si kwa jina Ni Mangi Kimambi. Naye ameibuka kumshambulia Diamond kwa kumtaja kuhusika kukoleza ugomvi baina ya Gwajima na Makonda. Je Kuna Uongo katika hilo pia? Kama mtu anafuatilia sakata hili ataelewa mchango wa Kimambi katika hili je kosa la msanii Ni Lipi hapo?
3. Najaribu kulinganisha wimbo huu wa "naamua kukaa kimya" na ule uliovuma mpaka kuohusisha serikali unaojulikana kama "wapo" dhana ile ile ya haki ya kujieleza Ni kwa nini mmoja apate support kulinda haki yake ya kutoa maoni kwa jamii ile ile na huyu mwingine akaonekana anatakiwa kuomba radhi kutumia haki hiyohiyo?
Hebu nenda sikiliza wimbo wa Diamond vizuri bila kuwa na urazini (biased) kisha fanya hukumu iliyo ya haki.
Naogopa tunaweza kuwa na Watu tunaowajenga kuwa miungu kwasababu ya mazoea au ukaribu nao nasi. Vinginevyo hawana chochote zaidi ya wanadamu wengine. Sifa, uweza na nguvu zinabaki kwake Mungu muumba wa mbingu na ardhi. Pekee hakosei wala hachunguziki.
Siku nyingine nitakuja na uzi unaoonesha jinsi wa Tanzania tunavyofanya character assassination kwa Watu wetu waliotuletea heshima kubwa nje ya mipaka yetu kwa kutumia funzo dhima (case study) ya;
1. Prof. Muhongo
2. Prof. Tibaijuka
3. Ndg. Tido Muhando
4. Ndg. Jenerali Ulimwengu
5. Ndg. Salm Ahmed Salm.
Wasalaam.